Wadau,
Heshima yenu. Mie naishi Arusha maeneo ya Maji ya Chai. Kwa wale ambao tunaishi wote hapa au wanalisikia ni kuwa ipo shida kubwa ya maji. Jitihada zangu zote za kuona kama naweza kupata maji mpaka kwangu zimeshindikana mpaka sasa.
Kwa sababu hiyo nimeona bora niamue kuuliza kama naweza kupata huduma ya kuwa naletewa maji kwa gari zile zinazotoa huduma hii. Kwa maana ya kuwa kila mwezi angalau lita 10,000 -15,000. Anayejua kama huduma hii naweza kuipata naomba anisaidie kunipa mawasiliano na bei inaweza kuwa ngapi kwa kiasi hicho cha lita/trip.
Natanguliza shukrani