Elections 2010 How to Chakachua matokeo

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Kuna njia nyingi zinazotumika kuchakachua matokeo na njia mojawapo ni ile ya kubadili masanduku na kisha kutaka kura zihesabiwe upya na njia kuu ni ile ya kubadili takwimu.
Nitaongelea njia hii ya kubadili takwimu. Kinachofanyika ni kuwa msimamizi wa kituo anapaswa kujaza fomu 15 katika mafungu ya fomu tano kila moja. Fomu ya kwanza katika kila fungu inakuwa ni orijino na moja huenda kwa msimamizi wa jimbo wakati mbili huenda tume kwa majumuisho. Fomu ya pili (copy) hubandikwa kituoni lakini kasoro yake ni kuwa haisomeki kabisa. Fomu zilizobaki (copy zinazosomeka vizuri) hupatiwa mawakala wa vyama husika. Baada ya zoezi zima la kuhesabu na kujaza fomu masanduku hufungwa na kusafirishwa kwenda kata.Hapa ndipo uchakachuaji huanzia kwani msimamizi wa kituo anakuwa na uhuru wa kufungua masanduku na hapa huweza kuongeza kura feki au kubadilisha fomu ya matokeo (hususani upande wa rais). Hapa mawakala wa vituoni hawatakuwepo hivyo wakala wa majumuisho anapigwa za uso kavu kavu. Matokeo yanapoenda jimboni kama wakala wa jimbo si mjanja anaibiwa tena kwa kisingizio kilekile cha kugomea matokeo na kutaka kura zihesabiwe upya. Inapotokea upinzani wakashinda ujue juhudi za ziada zilifanyika kudhibiti uchanganyaji wa petroli. Kwa mfano jimboni Hai pamoja na kuzuiwa mawakala walishikilia msimamo wa kuwa na nakala ya daftari la wapiga kura hivyo kuwa na idadi kamili ya wapiga kura. Pia mawakala wa CHADEMA walihakikisha wanashiriki kila hatua ya ujumlishaji au uhesabuji upya wa kura hivyo ushindi kuwa dhahiri hata kabla matokeo hayajatangazwa.
Kama mawakala waliondoka mara baada ya kupatiwa fomu za matokeo walikosea sana kwani kama kura zilichakachuliwa (hapa kuna ushirikiano mkubwa kati ya mgombea wa ccm na msimamizi wa kituo kwani ndiye anayetoa idadi ya kura zinazotakiwa kwenye box la kubadili.). Jimboni Hai mawakala wa CHADEMA waliwashurutisha wasimamizi wa vituo kuzima simu zao hadi baada ya kumaliza kujumuisha kata.
Nimetumia jimbo la Hai kama mfano kwani nami nilikuwa mmoja wa vijana tuliohakikisha ushindi unapatikana na nilikuwepo katika kila hatua ya uhesabuji wa kura. Na hata mgombea wa ccm alipogomea matokeo nilimshauri Mbowe ampatie kura zote 300 za kituo hicho na bado haikumsogeza popote.

KAMA MLIFIKIRI KUWA NA MAWAKALA VITUONI ILITOSHA KUZUIA UCHAKACHUAJI,....HEBU FIKIRINI UPYA!
 
Mbona hamkuiweka kuwa policy ya chadema ili kila mmoja afuate???? unatuumiza roho, wasiwasi wetu yawezekana tulipokuwa tukiandika humu jf mikakati ya kulinda kura viongozi hawakufuatilia na kuifanya uniform policy kwa nchi nzima.Inauma sana.

TULIANDIKA SANA SWALA LA MAWAKALA NA KUTOA PROPOSALS
 
Mkuu kuna policy ambayo ni general na kuna initiatives ambazo zinategemea sehemu husika. By the way tulikuja kugundua kuwa kuna mwanya huo mwishoni na hata hapa kwetu si mawakala wote walilifanyia kazi. Baadhi waliondoka vituoni mara baada ya kupatiwa fomu za matokeo.
Mkuu hamna haja ya kuwa na shaka,kama sio leo basi kesho.
 
sasa nimepata kujua ni namna gani wameweza kuiba kura za baadhi ya majombo na za uraisi. naamini kuna zingine pia hatujapata,
 
Back
Top Bottom