Huduma ya supa cheka, vodacom inawalaghai/inawatapeli wateja wake?

mwanaasili

New Member
Apr 2, 2012
4
3
Vodacom imeanzisha huduma ya SUPA CHEKA ambayo wanadai kuwa inakupa muda wa kuongea, SMS na internet bandwidth kwa saa 24.

Cha ajabu ni kuwa unapojiunga kwenye huduma hiyo, bila kujali umejiunga saa ngapi, unatumiwa SMS kuwa utumie benefits hizo kabla ya saa 5:59 usiku. Ninajiuliza masaa 24 ya vodacom yanahesabiwa vipi.

Napenda vodacom wajue kuwa ushindani wa biashara unahitaji kuwa muumgwana Hass kwa wateja Wako. Mimi nilitegemea kuwa SUPA CHEKA ni jibu la Tigo X-TREME. Lakini sasa wakati Tigo wanakupa saa 24 za ukweli toka unapojiunga, vodacom wanafanya kutuvunga.

Ninashauri huduma itangazwe mama vile inavyotolewa kwa Nia njema kuwa atakayeipenda ataitumia lakini sio kutoa matangazo ya ulaghai halafu huduma inakuwa ndivyo-sivyo.

Ninaomba Vodacom wajirekebishe!
 
lakini mimi nimeipenda dak 30, sms 100 na internet 50mb tatizo ni tangazo wangesema kwa siku na siyo kwa saa 24..
 
Kama unataka ufaidi kwa masaa 24 then jiunge saa sita kamili usiku.

Kwangu mie dk 30, sms 100 na 50MB kwa tshs 400 sina cha zaidi cha kuidai voda.

Kazi ni kwako!!
 
Watu bana hawana fadhila.
Cheka zilizopita haijalish ulijiunga mda gani mwisho wa cheka ilikuwa 16:59.Leo wameongeza hadi 23:59
mfanyiwe nn mridhike.
"Ama kweli bora ile kuliko hii"
VODACOM KAZI NI KWAKO.
 
wee,hao jamaa ni aibu,wana bando yao fulani hv inaanzia saa nne usiku hadi asubuhi unakatwa sh.200,unlimited,ina speed hatari,ma-you tube n line free bila kustuck,unadownload uwezavyo,cha kuomba usiwe na usingizi tu
 
Bora mhamie Zantel kwa habari promosheni;kuliko Super cheka,ambayo ni usaini mtupu !
 
Tsh/=400, unapata dakika 30,sms 100 kwenda mitandao yote,MB 50..Unataka nini tena.? Kazi ni kwako.!
 
wee,hao jamaa ni aibu,wana bando yao fulani hv inaanzia saa nne usiku hadi asubuhi unakatwa sh.200,unlimited,ina speed hatari,ma-you tube n line free bila kustuck,unadownload uwezavyo,cha kuomba usiwe na usingizi tu

Bando fulani ndo ipi hiyo?
 
Ni jambo la aibu kuwa wateja wa makampuni ya simu wanafikiri kuwa hizi huduma ni fadhila. Hizi sio fadhila, sana-sana zinaonyesha ni kwa kiwango gani tulivyokuwa tunavunwa kabla ya hapo.

Kwa kila huduma inayotolewa hawa operators wanauhakika wa faida nono. Usifikiri ni fadhila, kwamba eti Vodacom satakubali kupata hasara eti ili wewe mteja ufaidi - hats siku moja. Hii huduma imekuja mama majibu kwa Togo xtreme.

Ninachowaomba ni uungwana Tu - waseme "publicly" kuwa ni huduma inayoisha saa 5:59 usiku halafu mtu ajipange mwenyewe; au waseme ni huduma ya saa 24 na waiweke hivyo. Hiyo ndio biashara ya kiungwana.
 
Mwenye Uzi bora umeliona hilo hawakupi hizo dk wala internet hizo bytes wanazoahidi unasurf tu kidogo unaona connection lost kuashiria kifurushi kimeisha tofauti na tigo extreme. Unaongea hadi sikio linapata Joto na haiishi
 
Hii supa cheka imenifanya ninunue voda, ila swala lao la muda wanatakiwa warekebishe iwe masaa 24 ya ukweli,nalazimika kujiunga saa6 usiku. pia voda ni safi maana 10mb zina nguvu kuliko 50mb za tigo ambazo most of the time no connection.
 
Voda wastaarabu,hata ukiangalia huduma zao huwezi kuzilinganisha na za tigo na airtel,kama unaona vipi hamia airtel au tigo ili wakiona wateja wanapungua watalegeza tu
 
Voda wametangaza ofa yao ya supa cheka inaisha saa 5 na dka 59 uciku.. Ukijiunga saa 6 uciku c ndo inakuwa 24 hrs..! Mnataka nini tena..? Mnawalazimisha watoe ofa mnayotaka nyie..? Ndio maana kuna ushindani na makampuni mengine.. Kama unaona wanakubana unajimuvuzisha kwa kampuni nyingine.. Ninachopenda ushindani Tanzania ni kwenye mawaciliano tu ya cimu na wala sio kwenye mafuta au huduma nyingine..
 
dakika za package za ofa kwa mitandao yote pia inahesabiwa kiutata. Hii nimei-note Tigo (Extreme) na Voda (Cheka). ukiongea less than or equal to 59 second hiyo iko counted kama dakika 1 mfano sekunde 5, au 22 au 48 inahesabika kama dakika moja. Pia sekunde 60+ but less that 120 ni sawa na dakika mbili mathalan dakika moja na sekunde 7 hii ni sawa na dakika 2. Kwa maantiki hii cummulatively kwa siku unaweza kuongea sekunde 700 kwa kukata kata ikahesabika ni dakika 30 (sekunde 1,800). ukiuliza unaambiwa 'Vigezo na Masharti Kuzingatiwa'
 
Back
Top Bottom