How do you patent an idea in Tanzania?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Nina idea moja ambayo kama serikali ikiamua kuifanyia kazi
a. Itainua jina la Utalii wetu
b. Itaingiza fedha za kigeni kuliko mahali popote Afrika
c. Na itaifanya Tanzania kuwa katika hadhi ya pekee yake kila watu wanapozungumzia utalii duniani.

I would like though to patent it. Sijawahi kuisikia mahali popote, haipo katika sera zetu za utalii, na siyo mawazo ya mtu mwingine (I didn't plagiarize). How can a Tanzanian patent an idea that will affect the tourism industry and earn him some good money?

Can I patent an Idea in US that will affect another foreign country? I'm willing to share that idea with someone who knows architecture, drawing, and marketing.....Believe me, once you hear it, It'll blow you mind!!!!!!
 
Mzee Mwanakijiji said:

Mzee Mwanakijiji umekamata kwenyewe.Nadhani Mh.km amerudi ktk hii safu basi hii aiwekee note,ni extract muhimu.Serikali hadi leo bado wapo wanjisuasua kwa copywrites za wasanii tuu hawajui hata ktk patent kunaweza watoa wabongo kibao,kwani mtu km analowazo jipya na zuri akilewekewa patent analiuza au kukopea nalo na kuweza fanya kazi kwa kipindi fulani ambacho atakuwa amerudisha gharama zake na ndio sasa fungulia mbwa ianze ili kuleta upinzani.
Lakini leo hii hata jamaa wa chai maharage enzi zile,au chakula cha waathirika Arusha,Au mchoraji wa leo anaweza fikisha proposal yake bank leo ya kuomba mkopo kwa ajili ya wazo lake kesho akakuta hilo wazo limeshafanyiwa kazi na tajiri moja nguvu za kutisha.
Mzee mwanakijiji hii itapiga bao si utalii peke yake bali kila sector.Patakuwepo mfumuko wa mawazo na ubunifu wa kila nyanja ambao utaleta mafanikio makubwa.Mtaji wa kila raia utakuwa akili yake,na mafanikio ya makampuni yatakuwa mitaji yao.
 
MONEY LAUNDERING BADO BONGO SIO KITU CHA MUHIMU.
Nakumbuka kuna mwaka mmoja muheshimiwa Mbowe kipindi hicho akiwa mbunge wa Hai,alisema hatari ya money laundering,kwa kweli kile kitu kiliniingia sana na bahati mbaya waandishi wetu wa habari hawakona umuhimu hilo jamabo.Sijui ni kutoelewa au basi wameona aliyeongea hana maana.
Walichoshindwa elewa ni kwamba Mh Freeman mbowe katembea na ni mfanya biashara wa kimataifa, kaona mataifa mengine, kaona wafanya biashara wanavyohamisha fedha kwa njia haramu kiasi cha kuicha serikali ikikosa fedha za kigeni.
Sasa hapa kuna njia nyingi za kucheza na hii money laundering.Hapa wachumi wetu ndio inabidi waonyeshe thamani ya elimu yao.
Leo nimewawekea hii link kuwafikisha ilipo article ambayo pia inaelezea mambo mengi kuhusu nchi zetu za SADC na uporaji unaoendelea,kupitisha madawa ya kulevya ,kutoroshwa madini na utdahifu wa mifumo yetu ya usalama wa mipaka,mamlaka ya kodi,na vyombo vya sheria.

http://www.iss.org.za/pubs/Monographs/No90/Chap3.pdf

Nategemea watakuwepo watu watakaoangalia hay yote kwa makini na kufanya mabdiliko kwa ukombozi wa nchi.
 
Nicholas,
Hiyo site inatakiwa aipate JK mwenyewe maanake imegusa kila kitu ktk real world ya mlalahoi. Na hakuna dawa isipokuwa kwanza ujue chimbuko la maradhi. Huyu Prince Bagenda, sii mchezo mdogo nampongeza sana kwa taarifa yake.
Kuhusu Freeman, unajua kaishi maisha yote ya ubangaizaji mbali na kulifanyia swala utafiti. Anaelewa kiundani mambo mengi ambayo viongozi waliokulia CCM hawawezi kuyafahamu - unless kiongozi huyo kajihusisha yeye mwenyewe pia kumbuka tu kwamba zamani mtu yeyote ndani ya CCM alikuwa akiitwa shushushu kwa hiyo sii rahisi viongozi hao kuhusishwa na biashara kama hizi moja kwa moja.
Inasikitisha tu kwamba taarifa kama hii viongozi wa juu wataichunguza na kuchambua vipandevipande kupinga ukweli uliosimama kulinda maslahi yao. Na ni hawahawa viongozi wanaotumiwa kupeleka fedha nje kwa malipo ya njugu! wapo radhi kulididimiza taifa ili mradi wamepata KULA yao.
Kwa mwondoko wa JK nafikiri taarifa kama hii itamfaa sana ktk jitihada zake za kurudisha sheria juu ya kila mtu.
 
Watu wenye kudownload windows xp sp3 kwa bure na patent ni vitu viwili tofauti. Sisi tuendelee hivihivi mpaka mwisho wa dunia.
 
Nina idea moja ambayo kama serikali ikiamua kuifanyia kazi
a. Itainua jina la Utalii wetu
b. Itaingiza fedha za kigeni kuliko mahali popote Afrika
c. Na itaifanya Tanzania kuwa katika hadhi ya pekee yake kila watu wanapozungumzia utalii duniani.

I would like though to patent it. Sijawahi kuisikia mahali popote, haipo katika sera zetu za utalii, na siyo mawazo ya mtu mwingine (I didn't plagiarize). How can a Tanzanian patent an idea that will affect the tourism industry and earn him some good money?

Can I patent an Idea in US that will affect another foreign country? I'm willing to share that idea with someone who knows architecture, drawing, and marketing.....Believe me, once you hear it, It'll blow you mind!!!!!!

Ulifikia wapi na hii idea Mkjj?
 
Never got a satisfying response... nimeishia kupatent hapa hapa US...

Kwani Tanzania imefungwa na U.S. patent rights?

Ulishajaribu kuwasiliana na wahusika wa hizi Tanzania legislations:
- Trade and Service Marks Act
- The patent rights
- the copyrights and Neighboring Rights Act

By the way, you don't patent an idea, you patent an invention. Oh well, all inventions begin with ideas anyway. So.....
 
Swalii langu lilikuwa linahusiana na hayo yote.. ya copyright, trade mark na patent... We'll see... bado kuna vitu vingi vya kujaribu
 
kwa tanzania waone jamaa wa brela watakusaidia.

us wana kitu kinaitwa business methods patents nadhani kwa maelezo yako hiyo invention yako yaweza angukia katika kundi hili. bahati mbaya patents ni "teritorial" hivyo ukipatent uvumbuzi wako us utalindwa us tuu na sehemu/nchi nyingine wanaweza kuiga bila kuvunja sheria.

mara nyingi maamuzi ya wapi u-patent uvumbuzi yanabidi pia yazingatie mkakati wa kibiashara ingawa sio wengi wanaofanya hiyo. kwa hali uliyoeleza inabidi u-patent uvumbuzi wako katika nchi zilizo vivutio vya utalii kwani huko ndiko jamaa wanaweza kutumia uvumbuzi wako. aidha inabidi upate patent katika nchi ambazo zinauwezo wa kucopy uvumbuzi wako.

nadhani utaona haya machache yanaweza kukusaidia.
 
Nina idea moja ambayo kama serikali ikiamua kuifanyia kazi
a. Itainua jina la Utalii wetu
b. Itaingiza fedha za kigeni kuliko mahali popote Afrika
c. Na itaifanya Tanzania kuwa katika hadhi ya pekee yake kila watu wanapozungumzia utalii duniani.

I would like though to patent it. Sijawahi kuisikia mahali popote, haipo katika sera zetu za utalii, na siyo mawazo ya mtu mwingine (I didn't plagiarize). How can a Tanzanian patent an idea that will affect the tourism industry and earn him some good money?

Can I patent an Idea in US that will affect another foreign country? I'm willing to share that idea with someone who knows architecture, drawing, and marketing.....Believe me, once you hear it, It'll blow you mind!!!!!!

Kwanza nakupongeza MMKJJ. Kitendo tuu cha kuwa na idea ya maendeleo ya taifa letu kinahitaji pongezi. Wewe ni mtu tajiri sana kufuatia maneno ya Nyerere 'Umasikini mbaya kabisa ni umasikini wa fikra'. Sio siri wabongo wengi bado tuko umasikini wa fikra. Mimi naamini tanzania itakombolewa kiuchumi na wenzetu wachache mliopata good exposure ikawafunua kuona mbali na licha ya kuwa mko ughaibuni kwenye brain drain lakini sasa mko tayari kulisaidia taifa. Thanks for that.
Coming back to the point, -
Trade and Service Marks Act, The patent rights and The copyrights and Neighboring Rights Act,1999 haziwezi kukusaidia kupatent idea yako. hakuna copyright ya idea Tanzania.
The only thing you can do ni lazima uandike paper au kitabu kuhusu hiyo idea yako. hilo andiko unaweza kulipatia copyright under Interlecture Property Act kwamba ni mali yako. Then seek oudience with waziri wa utalii ama rais mwenyewe. wasilisha andiko na naamini litakubaliwa.
Mkapa alilikubali wazo la Prof.Hernando De Sotto wa Peru.Akamwalika kuja kufanya presentation Tanzania kwa cost ya Dola 1m. Jamaa akaja, akamwaga sera, tumezikubali ndio tukaanzisha MKURABITA.
Fanya mambo Mzee, sio mpaka wazungu tuu.
 
Nadhani masuala ya patent yanazingatiwa zaidi kisheria na "hawa wenzetu" wanaojali,kuthamini na kulinda ubunifu.That's not to say huko nyumbani hakuna sheria na kanuni za aina hiyo bali ni mambo yaleyale ya who cares.Njoo na idea au project yako Bongo,and next day utamkuta m-babaishaji flani kaifanyia some slight modifications (tena bila hata ku-acknowledge kuwa "wazo hilo la wizi" lilizaliwa baada ya kuona ubunifu wa mtu flani i.e. mwenye patent) na anatembea kifua wazi macho mita 100 akijigamba kwa "ubunifu" wake.

Kama sheria nzito na muhimu kwa maslahi ya wengi kama ile ya Wahujumu Uchumi (ambayo ingetumika vizuri kuwapeleka Segerea,EL,RA,et al) haitiliwi maanani,tutegemee nini kwenye mambo ya patent?
 
naamini tanzania kuna sheria zinazohusu masuala ya patents na copyright. shida ipo, kama alivyosema mkuu mlalahoi hapo juu, utekelezaji wake yaani "enforcement" uwezo wa vyombo vinavyohusu usimamizi wa utekelezaji wa sheria hizo. aidha pia uelewa wa wananchi kuhusu kosa la kuiga bila idhini ya muhusika.

kama huo uvumbuzi wako ni patentable,
kama nilivyoeleza awali kuna mikakati mbalimbali ya kibiashara inayoweza kutumiwa ili kujaribu kufanikisha kunufaika kwa uvumbuzi wako. moja ni hilo la kuchukua patent kwenye nchi unazoamini uvumbuzi wako utakuwa na mvuto wa kutumiwa na nchi ambazo zinaweza ku-copy kwa mafanikio uvumbuzi wako.

njia nyingine ni "preventive publishing" yaani una-publish uvumbuzi wako hivyo unakuwa na haki miliki (copyright) lakini pia unazuia mtu mwengine kuchukuwa patent juu ya uvumbuzi wako. ubaya wa mkakati huu ni kwamba mtutu yeyote anaweza kuutumia na hapa ndio utakuta unapigwa bao na wale wenye pesa kwani wao wanaweza kuwekeza sehemu nyingi na kukutoa nje ya soko.

kwa kweli copyright hailindi "ideas" bali hulinda "expression of idea" ndio maana watu wengi wanaweza kuimba au kuandika kuhusu "mapenzi" bila kuingilia copyright ya mtu mwengine au kama dan brown wa "da vinci code" alivyowapiga bao jamaa waliotunga "the holy grail".

naona kwa sasa niishie hapa
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom