Katika kufanikisha adhma hii ya kuondoa simu zote zisizokidhi ubora zilizofurika sokoni na kuhakikisha watanzania wana uwanja mpana wa kupata simu bora za mkononi, Huawei Tanzania hivi karibuni wamezindua aina mbalimbali za simu za mkononi ili kukidhi mahitaji ya wateja wao kiuchumi na hali tofauti za maisha. Simu hizo ni kama GR5,Y6 Pro,Y6 Pro 4G ,Mate 8 32GB,Mate 8 64GB,Y3 lite,Y3 II,GR3,Y6, Y5C,Y3C,Shot X, Mate S, P8 64GB,P8 32GB,G8, P8 lite ,G play min,P9, na P9 lite. Kwakua soko la Tanzania ni pana na lina utofauti Huawei Tanzania wamejikita katika kuboresha vifaa vyao kwa kutenga asilimia kumi ya mapato yao katika kuwekeza kwenye soko ili kuongeza na kuboresha vifaa na simu za kisasa za Huawei. Huawei imeazimia kuwa kinara katika soko na kilele cha ubora.
Watanzania pia wamesisitizwa kuhakiki simu zao kabla ya katika ya mwezi Juni. Rai hii imetolewa na Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania, akizingatia kuwa watanzania wengi hawana elimu na uelewa wa kutosha wa namna ya kuhakiki simu zao.
“Ni muhimu sana kuhakiki simu yako unapoinunua ili kuwa na uhakika kuwa simu hiyo ni orijino. Ili mteja afahamu kuwa simu yake ni halisi au la, apige *#06# kwenye simu yeyote, atapata IMEI namba kisha atume namba hizo kwenda 15090 ili kupata ujumbe kama simu hiyo ni halisi ama la. Kwa simu za Huawei mteja atapokea ujumbe kutoka TCRA ukiwa na aina ya simu mfano (Huawei Technologies Co Ltd-Huawei Mate 8)”. Alisema Bwana Jacko.
Kwa mujibu wa TCRA takribani asilimia 40 ya simu za mkononi zinazotumiwa na watanzania ni feki. Simu feki sio tishio tu kwa wauzaji wa simu za mkononi bali pia kwa serikali na taifa kwa ujumla. Wakati Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imeazimia kuzima simu zote feki nchi nzima, Huawei Tanzania wanaona mpango huu upo sawia na mikakati yake katika kukabiliana na uhalifu, kuongeza mapato, kuwalinda wateja na simu zilizo chini ya viwango, kulinda matumizi ya fedha kupitia simu au miamala inayofanywa kwa njia ya simu pamoja na kuruhusu mawasiliano yaliyo bora nchini kote.
Kuna upotoshaji ulioshika kasi nchini Tanzania kuwa simu yoyote iliyo na kioo cha kugusa “touch screen” ni smartphone. Na hii ndio iliyopelekea kuongezeka kwa idadi ya simu feki katika soko la Tanzania. Kifupi smartphone inamuwezesha mtumiaji kupiga simu, ina sifa kama za kompyuta au laptop, uwezo wa kupata huduma za intaneti na kadhalika.
Pia tofauti na mawazo ya wengi kuwa bidhaa zote kutoka China ni feki au ni za kiwango cha chini katika ubora, Huawei kama bidhaa ya kimataifa imeendelea kuthibitisha msimamo wake kutengeneza bidhaa zilizo bora kwa wateja wake katika masoko yao yote. Akielezea hilo Bwana Sylvester Manyara Mkurugenzi wa Mauzo ya Rejareja, Huawei Tanzania anasema “Huawei inaongoza katika kutoa masuluhisho ya teknolojia na habari duniani, kampuni hii ilipokea zawadi ya ubora China, zawadi ya kiheshima kwa ubora wa bidhaa China, Machi 29. Huawei ilipata zawadi ya juu katika watengenezaji katika kitengo cha wateja na msimamo wa ubora. Kansela Yong Wang alitoa zawadi hiyo kwa Huawei katika ukumbi wa Great Hall jijini Beijing Machi 29 2016. Hiyo ni zawadi kubwa katika serikali ya China kwa ajili ya bidhaa zilizo na ubora. Bidhaa zilizo na ubora wa kipekee na watu wanaoonyesha mafanikio ya kipekee ndio wanaopewa zawadi hiyo.”
Akizungumzia ubora wa vifaa vya Huawei, Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja Mkazi wa Huawei Tanzania alisema “Huawei tunaamini kuwa ubora ndio fahari yetu. Zawadi ya ubora China ni alama ya msimamo endelevu wa Huawei katika ushindi. Kwa takribani miaka ishirini, Huawei kama Kampuni iliyojikita kutimiza mahitaji ya wateja imeweka mkazo katika uvumbuzi na ubora wa bidhaa. Huawei itaendelea kufanya Juhudi katika ubora na kutengeneza bidhaa zilizobora kwa wateja wetu duniani na Tanzania.”
Mahitaji ya wateja yamekua kiangalizo kikubwa katika shughuli za Huawei. Toka mwaka 1987, Huawei imeweka wateja wake karibu na inalenga kutengeneza bidhaa za ubora wa hali ya juu kwa namna ya pekee. Miaka ishirini na nane baadae, Huawei imezawadiwa kote China na nchi za nje kwa ubora wa viwango. Bidhaa za Huawei sasa zinapatikana zaidi ya nchi 170 na asilimia sitini ya mapato ya Kampuni yanatoka katika masoko ya nje.
Huawei imeweka mpango madhubuti wa huduma kwa mteja, unao wawezesha kupata maoni yote ya wateja wao kupitia namba ya simu, mitandao na maoni haya hutumika katika uvumbuzi na maendeleoa ya bidhaa. Katika safari yao ya ubora, mwaka 2014 Huawei ilishika nafasi ya 94 kwenye Interbrand Top 100 ya Kampuni zinazothaminiwa duniani, ikiwa Kampuni ya kwanza kutoka China kuingingia katika orodha hiyo. Mwaka mmoja baadae, Huawei imepata mafanikio Zaidi na kushika nafasi ya 88. Kiujumla, katika ripoti za hivi karibuni imeshika nafsi ya 47 na ikiwa na thamani ya dola bilioni 19.7. Hii imefanya Huawei kuwa kampuni ya kwanza ya kichina kuingia katika 50 bora. Kampuni ya Huawei pia imetambuliwa na shirika la Kimarekani US-based Reputation Institute kama Kampuni pekee ya kichina kuwa katika kumi bora ya Kampuni zinazoheshimika China.
Pamoja na ushirikiano kutoka TCRA, wadau wake na wateja wake, Huawei Tanzania imekua kwa kasi kubwa toka ilipoingia katika soko la Tanzania. Na msimamo wao wa ubora na kukidhi mahitaji ya wateja wao, Huawei itaendelea kudumu. Kupitia kampeni ya TCRA kuondoa simu zote feki na matatizo yanayohusiana na simu hizo, Huawei inaamini kuwa itakua bidhaa pendwa ya Tanzania.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ikiwemo Kenya, Uganda na Zambia ambazo zimechukua hatua kuzima simu zenye IMEI namba feki. Huawei ikiwa kampuni inayoongoza kwa simu za mkononi Tanzania inawaahidi Watanzania wote kupata na kufurahia simu zilizohalisi na kwa bei nafuu. Kampuni ya Huawei imetoa ahadi kuongeza ubora wa bidhaa kwa asilimia 30 kila mwaka. View attachment 355353