How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

Mnapomsifu mnunua ndege, wasifuni na waliojenga viwanja vya ndege.
Maana bila wao tungekosa pa kutulia
 
Mimi naona ingekuwa bora kushauri tutafute pesa kwa ajili ya sekta zingine kama kilimo, mifugo, uvuvi, maji/umwagiliaji na ajira kwa namna yake badala kukosoa au kulaumu kwa kile kinachofanywa na kuona kama vile ndicho kinachotukwamisha. Umeme, reli na usafiri wa anga nayo ni muhimu. Bila reli ya haraka, bandari yetu itakuja kuwa tembo mweupe huko mbeleni.
 
Hivi ni kweli watanzania hatuelewi umuhimu wa hizi ndege kweli?

Hivi ni kweli kuna mtoto asielewa sababu ya kwanini baba yake amenunua lory la mizigo au basi la abiria badala ya kumfungulia duka kwanza.

Hivi ni kweli kuna mpangaji asie elewa umuhimu na faida ya kujenga nyumba yake.

Au mpaka leo kuna mtanzania ambae haelewi faida ya kujenga shule za sekondati kila kata nchi nzima badala ya kuboresha kwanza zile zilizo itwa shule za vipaji maalumu.

Hivi kuna mtanzania wa kawaida anae elewa hela za kuendesha elimu bila malipo na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu zinatoka wapi.

Inamana tunaka kusema kwamba ni afadhali hizo hela zilizonunua ndege zingegawanywa katika wizara mbali mbali zikatekeleze miradi ya maendeleo kuliko kunua ndege zitakazo leta faida zaidi hata kwa miaka kadhaa ijayo kisha faida ndo itumike.

Hivi kweli kuna mtu anaogopa kuanzisha mradi flani kwa kumuangalia flani anaelega lega kisha mtaji aliokua nao anakula wote?

Hivi kweli kuna mtu asiefahamu kwamba kuyumba kwa biashara kuna changizwa na vitu vingi ikiwemo poor managment

Hivi kweli tuache kununua ndege eti kwakua ethiopia shirika lao limeyumba basi nalakwetu litayumba bila kujiuliza sababu za kwanini limeyumba pengine ni poor managment je sisi tuki improve managment hatuwezi kufanya vizuri?

Mambo ni mengi sana ngoja niishie hapo kwanza.
 
Mmejipangia kubakia miaka mingapi madarakani?
Maana kwa mujibu wa katiba yetu ni miula miwili tu.
Mihula mwisho ni miwili ile ile, ila for the sake of national development, we can give him enough time as long as it takes mpaka akamilishe miradi yake yote.
P
 
Mmeamua wewe na nani Mkuu
QUOTE="Danny Jully, post: 33271510, member: 160061"]
Mkuu Pascal tumeamua na nani? Au ameamua tu mwenyewe!!
[/QUOTE]
Japo mwamuzi wa mwisho ni mmoja, ile principle ya a collective responsibility applies. Hivyo sisi wote tulioamua kuunga mkono juhudi, tumeamua kwa pamoja.
P
 
Kun uzi upinzani mliuanzisha kitambo mkiishangilia rwanda kununua ndege na mkajiuliza nchi kubwa kaa tz tunashindwa wapi na nchi ndogo. Leo kibao kimegeuzwa.

..Rwanda wamesalimu amri kwenye biashara ya ndege.

..shirika lao la ndege halijawahi kupata faida tangu lianzishwe.

..majuzi wamechukua uamuzi wa kuuza baadhi ya hisa kwa Qatar Airways.
 
Kupanga ni kuchagua, tumeamua kuchagua kufanya maendeleo ya vitu kwanza, kama ndege, miundombinu, SGR, Stigler, flyover, na kujenga Tanzania ya Viwanda. Miradi hii mikubwa ikikamilika, ndipo tutageukia maendeleo ya watu.
P
Mlipanga na nani, sisi hatuwezi kushiriki kupanga ujinga wa kununua ndege huku watu wanakunywa matope, nani ashiriki dhambi hiyo.
 
Kupanga ni kuchagua, tumeamua kuchagua kufanya maendeleo ya vitu kwanza, kama ndege, miundombinu, SGR, Stigler, flyover, na kujenga Tanzania ya Viwanda. Miradi hii mikubwa ikikamilika, ndipo tutageukia maendeleo ya watu.
P
kulipaswa kuwa na uwiano, maendeleo ya watu yatengeneze uhitaji wa vitu.
 
Huwezi endeleea bila kuwa na kitu cha kuingiza pesa za kigeni ndani. Ndege ni moja ya biashara nzuri sana ya export inayokuingizia pesa ndani na time to market is very short.

Biashara zinazozungurushwa ndani mnazotaka ndo zitawatia watu umasikini zaidi.

Ukitaka kufahamu hilo, nenda kijijini kwenu kawape milion 100 uwafungie wafanye biashara wao kwa wao, wasitoke nje, rudi baada ya miaka 5 utakuta wamekuwa masikini zaidi, na hizo milion 100 zimepugua zaidi maana zingine zimechanika na zingine zimepotea.

Mkumbuke biashara inayofanyika humo ndani bila export hiyo si biashara bali ni service. Hii service itaenda kwa pyramid scheme na mwisho kuanguka.
Magufuli na serikali yake kununua ndege is the right approach.
Schupid articulation!
 
kulipaswa kuwa na uwiano, maendeleo ya watu yatengeneze uhitaji wa vitu.
Theory za Economic Development Vs Economic Growth Vs Community Economy Development mpaka sasa zina mijadala mingi na haitaisha duniani.

Tukubaliene namna gani tunatumia uwepo wa ndege kuongeza ukuaji wa mifumo mingine au biashara zingine.

Sio uzalendo kulaumu hata kwenye mambo ya msingi. Kama JKN alikuwa na ndege miaka ya 70 na 80 kwa sasa purchasing power ya Watanzania ni kubwa kuliko wakati wa Mwl. na uhitaji wa usafiri wa ndege ku-facilitate biashara na utalii.

Wale tuotaka mzee aweke hela kwenye miradi mingine, walau tuna businesses model au investment models zipi ambazo say akiwekeza 50bil Return on Investment inaweza kuwa.... ndani ya muda.... na inapunguza imports kwa .....na kukuza ajira kwa kiasi... na kupunguza bei ya bidhaa madukani kwa kiasi....

With such facts, huyu mzee unaweza kukaa nae juu ya meza
 
Aibu kwa kujisemesha vitu usivyo vijua. Miradi ya afya , elimu ,kilimo iko juu zaidi kutekelezwa.vituo zaidi ya 300 vimejengwa kwa mkupuo, elimu vivyo hivyo. Ikila kona ujenzi tu.
 
Mleta mada nimependa uandishi wako na utaalamu wako wa lugha ya malkia. Pascal kaona nyota nyota akakurupuka na ma thread yake yake ya propaganda za kujipendekeza ili apate ukuu wa wilaya.
 
Kupanga ni kuchagua, tumeamua kuchagua kufanya maendeleo ya vitu kwanza, kama ndege, miundombinu, SGR, Stigler, flyover, na kujenga Tanzania ya Viwanda. Miradi hii mikubwa ikikamilika, ndipo tutageukia maendeleo ya watu.
P
Ni kweli kupanga ni kuchagua, LAKINI JE, KWENYE KUCHAGUA HAKUNA KUKOSEA?
 
Back
Top Bottom