Huduma Bongo: TIGO yashikilia usukani, yaiondoa TANESCO kileleni

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,417
3,154
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, Tigo imeshikilia usukani wa biashara inayoongoza kwa kero kwa wateja baada ya kuibuka kuwa mshindi miongoni mwa biashara 31 zenye kero kwa wateja nchini .

Taarifa hii ni matokeo ya zoezi linaloendeshwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wenye lengo la kuboresha sekta binfasi nchini Tanzania hususani huduma kwa wateja.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO mkoa wa Dar es Salaam ambao katika mzunguko wa kwanza ndiyo walishikilia usukani wa kero. Wakiongoza kwa kero ya kukata umeme bila taarifa kitu kinadaiwa kuwa ni mgao.

Nafasi ya tatu imeendelea kushikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo imeendelea kushika nafasi hiyo katika mzunguko wa pili.

Hakukuwa na mabadiliko katika makundi mengine mfano huduma za usafiri wa anga ambapo mshindi amebakia kuwa ni Precision Air, huku katika huduma za kibenki zikiendelea kushikiliwa na benki ya CRDB. Huduma za ving’amuzi vya kulipia vyenye kero imeendelea kushikiliwa na Star Times waliopata kura 4 za ziada ukilinganisha na matokeo ya mzunguko wa kwanza.

Katika mzunguko huu biashara mbili zaidi ziliingia katika kinyanganyiro hicho ambao ni Kampuni mpya ya huduma za ndege ya Fast Jet na Dalalada inayofanya safari kati ya Mwenge na Kariakoo yenye nambari za usajili T 868 BHU.

Haya ni maoni ya wateja wa huduma hizi yaliyokusanywa kupitia akaunti ya
twitter Hudumambayatz na Facebook
group ya HUDUMA BONGO ambapo jumla ya kero 174 ziliwasilishwa na wateja toka mchuano uanze. Zoezi la kukusanya maoni haya linaendelea katika mzunguko wa tatu ambapo kauli mbiu ya ni “Sisi ndio waajiri wenu , huduma bora ni haki yetu”. Kero katika huduma na bidhaa mbalimbali za kulipia mfano afya, elimu, usafiri, benki, mawasiliano zinapokelewa na kutafutiwa suluhisho kwa maendeleo ya taifa letu. Kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea link ifuatayo www.twitlonger.com/show/k2j923
 
Last edited by a moderator:
vita vya telecom industry.
So far hakuna ahueni be it Tigo, Voda, Airtel....
Neutral observer!
 
Tigo wamezidi unajiunga XTRIME net hupati mpaka muda unaisha! Wanastahili!
 
vita vya telecom industry.
So far hakuna ahueni be it Tigo, Voda, Airtel....
Neutral observer!

Tigo wamezidi. Jana nilikuwa sina salio na sikupata vocha maeneo niliyokuwepo. Nikakopa. Leo asubuhi kabla ya kupiga popote nikacheki salio. Nilibakiwa na Salio kwenye akaundi ya niwezeshe. Nikahamisha pesa toka akaunti yangu ya tigo pesa na deni lote likalipwa. Muda huo huo nikacheki akaunti ya niwezeshe. Hamna hata senti 5. Wamechukua.
 
Ofisi za serikali especially wizarani na manispaa ni balaa. Temeke municipal kwa huduma mbovu ni next level
 
Nimeona mmeorodhesha viingi kwani afya sio huduma. Maana inavyokera hasa hizi hospital za kata hasa mwananyamala
 
Toka lini Tanesco ni sekta binafsi? Kama unapima ubora wa huduma katika sekta binafsi tanesco haiwezi kushika namba yoyote hapo, ipo katika sekta tofauti mkuu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom