How to fix no network/null or unknown baseband on mtk Android phone

Ramlis

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
597
494
Tatizo hili hutokea pale tu inapofutika IMEI number au baseband file, kama una tatizo kama hili inabidi uangalie kama IMEI number au baseband inasoma null.

IMEI number ni rahisi kuiangalia kama ipo nenda kwenye call menu piga *#06#.

Kuangalia baseband anza Menu>setting>About phone utaona Baseband version kama imeandikwa null tambua kama imefutika.
Kama baseband imefutika tafuta Stock rom au flash files model ya simu yako ndo uifanyie full flash.

Kwa kuandika IMEI number fuata maelezo haya.
Download; Driver za simu yako, imei_sn writer, Android Gadget CDC driver,MediaTek USB VCOM drivers na MT65xx modem DB file.

1.Install driver za simu yako + MediaTek USB VCOM drivers

2.Andaa IMEI number ambazo ni tarakimu 15 ukianza na 35-------- kama simu yako ni lain mbili katika IMEI number ya pili itofautishe na herufi mbili au moja za mwisho katika IMEI number ya kwanza.

3.Fungua imei_sn writer, kwenye platform setting weka Smart Phone. Weka alama ya vema kwenye IMEI number na kama uliandaa IMEI number zako kwenye text editor Copy na u-paste sehemu ya IMEI number.

4.Bonyeza kwenye neno select DB, elekeza sehemu ulipoweka file zako za DB, chagua kulingana na cpu ya simu yako mfano ni mt6572.

5.Toa betri kwenye simu yako, unganisha USB cable kwenye kompyuta yako na simu.

6.Nenda My computer >Manage >Device Manager.

7.Bonyeza start katika imei_sn writer, kwenye simu bonyeza Volume down+power button na weka betri kwenye simu achia button baada ya simu yako kusoma kwenye kompyuta.

8.Kwenye Device Manager itatokea missing driver ikiwa na alama ya njano, Right click ile driver >update driver software > Browse my computer for driver software ielekeze ulipoweka driver za CDC halafu install.

9.Subiria baada ya mda ikimaliza itaandika Write ok. Umefanikisha zoezi lako.

NB: Ni kosa kisheria kubadili imei number, rudisha zile za mwanzo utazikuta sehemu ya kuwekea betrii.
 
Last edited:
Back
Top Bottom