HR/CUF kukukubali kujiunga na Chadema kambi ya upinzani ni Hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HR/CUF kukukubali kujiunga na Chadema kambi ya upinzani ni Hatari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LAT, Nov 28, 2010.

 1. L

  LAT JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Naomba niende kwenye msingi wenyewe bila maelezo mengi... Kuhusu yaliyojiri kwenye mdahalo wa jana

  Baada ya Mh. Hamad Rashid kujibiwa hoja zake kwa kina na Mh. Freeman mbowe ampapo iliwekwa bayana kabisa kwamba kitendo walichofanya chadema ni Protest which is the right and freedom of expression na pia ilifanyika mbele ya watanzania wote na mkuu wao wa nchi wakiwemo wawakilishi wa kimataifa, jaji mkuu... na mwanasheria mkuu... Mh. Mbowe pia alifafanua kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria za nchi zinazomtaka mtu kutambua matokeo ya uchaguzi

  Haya yalitokana na madai ya Mh. Hamad Rashid kudai kuwa hawawezi kuungana na chama kisichomtambua rais wa nchi..... na chama kisichokua na sera ya serikali ya umoja wa kitaifa

  ninajiuliza.... mwenyewe


  1. je sera ya chama kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa inaweza kutekelezeka bila kubadili katiba ambayo hairuhusu hili
  2. Mh. RH kwa akili yake ya kawaida anajifanyisha kwamba hakuelewa maana ya kitu CHADEMA walichofanya
  3. CUF kuna double standards.... katibu wao mkuu ni Makamu wa kwanza wa rais visiwani.... hivyo ni part and parcel of the isles government.... je wabunge wa CUF kunauwezekano wakatumwa hoja za msingi zilizo tengenezwa kwa pamoja na CUF na CCM hivyo kuugawa upinzani..... hauoni CUF wapo mguu nje mguu ndani
  4. je.. serikali ya umoja wa kitaifa mara nyingi inatokea wakati gani.... au basi uelewa wa HR unahitilafu..... je serikali mbadala sio serikali ya mseto?
  Kwa maono yangu,Kuanzia jana usiku Mh. Hamad Rashid anakubali na anaweka milango wazi kwenye kuungana katika kambia ya upinzani na chadema, Mini ninaona jambo hili ni Hatari sana kwa kambi ya upinzani...kwa sababu ameshawatenga na kuwachanganya vyama vingine kama NCCR na TLP..... jee hii si tactic ya CCM ya Divide and Rule?
   
 2. m

  mpingomkavu Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii haijatulia kabisa, kwa upande wangu cuf kwa sasa ni kama serilikali sasa sijui wanataka kuwa upinzani kwa lipi, hebu ngoja tuangalie, lakini chadema wanapaswa kuwa makini la sivyo mambo yao yakwamishwa sana na hawa ccm b
   
 3. J

  John10 JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Mbowe ni mmoja wa viongozi Corrupt ndani ya TZ. Vyama vyote vya Upinzani TZ pamoja na CCM, vyote vimejaa na viongozi ambao ni CORRUPT, LIERS, and JOKERS.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  pole pole.... be relevant to the thread
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Msimamo wa CHADEMA ni sahihi kuwa wao wana wabunge wa kutosha kuweza kuongoza kambi ya upinzani bungeni kwahiyo hawana sababu ya msingi kutaka kuungana na vyama vingine ambavyo ni cronnies wa CCM!! Kazi ya chadema itakuwa ngumu sana bungeni iwapo watanasa kwenye huu mtego waliowekewa wa kushinikizwa kuungana na vyama ambavyo ni matawi ya CCM!! Chadema should go it alone for an effective opposition!
   
 6. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ki-MSIMAMO CDM wako makini na wanaonekana kwamba wao wanafahamu nini wanachofananya! Kuonyesha kwamba wako makini hata maelezo yao yamejaa USHAWISHI WA KISHERIA na KI-KANUNI! Wao hawapingi ili mradi kupinga! Kwa mfano:-
  1. Wameeleza wazi kwamba wao walichokifanya Bungeni ni "KUPROTEST" na kumuonyesha JK kwamba hawakubaliani na NJIA ZILIZOMPA USHINDI na walitaka hilo liwe wazi kwa kila mtu
  2. Wameeleza wazi kwamba wao WALIKUWA TAYARI KUSHIRIKIANA NA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI....tatizo ni kwamba vyama vyenyewe VILIWATENGA na kuanzisha kambi yao!! Kwa mantiki hii wakaamua WAENDELEE KUUNDA KAMBI YAO
  Sasa hawa CUF wao ni WABISHI TU, ni watu wa shari, wanatakak tu kushindana na kuleta ufa ndani ya upinzani! Kimsingi tayari wameshakuwa sehemu ya dola/serikali, wamejipunguzia sifa ya wao kuwa "wapinzani" maana wameshirikiana na serikali kule Zanzibar.

  Najiuliza masuala mengi sana, namshngaa HR anapotaka kila chama kikubaliane na SERA YAO....this is bull shit!!
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Duh! kila nikisoma thread hizi za chadema na cuf na kusoma michango ya watu napata kitu kimoja, wengi bado hawajui maana ya serikali ya mseto, na hawajui maana ya upinzani hasa!

  what happened in zanzibar is desirable in Bara, however, this will not eliminate the title of oppositon party, serikali na vyama ni vitu viwili tofauti.

  At a glance in mainland Slaa or should I say chadema where supposed to have atleast three ministries to lead on!

  Serikali ya mseto is not an option ia must! CUF have done so in zanzibar, eti kuwa na serikali moja ya mseto kunaua upinzania YES and only yes kama hao opposion lengo lao ni uongozi tu! but NO and big no kama tu lengo la viongozi ni kuweza ku-achieve certain remakable golas

  These kinds of governments are common in many countries!!!1 guys ebu amkeni acheni kutuaibisha duh!!
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  please kaka ..... zanzibar kuna serikali ya umoja wa kitaifa.... sawa sawaaa
   
 9. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Sikupenda body language ya HR hata kidogo maana ilikuwa inaamsha hisia hasi kwa wafuasi wa CUF. Na ni dhahiri sasa kwamba CUF ni chama pinzani kwa CDM. Hoja za CDM zimejaa mantiki na kutowaelewa CDM ni wendawazimu tu!
   
 10. L

  Logician Senior Member

  #10
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tumulize Mh. RH kwani CUF walivyoingia ktk maridhiano kule znz bila kuwashilikisha wapinzani wezao walikuwa wanajisikiaje? Msimamo wa CDM upo sawa!


  Mungu ibariki Tz!
   
 11. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Cuf wamenunuliwa.Wanalazimisha sera yao iwe sera ya vyama vyote.Ni kama vile malengo yao kisiasa yametimia.Hawa jamaa sio wapinzani tena.CUF ni hatari kwa opposition nchini.Wanaongea kishabiki,chadema wanaongea kimantiki
   
 12. t

  tonyk2 Member

  #12
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HR/CUF SIYO MJINGA ILA CUF WAMEUMIZWA SANA!
  In any politics especially serious political party timing ni kitu muhimu saana na HR/CUF analielewa hilo na kitendo cha CHADEMA kuitumia ile fursa adimu pale Bungeni na kutoka nje huku macho na masikio ya Watanzania na watu mashirika ya kima-taifa, kidini na taasisi mbalimbali wakitega masikio na macho yao kumsikiliza Rais akitoa mwongozo wa serikali yake na ghafula CHADEMA chini ya FREEMAN ELIKAEL MBOWE ana overshadow kila kitu na ku mfunika Rais na maswaiba wote si swala dogo hilo ni pigo ki siasa.
  Hilo ni jeraha kubwa mno kisiasa ni , nafasi inayotokea mara moja kwa kila miaka mitano ni watu wenye akili ndogo sana wanaoweza kulipinga hili huu ni ushindi kwa CHADEMA na CCM,CUF na wana siasa Duniani wanaelewa hayo "window of opportunity" umewaweka CHADEMA mahali pazuri kisiasa baada ya kuteka nyara anga zote za habari na jina lao kuwe a "Household name" overnight kwa gharama ndogo ya sacrifice kubwa ya Wabunge waelewa.
  CUF kama majeruhi wamekosa Front pages amabazo walikuwa nazo na wakadhani zitaongezeka kwani hata magazeti ya CCM yangeendelea kuwapamba. hiyo ndo hasira ya HR/CUF.

  BaadMAALIM SEIF KUTENGENEZEWA ulaji hawa wote wametoswa na habari zao hazitauzika tena kwani wamejiweka kwenye ka dirisha kadogo ka kuzungumza na Mwenyekiti/Katibu wamejifunga mdomo na hii ni hatari kwa chama chochote cha ki siasa.

  HR/CUF ongeeni nao lakini kwa ushirikiano hawafai hata kukaribishwa kwenye Coffee table ya CHADEMA.Watawahujumu.
  CUF BARA UONE HUO MTEGO NA ANGALIENI MTAKUWA WAPI MIAKA MITATU IJAYO, CHUKUENI HATUA KWANI ZANZIBAR ITAKUWA ZANZIBAR BARA ITAKUWA BARA TUKUTANA KWENYE MUUNGANO MPYA NA SAFI AMBAO HAUTAHITAJI KUWA NA CUF BUGURUNI.

  CHADEMA IMEFIKISHA MESSAGE NA MSIMAMO NA MADAI YAO DUNIANI KOOOTE NA NCHI NZIMA KWA MUDA ULE MFUPI.
  CHADEMA KIMEANDIKA HISTORIA NA KUCHUKUA FRONT LEAD YA KUDAI KATIBA NA NEC MPYA KWANI CUF KWA SASA WANACHODAI NI KIRAKA KIDOGO TU KWENYE KATIBA KWANI ILIYOPO IMEWAFAA NA WAMEAMUA KUUNGANA.
  MUUNGANO WA CUF NI BOMU LA MUDA LITAKALO PASUKIA HUKU BARA KWANI CUF/BARA WATAKAPO JUA HAWANA STAKE KWENYE MUUNANO ULIOWATENGENEZEA MASLAHI VIONGOZI WAO WA VISIWANI WATAAMUA KUJITENGA KWA KUIDAI TANGANYIKA YAO NA CHADEMA WAIT AND SEE.
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani ni sahihi kabisa kama alivyosema Mh. Mbowe kwamba HR/CUF imechanganyikiwa kutokana na mkanganyo mkubwa wa kikatiba baada ya MUAFAKA kati ya CCM na CUF zanzibar.... hatimaye wamebadilisha katiba ya Zanzibar ku accomodate MUAFAKA THUS... what is the effect to the UNION ..... everything is dumb...... and silent and CUF and CCM zanzibar intentionally did not want to root on this because it could have been a blessing for the opposition....

  kikubwa hapa ni kuweka wazi kuwa CUF ni wapinzani bara lakini Zanzibar sio wapinzani..... je hii sio mkanganyiko na double standards ?
   
 14. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tonyk2 amelielezea vizuri sana ili la chadema kususia hotuba ya JK; watu wengine inabidi wajilipue nakuteketeza maelfu ya wengine ili ujumbe wao uweze kufikia jumuia ya kimataifa, kwa chadema imeweza kufikisha ujumbe wake katika medani ya kimatifa kwa njia ya amani, bila ya kupoteza roho ya mtu yeyote. Huo siyo ushidi mdogo, ni mwendawazimu au yule mwenye mtindio wa ubongo hasiyeyaona mafanikio hayo. Kuhusu hoja ya waberoya kuwa Afrika inahitaji kuwa na serikali za mseto kama ile ya Zanzibar hoja yake hiyo haina ukweli wowote. Katika nchi zilizoendelea, kuunda serikali ya mseto maana yake ni vyama vya siasa husika kukaa pamoja na kukubaliana kuunganisha sera za vyama hivyo wakati wa uhai wa serikali hiyo ya mseto. Kwetu huku serikali ya mseto nikuchukua watu wachache kutoka kwenye chama cha upinzani na kuwapa uwaziri. Utaratibu huo hauna manufaa yeyote kwa taifa mbali na kuwapa ulaji wahusika ili kuwaziba midomo.
   
 15. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nawasihi sana chadema wasiungane na cuf kwa sababu mbili tu ya msingi kwamba:-
  1. Wameingia dhambi ya kuvunja katiba ya muungano wa tanzania kinyemela na kwa kigezo kwamba wananchi wa zanzibar wameridhia ilhali hawajaridhia kuvunjwa sheria mama! [wameongeza kipengele cha makamu wawili wa rais kinyume na tamko la katiba ya jamhuri ya muungano inayoongelea waziri kiongozi]

  2. Wamedhamilia kugonganisha/kugombanisha vyama vya upinzani na chama tawala ilhali kinachotakiwa ni hoja mbadala kati ya chama tawala na vyama vya upinzani. Wanagombanisha kwa kuungana na chama tawala kuunda serikali wakati huo wakiiambia jamii kuwa wao ni wapinzani wa serikali! Je, utapinga wazo lako mwenyewe na ukaeleweka?
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu .... mimi nipo nyuma yako nikitoa angalizo la kwamba je kikao cha wawakilishi officially kina upinzani na ni nani?

  kama Tanzania ni moja basi kwa nini katiba iruhusu pande mbili kuwa na mfumo tofauti wa muundo wa serikali.... pamoja na kwamba zanzibar wamesha declare kwamba ni nchi..
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180


  mhhhhhhhhh!!!!!!
   
 18. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,054
  Likes Received: 4,619
  Trophy Points: 280
  from as of today nitawaita CUF = FUC, hawa FUC hasa HR hawafai tumeongea mengi stay away from them
   
 19. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF wamepoteza haki ya kuwa chama cha upinzani Zanzibar. Je, 2015 kama Maalim Seif akigombea urais na akashindwa atalalamikia serikali wakati ye ni kiongozi wake? Au tume ya uchaguzi ambayo ipo chini yake?
   
Loading...