Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,095
- 2,429
Nilipomsoma Walter Rodney na Kitabu chake How Europe Underdeveloped Africa kuna mambo nlikubaliana naye na mengine mengi sikukubaliana naye.ulikuwa ni ule ule mwendelezo wa miaka yote ya malalamiko, uonevu n.k nilimwelewa alipenda kutujulisha namna gani ambavyo tulinyonywa na kurudishwa nyuma kiuchumi,utamaduni n.k
Miaka mingi baadaye afrika inatawaliwa na waafrika wenyewe. miaka zaid ya miaka 50 ingawa yeye walter rodney ali publish kitabu chake 1972. Namshukuru aliweza kuandika alichoandika kutusaidia kihistoria. Miaka zaidi ya 40 baadaye Afrika bado ni ile ile yenye wakoloni weusi. Hawa wameonesha kuwa ni wabaya sana pengine zaidi ya hata ya weupe. Miaka 40 baadaye viongozi wa afrika wanahusika katika kuinajisi afrika kuiba pesa na wkend akuficha nje ya afrika, kuuana, kufungana, kuua tembo, kuuza madini, kuuza madawa ya kulevya kuwaumiza waafrika wenyewe.
Miaka 40 baadaye kama lumumba angeweza tizama kinachoendelea katika nchi za Afrika angeumia sana kujilaumu kwa kuifia Afrika isiyotambua mchango wake. Kama angeiona kongo ya sasa. Angetembea tembea mpaka Afrika ya Kati, angeenda huku kusini mwa Afrika,Afrika Mashariki,Afrika Magharibi na maeneo mengine angejikuta ana huzuni ya kifo.
Miaka hii hatuna wazungu wa kuwalaumu. ni waafrika wenyewe wanaotesa waafrika wenzao kwa uroho wa madaraka, ulevi,ushetani n.k waafrika wamekuwa kila baada ya miaka kadhaa wanachagua mungu wa kumtumikia. Marais wa afrika wamekuwa miungu watu wakijitajirisha wao na familia zao. Wakiwatesa wananchi wao kwa njaa kwa kuwapiga na polisi wanaolipwa kodi za wananchi hao.
Nyerere alishaanza kuchoka na maisha haya. Hakuwa mkamilifu lakini alikuwa na maono. Viongozi wa sasa wa afrika wanaongozwa na matumbo yao, wanaongozwa na jazba. Najiuliza akina Kwame Nkurumah wangeangalia afrika ya sasa wangesemaje? Nchi zetu zimeduwaa tunauana na kukomoana. Tumekuwa na siasa chafu za kizandiki,kinafiki ,kifisadi na kishetani.
Miaka hii hatuna wazungu wala waarabu wa kuwalaumu. Hawa walitupeleka utumwani na kututesa n.k miaka hii hatuna akina Chief Mangungo wa Msovero. Ambaye maskini hakujua kusoma wala kuandika.