How to Register NGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

How to Register NGO

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by newmzalendo, Jul 6, 2011.

 1. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,351
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  How Do i register an NGO? naomba msaada wa Taratibu za kusajili NGO,na inachukua muda gani kupata usajili kamili?

  kuna vitendea kazi natarajia kutumia kutoka hapa nchini na baadhi kuagizia kutoka nje ya nchi ,JE kuna misamaha ya KODI ya aina gani ktk NGO.

  asante in Advance
   
 2. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,622
  Likes Received: 1,079
  Trophy Points: 280
  mkuu inategemea na aina ya ngo, kwa sasa ngo za humu ndani ya nchi nazani zinasajiliwa maendeleo ya jamii , naz ile ambazo nikutoka nje ya nchi zinasajiliwa mambo ya ndani wizara.

  Kwenye ishu ya misamaha, mkuu si rahisi kama unavyo fikilia kama huna mtu wa kukukingiz kifua, ni vigumu sana kupata msamaha na ukizingatia kwa sasa wameondoa baadhi ya misamaha ingawa sijajua ni ipi.

  Kama una mtu yuko huko juu atakusaidia kwenye ishu ya msamaha wa kodi but kama huna sahau kuhusu misamaha.
   
 3. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sijakupata vizuri mkuu! unataka kuanzisha ngo ama kampuni ya biashara? fafanua please!!
   
 4. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,146
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Wewe nawe vipi?

  Afafanue nini sasa wakati kitu kinajieleza wazi kabisa kwamba anataka kuanzisha na kusajili NGO? Wa-TZ bwana!! Kila kitu nyie mnaona ni mtego tu! Hata hilo nalo mpaka ufafanuzi?

  Kuhusu usajili ndugu, nenda tu hapo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya mwone DAS wa hapo atakupa maelekezo yote maana taratibu za kusajili NGO zinaanzia kwa Mkuu wa Wilaya. Siyo kweli kwamba NGO za nje peke yake ndo zinasajiliwa Mambo ya ndani, hapana! Kama unataka NGO yako iwe ya ki-Taifa unapaswa kwenda kusajili Mambo ya Ndani (ofisi ya msajili wa vyama), lakini kama itafanya kazi kwenye wilaya moja tu basi usajili wako utafanyikia kwenye wilaya hiyo hiyo.
   
 5. big-diamond

  big-diamond Senior Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kusajili Ngo mkuuni rahic sana jec nenda kwa mkuu wa wilaya kama ni ya wilaya i mean area of operation,kama ni mkoa nenda kwa mkuu wa mkoa pote hapo unapata fom unajaza then unalipia. Sijui cku hiz kama utaratibu umebadilika kipindi mm narejista ya kwetu na kwa kuwa inaoperate nchi nzima baada ya kupata fom na kujaza nlienda ofisi ya makam wa raisi pale ndo nilipeleka fom na katiba wakapitia na kurekebisha sehem nilizokosea then nikabind baada ya marekebisho afta one wik nkarudi kuchukua cheti, but cjui kama utaratibu umebadilika coz hiyo ilikuwa ni 2006.
   
 6. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,351
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Asante sana,NGO inalenga good governance and public rights + education and Access to information.nadhani italenga zaidi kimkoa na kitaifa.
   
 7. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,622
  Likes Received: 1,079
  Trophy Points: 280
  una uhakika? Hakuna ngo hata moja inayosajiriwa kwa mkuu wa wilaya au kwa mkuu wa mkoa. Hata kama ina operate kwenye wilaya moja.

  Muwe mnaandika vitu ambavyo una uhakika navyo na si kukurupuka tu. Kwa kifupi mwanzoni ngo zote zilikuwa zinasajiriwa wizara ya mambo ya ndani lakini hivi baadae wameamua wapeleke swala hilo wizara ya maendeleo ya jamii. Na wizara ya mambo ya ndani inasajiri zile za kimataifa tu kutokana na mambo ya kiusalama.
   
 8. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,622
  Likes Received: 1,079
  Trophy Points: 280
  MKUU KWA KIFUPI NI KWAMBA HAKUNA HATA SIKU MOJA AMBAPIO MKUU WA WILAYA ANASAJIRI NGO. WATU WANASHINDWA KUTOFAUTISHA VITU HIVI,
  1. KUSAJIRI
  2. KUJITAMBULISHA. ili uanze shughuli.
  KWA MKUU WA WILAYA UNAENDA KUJITAMBULISHA NA UNASAJIRIWA KWENYE DAFUTARI LAKE KAMA MMOJA WA WATU WANO FANYA KAZI KWENYE ENO LAKE LA UTAWALA.
  mkuu wa wilaya hasajiri NGO hata siku moja
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sure,ni kutambulisha NGO au kutambulisha mradi kama mtapenda
   
 10. k

  kazobe Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kusajor mkuu nenda ofisi ya makamu wa raisi kwa upande wa ngo, lakini kama ni cbo wilayani ofifi ya maendeleo ya jamii anamaliza kama unahitaji kuandikiwa katiba tupo wataalamu na inachukua si zaidi ya siku moja au mbili kupata gamba lako ila tu uwe na katiba ambayo ipo freshi.
   
 11. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,146
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Nina uhakika ndiyo!

  Wewe ndo umekurupuka!

  Hebu muwe mnaelewa na nyie. Nenda hata sasa hivi kwa Mkuu wa Wilaya ukaulizie kama hutapewa fomu za kujaza kwa NGO itakayofanya kazi kwenye wilaya moja naona unaumwa wewe! Mimi niliyesema hayo nimeshafanya nikaambiwa hivyo, lakini baada ya kuona NGO yetu itakuwa ya Kitaifa nikaelekezwa wizara mambo ya ndani ofisi ya msajili wa vyama (na hicho unachosema wizara ya maendeleo ya jamii siyo kweli labda hiyo ni CBO wala siyo NGO). Hii kazi nimeifanya mwaka 2008 mpaka sasa hivi NGO yetu ilishasajiliwa.

  Hiyo sheria unayozungumza ya kusajili maendeleo ya jamii sijui ya mwaka?
   
 12. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,146
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Usiwe unajidai kuandika hapa kabla ya kwenda kuulizia.

  Ukishaonesha kwa Mkuu wa wilaya kwamba utafanya kazi kwenye wilaya moja anakupa fomu za kujaza (tena hii kazi inafanywa na Katibu Tawala wa wilaya, yaani DAS). Hicho unachosema kujitambulisha ni pale unapoingia na NGO yako kwenye eneo lake. Lakini kama utakauwa unataka kusajili NGO ambayo itafanyakazi Kitaifa yeye kazi yake hapo ni kukuandikia barua ya kukutambulisha kwa msajili wa vyama ambaye yuko hapo wizara ya mambo ya ndani au unataka mpaka tukupe na ramani ya ofisi yake ilipo?

  Sasa nakushangaa umekazana tu kuropoka mkuu wa wilaya hasajili NGO bila kufanya uchunguzi bwana! Hebu nenda ukaulize hapo wilayani kwenu taratibu zilivyo halafu uje utujuze hapa jamvini. Maana tunaosema haya tulishayafanya. Huo ndo uhakika!! Tena wala siyo zamani sana ni mwaka 2008 tu!
   
 13. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,351
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  asante sana, J3 natinga ofisini kwa DC,tayari kuandaa mpango wa kujisajili
   
Loading...