Huduma mbovu MultiChoice Tanzania

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Niko hapa DSTV main office Dar es Salaam niko kwenye foleni kwa zaidi ya masaa mawili huku mbele yangu kuna wateja wanne tu wote tukihitaji huduma ya kulipia malipo ya mwezi kwa packages mbalimbali. Kwa kweli ni aibu na utendaji mbovu usio na tija wala umakini kwa mteja mmoja kuhudumiwa kwa zaidi nusu saa. Maswali na concenrns zangu kwa wahusika juu ya utatuzi wa tatizo hili;

1. Je billing server iko hapa Dar au J'burg na kama haipo hapa kwa nini wasideploy local server kurahisisha billing process?
2.Kwa nini wahudumu wenu hawana kauli nzuri kwa wateja au mmeajiri watu ambao they are not professionals?
3.Kwanini msiongeze vituo vya kulipia hapa Dar na hata mikoani maana huduma yenu ya kuilipia kwa sms haifanyi kazi ipasanyo?
4. Tunaomba mlifanyie kazi suala hili nasi tufurahie huduma zenu ambazo tunazihitaji sana.

Mteja aliyekerwa sana
 
Pamoja na huduma duni eti wamepamdisha gharama ya premium package kwa US$2???

Hiyo bei mpya imetoka SA, hawa wa hapa ni kufuata tu ya huko sauz... Back to the point, Multichoice Tanzania (hasa Dar office) wameonyesha mapungufu kwenye customer service hasa payment section ingawa pia wameintroduce payment through bank accounts (you can get them there) kwahiyo wana excuse ya kuanzia
 
Mkuu nadhani bongo wapo nyumba kwa kila hawana cha hiki wala kile maana kwanza unajuwa kusoma raha sana tena sana sasa kama hao waliokuwepo hapo au hao wafanyakazi wamesoma nadhani wasingeweza kuwajibu wateja wao maneno machafu yasiyokuwa na mpango ila hawajasoma ndio maana...........Lakini ndio bongo yetu hiyo ilivyo....Je hao kingereza kinapanda????
 
Ni kweli huduma zao mbovu na majibu ni mabaya na hawana kauli ya biashara,mtu unauliza kitu badala ya kukujibu anakuagiza kamuulize mtu mwingine,wakati yeye ana uwezo wa kulitatua,hii inasikitisha sana! hawa jamaa wanahitaji upinzani kama simu za viganjani,vinginevyo kwa kauli za leo tutakoma.
 
Nakushauri nenda Voda shop upate recharge voucher bila usumbufu huna sababu ya kwenda ofisi ya watu wasumbufu katika dunia ya sasa,ni kitendo cha dakika tano
 
ndio matatizo ya monopoly.hata hiyo mpesa bado wnachelewa ku-activate account baada ya kulipa! they are just crap!
 
Nawashukuru mmeona hayo, mimi pia nimeona haya:
1. Ukipiga simu unakula ujumbe hata pesa yako yote inakatika kabla ya kupata jibu.
2. Ukifanikiwa kuongea na mhudumu atakuzungusha hadi pesa yako iishe kabla ya kusaidiwa
3. Naamini wa mewanda sana kwa serikali na jeshi lake toka wametekwa na huduma yao hata RISITI ya kielektronia ya kupokea malipo na kuonyesha kodi yetu HAWATOI tena siku hizi.
4. Wameshindwa kabisa kuboresha picha, mvua kidogo sikirini inageuka viboma viboma.
 
Na mimi yamenikuta ya hawa DSTv (Multichoice), nimelipa tokea jana mchana lakini mpaka leo mchana huu hawajaniwashia niweze kuangalia. Simu yenyewe napiga tokea hiyo jana lakini zote hazipokelewi.

Hii ni customer service ya aina gani? Huduma zimeoza kabisa, hapa wakija wengine natoa kabisa na hiyo Decoder yao.

Kama kuna mtu wa DSTv humu, tuambie tupige namba gani ambayo inapokelewa ili tuweze pata hii huduma. Hela tunazolipa ni nyingi halafu hatuoni kitu.
 
Ni wakwanza kudisconect kama salio limeisha ila huduma zao we acha tuu! Tafta mbadala wasikuzingue lool
 
What to expect if watoa huduma ni girlfriends & boyfriends....wa viongozi ...yeah I mean boyfriends & girlfriends and not husbands and wifes. It is them bosses who matters most wateja comes second.
 
Na mimi yamenikuta ya hawa DSTv (Multichoice), nimelipa tokea jana mchana lakini mpaka leo mchana huu hawajaniwashia niweze kuangalia. Simu yenyewe napiga tokea hiyo jana lakini zote hazipokelewi.

Hii ni customer service ya aina gani? Huduma zimeoza kabisa, hapa wakija wengine natoa kabisa na hiyo Decoder yao.

Kama kuna mtu wa DSTv humu, tuambie tupige namba gani ambayo inapokelewa ili tuweze pata hii huduma. Hela tunazolipa ni nyingi halafu hatuoni kitu.

Piga 022 266 6751
 
Mie ndo yamenikuta kabisa, nimelipia through NMB mobile Leo zimeisha week mbili na sijawa activated nowise Leo, ukipiga simu hawapokei hata utambikie na huko NMB mobile wanasema subiri siku nne, kila ukipiga baada ya hizo siku 4, unaambiwa subiri tutakupigia. This is kichefuchefu pasee.
 
Tatizo la dstv ni kuokota ma miss vitongoji na waliomaliza miji na kuwaweka hapo cash section. Pana huduma mbovu sana hapo na wateja hawathaminiwi kabisa. Baraka clean up ur mess pls
 
Yaani I thought to be the disturbances are from we up-country customers kumbe mpk mjini,
mi mwenyewe nimekuwa nikisumbuka sana kurudisha view pindi nikatiwapo services zao, initially nilidhani wakikata kuwa credit imeisha ukilipa wanarudisha but hiyo theory hai-function; pia ukiwapigia kuwa nimelipia package yangu you will need to wait at least 2 mins ili uunganishwe; kiukweli wanaboa sn
 
Back
Top Bottom