Housegirl apewa adhabu ya kufungwa kwenye mti kwa siku 4

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Mfanyakazi wa ndani mjini Ryadhi nchini Saudi Arabia amenusurika kifo baada ya kufungwa kwenye mti uliokuwa juani na bosi wake kwa kosa la kuacha samani za ndani juani.

ab9507eb20e8b48b857546ea04084468

Mwanadada huyo aitwaye Acosta Baruelo, 26 ambaye ni raia wa Ufilipino amesema alifungwa kwenye mti baada ya kuacha baadhi ya samani za thamani juani.

Akielezea jinsi alivyonusurika kwenye adhabu hiyo ya kinyama, amedai kuwa alimuomba mfanyakazi mwenzie wa kike ampige picha kisha asambaze kwenye mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya mkononi.

Baada ya tukio hilo, picha hiyo ilianza kusambaa hadi kufikia Mei 9, 2019 tayari Jeshi la Polisi mjini Ryadh lilikuwa limeshaipata nyumba hiyo na kumuokoa mfanyakazi huyo.

Mama huyo aliyetekeleza adhabu hiyo, tayari ameshafunguliwa kesi ingawaje mtuhumiwa wake amesharudishwa nyumbani.

Kufuatia tukio hilo, Ubalozi wa Ufilipino nchini Saudi Arabia ulilazimika kumsafirisha mwanamke huyo kumrudisha nyumbani siku hiyo hiyo aliyookolewa na polisi.
 
Kumbe ni wale wale..

Hao watu huwa wanachukulia watu wa mataifa mengine kama wasio na thamani yeyote duniani.
 
Mwarabu mtu mmoja poa sana!!!if you catch what i mean...

Kwa sasa hatuna kauli nyengine ya kusema zaidi ya hii,nitoe pole kwa mtendewa hilo tukio.
 
Mfanyakazi wa ndani mjini Ryadhi nchini Saudi Arabia amenusurika kifo baada ya kufungwa kwenye mti uliokuwa juani na bosi wake kwa kosa la kuacha samani za ndani juani.

ab9507eb20e8b48b857546ea04084468

Mwanadada huyo aitwaye Acosta Baruelo, 26 ambaye ni raia wa Ufilipino amesema alifungwa kwenye mti baada ya kuacha baadhi ya samani za thamani juani.

Akielezea jinsi alivyonusurika kwenye adhabu hiyo ya kinyama, amedai kuwa alimuomba mfanyakazi mwenzie wa kike ampige picha kisha asambaze kwenye mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya mkononi.

Baada ya tukio hilo, picha hiyo ilianza kusambaa hadi kufikia Mei 9, 2019 tayari Jeshi la Polisi mjini Ryadh lilikuwa limeshaipata nyumba hiyo na kumuokoa mfanyakazi huyo.

Mama huyo aliyetekeleza adhabu hiyo, tayari ameshafunguliwa kesi ingawaje mtuhumiwa wake amesharudishwa nyumbani.

Kufuatia tukio hilo, Ubalozi wa Ufilipino nchini Saudi Arabia ulilazimika kumsafirisha mwanamke huyo kumrudisha nyumbani siku hiyo hiyo aliyookolewa na polisi.
Spendi uonevu lakin hii picha ni photoshop bhana... kwan propaganda hizi lengo lake ni nin!?
 
unaweza kutoa source ya habari yako? bila ya hivo tutaendelea kufahamu kua ni muendelezo wa propaganda za uwongo
 
Wanawake Bhana Sasa Unakubari Kufungwa Vipi Asiwe Anajitengezea Mazingira Ili Ajipatie Pesa
 
Warabu hasa Saudia wanaroho mbaya sana. Mafunzo ya dini ya mnyazimungu, hufundisha haya?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
alimuomba mfanyakazi mwenzie wa kike ampige picha kisha asambaze kwenye mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya mkononi.
Sasa alishindwaje kumwambia huyo mfanyakazi mwenzie wa kike aje amfungulie mpaka asubiri polisi?
 
Nashangaaga mamtu meusi mengine yapo hapa Tz kupenda kujifananisha na waarabu.
 
Tukianza kutuma vituko wanavyofanyiwa mahousegirl katika majumba yetu utasema waarabu wana afadhali ni vile tu havisemwi kwanza kabisa anakuwa mtumwa wa ngono kama kuna vijana wakubwa watatu wa nne wote ujue watampitia baba mwenye nyumba nae hachezi mbali asilimia 70 ya wafanyakazi wa ndani wanakutana na kadhia hii
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom