Huduma Hospitali binafsi ni wakati muafaka kuangaliwa, Madaktari wengi ni part-time, inaumiza wagonjwa

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,488
3,263
Huduma za hospitali binafsi ni muhimu sana hapa nchini, kwani hospitali za umma hazitoshi. Hospitali kubwa hasa za mashirika ya dini yana maelewano na serikali (MOU) ambapo hupewa vifaa au nguvu kazi. Tatizo kubwa lilipo kwenye hospitali ni ukosefu wa mabingwa wa tiba. Huwatumia mabingwa toka hospitali za serikali.

Matokeo yake mgonjwa, mathalani alievunjika mifupa huweza kuwekwa wodini muda mrefu bila huduma akisubiriwa daktari toka hospitali nyingine. Ni jukumu la wizara ya afya kuliangalia hili. Wizara ya elimu kupitia TCU ilivifungia vyuo vikuu vingi, moja ikiwa ni kukosa wahadhiri wa kutosha na wenye sifa.

Ni vizuri wizara ya afya ikaliona hilo na kuzuia mfumko wa hizi hospitali zinazo pata mapato makubwa kupitia bima za afya kumbe hata hadhi ya kituo cha afya hazina.
 
Ukiacha Aga Khan hospitali binafsi nyingi huduma ni hafifu
Na madaktari wa kuazima hufanya kazi kama mamluki. Hujizungusha kuwatibu wagonjwa kwenye hospitali waliko ajiriwa na kuwashauri wagonjwa wawaone katika hospitali wanakofanya muda wa ziada.
 
Na madaktari wa kuazima hufanya kazi kama mamluki. Hujizungusha kuwatibu wagonjwa kwenye hospitali waliko ajiriwa na kuwashauri wagonjwa wawaone katika hospitali wanakofanya muda wa ziada.
Sure, baadhi huchukua wanafunzi wa udaktari vyuoni ili kuwalipa kiduchu
 
Back
Top Bottom