Hubert Kairuki hospital kuna tatizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hubert Kairuki hospital kuna tatizo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mayenga, Feb 16, 2010.

 1. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,831
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Ni hivi majuzi nilimpeleka rafiki yangu wa kike hospital ambaye alikuwa na upungufu mkubwa wa damu.Kwa kuwa kabla ya hapo alikuwa tayari amepewa dawa za kuongeza damu,siku hiyo nilimpeleka purposely kumfanya check up ili kuona maendeleo yakoje.Kama ilivyo ada nilimwacha rafiki yangu akaingia consultation room,ambapo kulikuwa na daktari wa kiume.Kumbuka rafiki yangu huyu anatibiwa kwa kadi ambayo ni bima ya afya ya serikali.Cha kushangaza baada ya kutoka humo ndani na baada ya kuchukua vipimo vya haja ndogo,daktari alimwambia haoni kitu,na binti alivyotaka ufafanuzi kutoka kwa daktari,daktari akamwambia kama anataka kujua zaidi aende darasani,huku akionesha mwenye hasira na hali ya kutojiamini kw kile anachokisema.Sijui wana JF but I think we are softly dying!!!!!!!!!!!!
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Dk nani alikuwa?

  - Yule Mrusi
  - Kaganda
  - Muga Kairuki
  - Ndile
  - Mchomvu
  - yyy Kairuki (Binti)

  Je hilo linahusihana vipi na CARD (Health Insurance)?
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  M h ile nayo Hospitali? Mie rafiki yangu alikwenda pale akiwa anatatizo la kuona spotting wakati alikuwa mjamzito. Wakampima na kumwadmit wakisema inabidi asafishwe kizazi kwa kuwa ni miscarrage tayari. Shemeji (mume wake) akasita akamtoa na kumpeleka Muhimbili akachekiwa tena wakakuta kiumbe kingalipo hai na hakina tatizo lolote- leo bintiye ana miaka 5 Mzima wa afya!
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,831
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  I did not take trouble to note the name of the Dk,Baba Enock.
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180

  My friend you have to - anyone putting your friend's or relative life on the line should be responsible - ndiyo maana kwenye sehemu staharabu wafanyakazi huvaa ID - Hilo jibu alilopewa mgonjwa wako it is purely an irresponsible practitioner anayeweza kulitoa - Madaktari wana ethics zao na pia kuna Council inayohakikisha kazi zao zinafuata ethics hizo!

  Sio vyema tueendelee kukubali kufa! Madakatari wana-play a big role kwenye "un-timely deaths" - Kifo siyo mapenzi ya Mungu!
   
 6. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  HK Hospital ni majengo, lakini services zao zina walakini sana... Last year, sister wangu alikuwa mjamzito, akawa anahudhuria clinics zake pale, during those sessions, wakamwambia kuwa placenta imetangulia lakini wakampatia dawa za kutumia ili kurekebisha hiyo hali.

  Mimba ilipofika miezi 8 na wiki 2 akapata maumivu chini ya kitovu, ilikuwa usiku, akaenda pale hospitali kama saa 9 usiku, akawa admitted, akapewa dawa za maumivu, Dr wake (somebody Mchomvu) alipokuja asubuhi akamfanyia ultra sound akamwambia kuwa placenta bado imetangulia na mtoto ame-engage... (ameshaanza kushuka), lakini akamwambia kwamba watampa dawa nyingine ili mtoto arudi vizuri na placenta itarudi kama kawaida, ilipofika saa 6 mchana akaanza bleeding... akapelekwa theatre... baada ya hapo ni kumshukuru mungu tu kwamba aliponea chupuchupu baada ya kukaa theatre 5hrs hivi, ingawa mtoto hakuishi.... Dada alitolewa theatre saa 11 jioni akawekwa ICU, kwanza alikuwa hajazinduka lakini pia akawa bado anableed kiasi kwamba kitanda chote kikawa kimelowa damu. Ikabidi tumtafute huyo Dr wake, alipokuja akamfanyia procedure nyingine tena hapo (akamsafisha tena tumbo) ndo bleeding ikaacha, which seems hakusafishwa vizuri kule theatre.

  Tulipomuuliza Dr sababu, akasema ni bahati mbaya mgonjwa wetu alipata Placenta Abruption, they did their best kumuokoa na lililobaki ni kumuombea tu mungu. Mgonjwa wetu alizinduka kesho yake saa 2 asb akiwa amevimba mwili mzima, then baada ya siku 2 akaanza tena bleeding, Dr. akamwabia kuwa inawezekana uterus haikufunga vizuri, akampa vidonge 3 ameze, alipomeza tu akaanza kutetemeka kama mwenye kifafa, Dr mwenyewe (Mchomvu) akachanganyikiwa akakimbia, ikabidi aje Dr mwingine amuwekee drip, then after a while akatulia. Sasa huyo Dr wa pili akataka kujua ni dawa gani alipewa, alipoelezwa na nesi kwanza akashangaa, kisha akasema kwamba hizo dawa huwa hazimezwi, zinakuwa administered per rectum, na zime-react kwa sababu wamekosea matumizi.

  Kwa kweli, inasikitisha... lakini ndio Ma Dr's wetu

  Respect
   
 7. M

  Mundu JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  so scary... twende wapi sasa?
   
 8. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,mmmamaaaaaa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,634
  Likes Received: 9,138
  Trophy Points: 280
  Nina mashaka huyo kajanja ni doctor at all, hata a decent pharmacist inabidi ajue patient psychology 101. Hata mimi ambaye sijaenda Med School najua kuhusu Hippocratic oath.


  [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Hippocratic_Oath[/ame]
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Askofu jamani uwiiiii hivi hakuna sehemu tunawezapeleka malalamiko yetu kuhusu madr hawa? mbona tutakufa wengi?
   
 11. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  MJ1, kwa kweli inasikitisha. Nafikiri inabidi hizi qualifications za hawa wataalamu wetu ziwe reviewed, ama zitaclaim so many lives
   
 12. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Pole ndg na jamaa zangu mliokumbwa na hayo! Naomba nishauri kwa wahanga wa Kairuki hospital, japo ile ni hospitali binafsi lakini inatakiwa kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za wizara ya afya. Sasa ningewaomba wahanga wetu wapeleke malalamiko rasmi ikiwezekana kwa maandizi kwa Katibu Mkuu wizara ya Afya. Pale wizara ya afya kuna kitengo cha hospital inspection chini ya ofisi ya Mganga mkuu Kiongozi (CMO) nina hakika katibu mkuu atapeleka malalamiko hayo huko na uchunguzi wa kina kufanyika na hatua muhimu. Tufahamu pia tutakuwa tumesaidia/ kuokoa maisha ya watanzania wenzetu kwa uzembe na unprofessionalism ya hapo Kairuki.
  Km kuna mtu atataka zaidi juu ya namna ya kupeleka hoja hiyo wizarani tuwasiliane tu...
   
 13. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  jamani msiwe mnakimbia hospitali za serkali eti kwa kuwa tu mn kadi za matibabu na mzigo wa gharama hambeb wenyewe moja kwa moja, baadhi ni hatari sana.

  kuna mtoto mmoja alipelekwa aghakan akaambiwa amepungukiwa damu na akatakiwa kulazwa kwa matibabu zaidi, nadhani hela ilileta matatizo wakamnyima kitanda, kumbe ndio salama yake. mama mtoto akalazimka kumpeleka hospitali nyingine maeneo ya kariakoo, lahaulah. dk wa kariako alipomuona tu hata kabla hajampima alibaini kuwa ana minyooo. alimpa dozi ya minyoo, kwisha abari. toto siku mbili tu hilo mitaani buheri wa afya!!!!!!!!!

  si kwa kairuki tu, beware of fake doctors in private hospitals ................
   
 14. S

  Somi JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  mimi binafsi sijapata matatizo kutoka hospitali ya hubert kairuki
  nimehudumiwa vizuri kabisa
  kuna dokta kutoka ukraine anaitwa dr.valery markukha kama sikukosea jina lake , anasiku nyingi za kufanya kazi pale mikocheni.
  Ni dokta mzuri anatoa ushirikiano wa kutosha,aliwahi kunitibu.
  Kiujumla sijaona tatizo hebert kairuki hospital
   
 15. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Nashtukia sana mtu binafsi kuanzisha hospitali yake!
   
 16. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Waogopa fanyiwa biashara eeh?...kumbe mjanja wewe!
   
 17. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Hospitali Getini unakutana na KaburiKUBWAA ka Kariuki...not a very good idea na sidhani kama nikiumwa nitakwenda pale

  BAD OMEN

  the last thing nataka kuona nikiumwa na Kaburi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...