Huduma muhimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma muhimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutekanga, Mar 22, 2010.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM, inajigamba kwamba ni chama kikongwe na kwamba itabaki madarakani milele. Sina tatizo na chama hicho kubaki madarakani milele, maana hata Banda, Bokkasa na Iddi Amin, walijitangaza kubaki madarakani milele. Hivyo hilo mimi sina tatizo nalo.

  Tatizo langu ni CCM pamoja na majigambo yote serikali yake, imeshindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi. Majigambo ya nini wakati watu hawana maji? Majigambo ya nini wakati watu hawana umeme, Majigambo ya nini wakati barabara zinazokwenda vijijini hazipitiki wakati wa masika? Majigambo ya nini wakati Jijini Dar-es-salaam, trafic Jam inatishia maisha ya kila mtu? Watu wanachelewa kazini, wanachelewa kurudi majumbani, wanavuta hewa chafu ya moshi wa magari. Majigambo ya nini wakati shule za kata hazina walimu? Majigambo ya nini wakati serikali inashindwa kutoa mishahara mizuri kwa wafanyakazi wake?

  CCM, imenunua magari mapya ya kusambaza nchi nzima, ili yasaidie kampeni na kuhakikisha CCM inabaki madarakani milele. Mbona badala ya kununua magari, CCM haikukumbuka kutumia fedha hizo kusambaza huduma muhimu kwa wananchi?

  CCM inaweza kubaki madarakani milele, nafikiri hili si tatizo. Lakini kama serikali yake itaendelea kushindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi, kuna siku wananchi watasema inatosha! Na wala huu si utabiri, bali ni hali halisi!
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uko sawa
   
Loading...