Hili ni duka la tatu la bidhaa hii katika jiji la Dar es Salaam, huku maduka mengine yakiwa yamezinduliwa katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya. Duka hili limekusudiwa kuleta hisia na mguso wa bidhaa za Huawei kwa wateja, na kuboresha kiwango cha huduma azipatazo mteja jijini.
Huawei Tanzania imejizatiti kuwa kinara katika bidhaa zya kisasa na zenye ushawishi zaidi Tanzania, kwa kuwapatia wateja simu zenye matumizi rafiki. Kampuni hii imedhamiria kuwa kinara wa bidhaa ya simu za kisasa Tanzania mwaka 2016. Kwa sasa Huawei Tanzania imeshika nafasi ya pili, ikiwa na hisa za soko za 22% kwa mujibu wa takwimu za robo ya kwanza ya mwaka 2016.
Akizungumzia kuhusiana na mkakati wa Huawei Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania, Ndg. Bruce Zhang amesema kuwa mwaka huu kampuni ya Huawei Tanzania imekusudia kuongeza wigo wa usambazaji Tanzania, ikilenga mikoa ya kanda ya Ziwa, kanda ya Kaskazini, kanda ya Kusini na kanda ya Kati.
“Tunampango wa kuongeza wigo wetu kutoka mawakala 250 tulio nao sasa mpaka kufikia mawakala 700, tunalenga kuwa na maduka 10 ya Huawei, maduka 20 ya mawakala wakubwa, 500 ya mawakala wa rejareja. Kampuni ya Huawei Tanzania imedhamiria kufikia 90% ya Tanzania.” Alithibitisha Mkurugenzi Mtendaji.
Kutokana na maduka haya, Huawei Tanzania inatazamia idadi kubwa ya watanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Akiongea na washiriki wakati wa uzinduzi, Mh. Raymond Mushi mkuu wa wilaya ya Ilala, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema, “ufunguzi wa duka la tatu la Huawei Tanzania hapa Dar es Salaam, ni udhihirisho wa kuongezeka kwa dhamira ya Huawei Tanzania kwa jamii.” Mh. Raymond Mushi pia aliipongeza Huawei Tanzania kwa hatua iliyochukua hivi karibuni ya kutambua mchango za mawakala katika mikoa yote na kuwatunuku vyeti pamoja na kuanzisha mpango wa motisha kwao.
Teknolojia imeendelea wakati wote kuchukukua nafasi muhimu ya jinsi tunavyowasiliana. Mawasiliano ya wanadamu yameendelea kubadilika kipindi hadi kipindi katika karne kadhaa. Huawei Tanzania imeleta vifaa vyenye teknolojia ya juu kabisa kama vile P9, Mate 8, GR5, GR3, Y6pro, Y3C, and Y3 Lite ili kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na uwanja mpana wa machaguo yao.
Akizunguzia kuhusu vifaa vipya vilivyoingizwa katika soko la Tanzania Bw. Zhang alisema “Msukumo wetu kwa wateja huenda mbali zaidi ya ubora wa bidhaa, kila ubunifu wa Huawei hutokana na ushirikishwaji wa wateja wetu na kuelewa mahitaji yao na uhitaji wa soko”
Katika kusherehekea ufunguzi wa duka hili la bidhaa za Huawei lililopo City Mall, Huawei Tanzania inatoa ofa ya punguzo maalumu la simu kuanzia tar. 14 hadi 20 Mei sambamba na zawadi mbalimbali zikiwemo fulana, spika zenye Bluetooth, na vifaa ya kusikilizia muziki masikioni vyenye Bluetooth pia.
Hivi karibu Huawei Tanzania imedhamiria kufungua maduka mengi zaidi na vituo vya simu vya huduma kwa wateja nchi nzima ili kuwahakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma bora na vifaa halisi vya Huawei na pia kutoka fursa nyingi zaidi za ajira kwa watanzania.
Huawei inatambua ushirikiano inaoupata kutoka kwa serikali ya Tanzania kwa miaka mingi sasa, kwa kuthibitisha dhamira ya Huawei katika upatikanaji wa vifaa orijino na kushiriki katika mkakati wa serikali kupitia kampeni ya TCRA ya kuondosha simu feki Tanzania. Huawei Tanzania inaendelea kuwaletea bidhaa orijino karibu zaidi kwa watumiaji wake kwa kufungua maduka yake nchi nzima na zaidi ya yote, tumeanza kutoa vyeti vya uthibitisho vya Huawei Tanzania kwa mawakala ili kujiridhisha kuwa wanauza vifaa na simu halisi za Huawei.