Huduma ya kutafuta Kazi kwa kutumia Simu yazinduliwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma ya kutafuta Kazi kwa kutumia Simu yazinduliwa Tanzania

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by justdoit, Sep 2, 2009.

 1. j

  justdoit Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Chini ya Uangalizi wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kupitia wakala wake wa Ajira (TaESA), Callix InfoTech ikishirikiana na Push Mobile Media Ltd imezindua rasmi huduma ya “PATA KAZI” ambapo watu wataweza kupata kirahisi na kwa unafuu nafasi za kazi nchini kote kwa kutumia simu zao za mikononi wakati wowote na popote pale walipo.
  Huduma hii ni kwa wateja wa Vodacom, Zain na Tigo. Uongozi upo mbioni kushirikiana na Makampuni mengine ya simu.
  Kufaidi urahisi wa huduma hii mtumiaji atahitajika kujiunga kwenye kundi au aina ya kazi anayotafuta halafu baada ya hapo ataweza kupata taarifa za kazi anayohitaji mara kwa mara mpaka atapopata au atapohitaji kujitoa kwenye huduma hii.Kwa mfano kujiunga Andika neno Kazi au Ajira acha nafasi ikifuatwa na jina la kazi unayotafuta halafu utume kwenda kwenye namba 15522.Mfano:Kazi Dereva kwenda namba 15522. Kujitoa andika Kazi Ondoa kwenda kwenye namba 15522.
   
 2. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huu ndo wizi huu. Mnachotaka ni kukata hivyo vipesa ambavyo mtu atatumia kuandika sms, sijui 30 au 500, na mwisho wa siku mnatajirika kwa kupitia watanzania hawa maskini. shame !
   
 3. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Haya ni maendeleo mazuri ila sisi bado hatujafika huko. Kuna mambo mengi sana naona tunaruka. Naona wahusika afadhali wangeanzisha vitu kama Job centres kwenye mikoa au wilaya kusaidia watu kupata kazi baadala ya kuwalia pesa zao kwa kutumia SMS!!
   
 4. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0

  Kwa nini wasidesign site mfano wa monster.com ambako waajiri watatangaza nafasi za kazi na wakati huo huo kubrowse resume za watu wanaotafuta kazi. Vivyo hivyo wale wanaotafuta kazi wanaregister bure na kupost resume zao na pia kuweza kubrowse nafasi za kazi ambazo zimetangazwa na waajiri.

  Kwa kutumia website wanatengeneza pesa kutoka kwa wale wenye nazo ambao ni makampuni yanayotafuta wafanyakazi na kwa kutumia matangazo. Hii ya kutuma text message ni njia ya kunufaisha wao, say nafasi 2 wanatuma watu laki moja hapo ni nani ananufaika? Chances are watu wataendelea kutuma hata baada ya deadline.

  Sasa hao waombaji wakishatuma hizo text message pale watakapotumiwa hizo nafasi za kazi hiyo message itainclude details za kazi, mfano job description, requirements, contact details na deadlines za kusubmit resume au ndio tena watatakiwa kwenda kununua gazeti? Kama watatakiwa kununua gazeti je hapa hawajapigwa bao mara mbili?
   
 5. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wizi mtupu,
  hiyo ya kujiunga inafanya kazi,ila hiyo ya kujiondoa,hasa baada ya kuona ujumbe mtu anaotumiwa ni tofauti na kazi aliyoomba,haifanyi kazi,so inabaki mteja anazidi kuibiwa pesa yake ambayo anajitahidi kuidunduliza ukizingatia hana kazi ya uhakika
   
 6. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wakiisha pata pesa zetu, watakwambia mfagiaji awe na diploma, kama huna sifa hiyo kula kona
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Sep 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tembelea www.naombakazi.com utapata nafasi za kazi za kila siku toka afrika ya mashariki
   
 8. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Naomba tuwekane wazi hapa. Hii program inamilikiwa na nani - Wizara an TaESA? na Push Mobile nafasi yake ni nini hapa - kama mobile agregator au ndio mwenye hii product?

  Kama ipo chini ya wizara, na lengo lao ni kusaidia wananchi - embu tuambie ni kiasi gani hawa watu watakuwa wanatozwa kwa hii huduma - alafu tuone kama lengo ni kusaidia watu wasio na ajira au kutumia hali yao ya umasikini kuiba hata kile kidogo walichonacho?

  Hata hivyo, ajira nyingi za hapa bongo, hasa zile za serikalini, zinakuwa na watu tayari wakati zinapotangazwa. Huo ujumbe hata ukimfikia mtu utakua una msaada mdogo sana ukizingatia tayari ameshaliwa hela kibao.

  Pili, kama alivyosema mndee, how would you get job descriptions? Single SMS is limited to 160 chars, ambazo hazitoshi kutoa job descriptions, deadlines, minimum qualifications etc -- Hata ukiunganisha SMS tano, I am sure zitakuwa hazitoshi kutoa information kamili.

  Pia nimeshangaa sana kwanini hujasema kuhusu gharama zenu - hii inanipa wasiwasi kuna uwezekano wa kutotendeana haki hapa!

  Waoneeni huruma masikini, tayari wameshapata taabu za kutosha. Hamna aja ya kuwanyonya zaidi ya hapo!
   
 9. j

  justdoit Member

  #9
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwanza naomba mniwie radhi kwa kutoweka info za kutosha. Na pole kwa kushindwa kuielewa hii huduma pamoja na info zote nilizoziweka.

  Hii service ni ya Callix Infotech ikishirikiana na Push Mobile kukamilisha lengo.Wakala wa Kazi TaESA wao wanaangalia tu kama kuna mapungufu yoyote wanasahiisha au wanatoa adhabu. Tuna kibali cha kufanya hii huduma

  Lengo hapa ni kuwafikia watanzania wote kwa mda mfupi na kwa bei nafuu. Kujiunga kwenye huduma hii ni shilingi 250 na baada ya hapo kila nafasi ya kazi itayotumwa itakuwa ni shilingi 150 pekee.

  ukilinganisha na gazeti ambalo ni kuanzia mia 300 mpaka 500(yenye nafasi za kazi mara kwa mara),na pia kuna uwezekano ukatumia mia tano na usipate aina ya kazi ambayo unatafuta.Lakini kwenye huduma hii unatumiwa kile ulichokichagua tu na unapokuwa hauitaji tena unaweza kujitoa.

  Fahamu kwamba kuna vijiji ambavyo magazeti hayafiki kabisa na kama yakifika yanakuwa yanachelewa siku kadhaa.Lakini kwa kutimia huduma ya simu ambapo watanzania takribani milioni 16 wana simu sasa wanaweza kuipata huduma hii kwa urahisi na kwa bei nafuu kabisa.


  This service is Cheap,Fast and Easily Accessible!!!
   
 10. j

  justdoit Member

  #10
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mzee,

  Kwa taarifa yako kuna watu wanajiunga wanajitoa na baadae wanaiunga tena. Huduma hii imefanikiwa kulingana ufanisi wake na gharama yake ni nafuu sana. Kujiunga ni 250TZS na kutumiwa nafasi za kazi ni shilingi 150TZS na huwezi tumiwa zaidi ya kazi moja ndani ya siku moja. "Equal Opportunity to all Tanzanians"

  Kumbuka kuna watu ambao hawapati magazeti na kama wakipata yanakuwa yameshachelewa hata kwa siku nne na zaidi. Na vile vile grarama ya gazeti ni kuanzia shilingi 300 mapaka shilingi 500 na waweza kununua gazeti ukakosa aina ya kazi unayoitafuta lakini huduma hii inatuma aina ya kazi uliyochagua peke yake mpaka utaposema haitaji tena. Stop being negative.
   
Loading...