Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,062
- 731
Mwafrica hujanielewa na unabidi usome message nzima. Hatuwezi kuishi bila misaada kwa sasa, miaka ijayo itawezekana lakini kwasasa tuna chaguo mbili misaada au madeni, na mimi nafikiri misaada ni mizuri kuliko madeni. Miaka 5 iliyopita nilikuwa natumia $500 kwa mwezi kununua dawa za ndugu yangu za ukimwi na sasa natumia $0 kwasababu dala zipo kwa wagonjwa kwa bure. Hii yote imewezekana kwa sababu ya misaada, kama wewe unataka mikataba ndiyo ilipe dawa ni mawazo yako lakini mimi binafsi na watanzania wengi wamefaidika kwa misaada tutake au tusitake.Nchi yetu itafikia wakati wa kujitegemea lakini kwa sasa kuhudumia watu 40 million na tuna deficit kwenye budget ya 30% na budget yetu yote ya Tanzania ni $3Billion misaada ni muhimu hasa ya afya. Je kuna ubaya gani kusaidia watoto net za mbu hata kama ni $25 million wametoa kwa hilo na watoto wanapona kunaubaya gani? Watanzania kwa upande mmoja tunatabia ya kupinga vitu kwani tunapenda ubishi na ubishi huu wa Mwafrica hauna msingi.
Si kila ufumbuzi unao onekana ni rahisi ni ufumbuzi sahihi.
Misaada ni ugonjwa mbaya kuliko magonjwa yote yaletwayo na umasikini.
Umasikini wetu ni wa mawazo zaidi kuliko kwamba hatuna rasilimali.
Misaada inatunyima nafasi ya kuchukua hatua madhubuti kumaliza matatizo yetu ya kiuchumi.
Misaada inawafanya Watendaji wa serikali,Wabunge na wananchi wengi kugeuza shingo zao na kuangalia nje ya nchi kwa macho ya kuonewa huruma badala ya kutazama ndani ya nchi kwa macho ya upembuzi na kutafakari uwezo wetu tusio utumia.
Deficit unayoiongelea inalelewa na Wabunge wetu na serikali kwa ujumla kwa kuendekeza mambo mengi yasiyo ya lazima. Kwa watendaji wa serikali na baadhi ya wananchi,Misaada kutoka nje ni nafuu yao binafsi ndiyo maana hawaoni aibu kutangaza bajeti tegemezi.
Si lazima viongozi wa serikali watumie VX na GX lakini ni lazima watumie magari imara ambayo yako mengi sana na ya kila aina. Ununuzi wa magari tu nchini Tanzania unaonyesha ni vipi watendaji wetu wa serikali wasivyo ona aibu kuomba misaada kutoka kwa kila wanaye muona anazo.
Si muda mrefu ujao tutaanza kuoamba misaada kutoka nchi masikini kama sisi.
Indonesia, Thailand, Vietnam na hata Kambodia tu kwa sababu sisi Watanzania tunadhani tulizaliwa kuomba na kusaidiwa.
Wabunge na viongozi wa serikali hushhirikiana kupanga bajeti tegemezi kwa sababu tu akili zao na maono yao ni tegemezi.Ndani ya vichwa vyao hawaioni bajeti inayo jitegemea. Ni walemavu.
Mtu akiwa kilema kiungo fulani nje ya mwili wake ni rahisi kwa kila mtu kumwona mlemavu. Lakini mtu akiwa mlemavu katika sehemu ya ubongo inayoshughulikia Vision, nje ataonekana yuko sawa lakini kumbe hayuko sawa hata kidogo, utamwona jinsi anavyohangaika kuiona kesho na keshokutwa katika mipango yake. Viongozi wa serikali yetu tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni walemavu wa ubongo katika sehemu inayoshughulikia Vision, wala siongopi.
Kama una $100.00 ni vipi unaweza gharamia maisha ya $130.00?
Wananchi walio wengi nchini Tanzania wanishi sawa sawa na vipato vyao.
Wale wanaoishi chini ya vipato vyao ndo pekee walioweza kupiga hatua kinyume na matazamiao ya wengi kama siyo wote.
Mafisadi na Serikali yetu ndo wao pekee wanaishi kwa fedha inayozidi kipato. Kwa sababu sehemu ya Bongo zao inayoshugulikia Vision imedata, wanashindwa kelewakwamba nchi ni lazima itumie sehemu tu ya kipato chake na zaidi ni lazima ichukue hatua madhubuti kupigana na jinamizi la kutegemea misaada.
Nchi kutegemea misaada ni ugonjwa mbaya kiuchumi ufananao na ugonjwa wa Ukimwi.
Kwa hiyo nchi inayotegemea misaada ni sawa na mgonjwa wa ukimwi.
Naomba nieleze mfano huu wa ugonjwa wa ukimwi kabla sijaonekana nina matusi na kukosa heshima.
Mgonjwa wa ukimwi hupewa dawa kurefusha maisha yake, kwani mpaka sasa hakuna dawa iwezayo kuponya ukimwi. Nchi inayoishi kwa misaada inaishi kama mgonjwa wa ukimwi kwa sababu misaada ni dawa ya kuairisha matatizo tu.
Hakuna nchi na wananchi wake walioendelea kwa kupewa misaada.