Huduma mbovu zinazotolewa sasa na benki ya CRDB

sinzahome

New Member
Apr 25, 2019
2
5
Mimi ni mteja wa Benki ya CRDB zaidi ya miaka 10 sasa, maana kwa ninavyokumbuka niko pale kama mteja wao tangu mwaka 2008,

Tangu nilipoijua CRDB mwaka 2008 huduma walizokuwa wanatoa ndio zilinifanya nijiunge na benki yao, ila kwasasa huduma wanazotoa zitanifanya niikimbie benki yao na kurudi kule nilikokuwa kwa maana kuna nafuu wa huduma bora za Kibenki kuliko hii CRDB ya sasa, Huduma zake kwa wateja zimekuwa mbovu kupindukia hadi kuna kuda namkumbuka DKT. CHARLES KIMEI, hadi kuwa najiuliza tuu hivi huyu mzee aliondoka na Benki yake au? Kama hali yenyewe ndio hii ya sasa sisi wateja tutakimbia wengi na kwa mtazamo wangu miaka 10 ijayo hii benki wasipo angalia inaelekea kufa kabisa.

HUDUMA MBOVU Mfano: Kadi za ATM za wateja wa CRDB zilizoisha Muda wake za tangu mwaka jana Novemba 2019 mpaka sasa Machi 2020 kwa wateja wao wa Tanzania nzima hawajapatiwa kadi mpya za kuendelea kufanya huduma za kifedha kwa kutumia KADI ZA ATM, ni malalamiko tuu kila siku kwa wateja ukienda Tawi lolote la Benki hiyo na majibu wanayotoa wafanyakazi ni hata wao hawajui hizo kadi zitakuja lini, mimi najiuliza Tuu Benki kubwa kama CRDB kweli Kadi za ATM tuu ndio zinawateteresha hivyo hii hatari.

Yako mengi tuu ya hiyo benki ila kwa sasa tuongelee hili linalokiki huko kwao ambalo kwa ukubwa wa CRDB Benki linanishangaza, kuna madudu kama kwenye mikopo, foleni kubwa benki kuliko hata benki Fulani Fulani zile tulizokuwa tunazilalamikia au kuzihama huko awali, n.k

Nadhani DKT. CHARLES KIMEI toka aondoke mwaka 2018 ameondoka na Benki yake maana huduma zimekuwa mbovu kupindukia tofauti na wakati wake alipokuwepo, na kinachonifanya niamini kuwa DR.KIMEI ameondoka na benki yake, ni tangu aondoke huduma za benki hiyo zimekuwa zinaporomoka kila siku iendayo kwa Mungu. Natamani DKT CHARLES KIMEI huko aliko sasa arudi CRDB hata Wiki 1 tuu aje kuweka mambo sawa maana hali ya Benki kwa sasa ni tete saaaaana.

Namshauri BW. ABDULMAJID NSEKELA awasiliane na DKT. CHARLES KIMEI ampe mbinu za benki alivyokuwa akiiongoza maana utendaji yeye wa sasa toka aachiwe kiti unaishusha Benki siku hadi siku

IMETOLEWA KWAKO na Mpenda Benki ya CRDB kimaendeleo.

Mlioko CDRB mna mchango gani?
 
Nimesubiri kadi yangu sasa wiki ya tatu,hawajanipa wanakuambia subiri.hizi benki zenye wateja wengi ni matatizo tu.hawajali wateja wao
 
Hivi hii karne ya 21 bado watu hamuishi kulalamika?

Tupo kwenye free market, kwanini msiende benki nyingine? na mabenk yapo mengi tu.
 
Ki uhalisia, 'every one care about their own interests' hata huyo Nsekela uliyomtaja hapo, usifikiri anajali chochote kuhusu wewe kupata huduma mbaya, anaangalia maslahi yake kwanza, huo ndo ukweli wa kwenye ubepari.
 
Wanasiasa wa CCM wanapoingia madarakani uhakikisha kila sehemu wanaweka watu wao ambao wakiamlisha wanataka pesa watapewa fasta

Ukumbuke serikani inakopa sana hii so usikute ndani na nje usikute Kimei alitaka watu wafate sheria sio wakitaka pesa kuchota tu ndio labda uyu akiambiwa tupe bilion 50 fasta anatoa na uwenda aliwekwa kimkakati.

Unakuwa na plan za kipumbavu unaweka mtu sehemu ili utimize haja zako bila kujua nyuma ya kioo unaua iyo taasisi pengine hata izo pesa utakazokuwa unazitaka kuna muda utafika hautazipata.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mimi nilienda kurenew card, nikatakiwa kulipia, mmoja akanitonya kadi ni ishu kwa sasa bora nisubr mpka patakapokaa sawa! Nkaondoka zangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bank zipo kibao nendeni huko hakuna usumbufu.
Ni rahisi kama ingekuwa unaenda kufungua a new account. Lakini kama ungelikuwa ndo umeshatumana majina zako huko na huko na accounts zako na hapa ndo unatumainia kupokea pesa zako. Utaenda bank nyingine gani?

Its easy sana kushauri hivo but practically it is very difficult. To ushari ingine.
 
Wakati wa kimei watu walikuwa wanalaumu ohoo kimei mkabila kajaza watu wa kabila lake, bora tu aondoke na watu wake safu ipangwe upya.

Haya kimei kaondoka na watu wake, haya sasa ipongezeni safu mpya ya uongozi kwa utendaji mliokuwa mnautaka
 
Nipo kwenye industrial ya banks indirectly, CRDB imeondoka na Kimei, CRDB ya sasa hivi full uswahili yaaani hapo trailer picha kamili bado, pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimpiga zengwe hadi akaamua kustaafu ila ukweli ambao baadhi yenu mmeujua saa hii hakuna CRDB kama ile ya Dr Kimei.

Bank ilikuwa unapewa high classic customer care ever in tz. Hata kwenye ufanisi umepungua kwa kiasi kikubwa mnoo mnoo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nime renew cadi baada ya wiki 3 naenda kuulizia naambiawa nitulie nitapigiwa simu. Nimeweka tageti zangu ikifika tarehe niliyopanga kama sijapata taarifa yoyote kuhusukadiyangu naanza kuhamisha mzigowangu taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom