How to Detect the Hard Disk..via CD

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
355
Hi JF
Nilikuwa na Computer yangu Aina ya Dell ambayo natumia kwa ajili ya kazi za offisini,Especial GIS and Database Software Like Acquire for Data base,Vulcan(3D),ArcView,MapInfo etc.ina RAM ya 4GH.

Hard Disk Ili Crash last year,sasa nimenunua Hard Disk nyingine yenye GB 260...Nimekuwa nikijaribu ku configure toka juzi nimeshidwa...tatizo ni kuwa ninapo weka istallation CD kwa ajili ya kudetect kutumia CR ROM...inashidwa kuitambua.Nimekwama na sijui nianzie wapi tena...je inaweza kuwa ni tatizo ka cable kwenye Mother Board..kama ni hivyo nifanyaje...au je kama kuna ushari mwingine mnaweza kunisaidia kuhusu ku istall Hard Disk tena.
 
Hard disk haiwi detected kwa kutumia CD, inatakiwa iwe detected kwa BIOS [Basic Input Output System] kwa Dell computer zilizo nyingi huwa zina detect automatically ikishindwa huwa inakutaarifu hata kabla hujaanza istallation. cha kufanya hakikisha unatumia 80 lines bus cable kama board yako ni IDE. kama ni SATA jaribu kubadili hiyo cable tumia iliyokuja na hiyo Hard disk. solution nyingine jaribu ku reset CMOS kwa jumper au kutoa na kurudishia CMOS battery. Kingine hakikisha jumper ya harddisk yako iko kwenye Master. Dell zingine huwa hazitambui Primary master Harddisk ilosetiwa kama slave au cable selector

Bila shaka umenipata.....
 
Buswelu,
Ndiyo umetuambia kuwa hdd yako ili crush na kuwa umeamua ku-solve tatizo kwa kununua hdd nyingine (sijui kama mpya au kuu kuu)... swali langu hapa ni kuwa, je symptoms gani zimepelekea wewe kuona ni tatizo la harddisk, yaani kuwa hdd yako ime crush na wala si kinginecho kilocho haribika? Kingine, je iliharibika kwenye mazingira yapi... computer ilidondoka, iliingiwa maji, au ilipitishwa kwenye mionzi mikali n.k.?!

BTW, na endorse maelezo ya Positive Thinker hapo juu, naomba uyafuate kama unauhakika kuwa hamna kingine kilicho haribika bali hdd tu.

Nyongeza, kama hdd uliyonunua ni mpya na inafanyakazi naomba usijali comment hii. Lakini kama ulinunua kuukuu, hakikisha inajaribishwa pahala pengine kujua haina ubovu nayo baada ya kuwa umejaribu yote ya Positive Thinker, kisha tupatie feedback. Otherwise, kama ni mpya na umejaribu yote hapo juu, naomba uhakikishe inafanya kazi kwa kuichunguza kwa mbinu nyingine na wala si kuunganisha kwenye laptop yako (kama huna hizo mbinu unaweza kuirudisha huko ulikonunua kama hilo linawezekana). Ahsante.

SteveD.
 
Positive Na Steved Tuongelee Mtu Ambaye Sio Expert Hajui Cmos Ni Nini , Hajui Jumper Ni Nini Huyu Tumsaidieje ?

Zaidi Ya Kumwomba Anunue External Case ?

Pia Umewahi Kureset Bios Ya Compaq Evo Mfano Uone Kinachotokea ??
 
Shy,
Compaq wana tabia mbaya sana wala usifikiri unaweza ku reset CMOS ya compaq. ukitaka ku reset CMOS ya compaq inabidi uwe na Flash Diskette ya hiyo compaq husika. compaq za zamani zilikuwa zina save part ya CMOS kwenye Non DOS pertition maalumu inayokuwa created kwenye harddisk ya hiyo laptop au Compaq PC husika. Ukitoa HDD huwezi kuweka nyingine hadi uwe na Firmware ya CMOS ya hiyo Motherboard. Compaq iliponunuliwa na HP ndio kuna mabadiliko maana sasa wanatumia HP technology.

Hakuna kinachoshindikana kwenye Ulimwengu wa Computer Hardware.
 
Positive Na Steved Tuongelee Mtu Ambaye Sio Expert Hajui Cmos Ni Nini , Hajui Jumper Ni Nini Huyu Tumsaidieje ?

Zaidi Ya Kumwomba Anunue External Case ?

Pia Umewahi Kureset Bios Ya Compaq Evo Mfano Uone Kinachotokea ??
Shy, Nimekusikia hoja yako...
ILA kilichonipelekea kumuunga mkono PositiveThinker na solution yake hapo juu ni kuwa,
sidhani hata description ya tatizo la computer yake imetolewa kwa marefu, amesema tu kuwa hdd yake ime crush na kuwa kashanunua nyingine, hatujui kama ni mpya au kuukuu..

Watu tuna filosofia mbalimbali katika kutatua matatizo, mimi kwenye matatizo ya computer mara nyingi hutumia mbinu ya elimination... tatizo baada ya tatizo, nikiwa na uhakika na tatizo langu na sababu zake. Hivyo basi ningekuwa mimi mtu wa kwanza kutoa comment hapo juu, wala nisingemwambia kuwa anunue case ya kuweka hdd yake, sijui alichonunua kama kinafaa, kama kime kuwa tested, pia sijui kama anajua jinsi ya kukiunganisha... hivyo kama mtu ambaye anatafuta ushauri, kumtuma tu akanunue kitu kingine mimi sioni kama ni njia nzuri ya kutaka kutatua tatizo ambalo halijaelezwa vizuri na kuwa na uhakika nalo.

Hata hayo maelezo ya PositiveThinker, nisingeenda huko kote kutaka kumuelekeza mtu ambaye kipimo cha ujuzi wake sinauhakika nao. Basi kwa elimination, ningetoa wazo moja baada ya jingine na kuona kitu gani kinafanya kazi na nini hakifanyi kazi, pia sababu za computer kuharibika. Sasa kama hapo juu tunavyotaka kumuelekeza na kujikuta kumbe computer yake ilidondoka na circuit board yake imecrack kiaina hivyo haikamilishi mawasiliano ya ndani kwa ndani, nasi tunamwambia akanunue kitu kingine... fikiri sasa,afanye hivyo halafu akute hata ports za connection pia hazi detect kitu externally... what do you do, go for refund or...Naomba kuishia hapa kuhusu hili. Ahsante.

Shy, kuhusu Compaq, sijatumia sana (sijatengeneza) siku za hivi karibuni, mara ya mwisho ilikuwa 1999, nakukumbuka nilipokuwa nafungua cases za desktop na kujikuta nahitajika kununua security screw driver set kwa ajili ya kufungua cases zake tu...Wanavyofanya firmware lock ya CMOS it's interesting point, nitacheck na kusoma matatizo ya CMOS zake, walau hizo za zamani kama vile Endeleaaa anataja pia. Lakini pia najua some of Dell machines, especially servers nazo zinatumia technique hiyo ya ku-lock CMOS na POST code, ukishatoa hdd yake tu mpaka upate CMOS password kutoka kwao ambazo ziko serialised na hdd. **As a matter of fact, it is quite possible that Buswelu's problem might relate to this***
Baadae.

SteveD.
 
Back
Top Bottom