Housegirl amchoma kisu mgeni baada ya kuambiwa “una roho mbaya kama sura yako”

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP, Ramadhani Kingai amethibitisha kifo cha kijana aliyechomwa kisu na dada wa kazi.

Ezekiel Nyamko mkazi wa Kimara, alichomwa kisu mara mbili kwenye kifua na mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa rafiki yake, tukio lililopelekea kifo chake.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa Nyamko alienda kumtembelea rafiki yake Kelvin ambaye wazazi wao pia ni marafiki na alipofika aliomba chakula lakini mtuhumiwa alimnyima na kumwambia kuwa bado wenyeji hawajala hivyo asubiri. Nyamko alimjibu kuwa “una roho mbaya kama sura yako” na kuongeza kuwa ndiyo maana Kelvin hamuoi.

Maneno hayo yalimkera mtuhumiwa na kufikia hatua ya kumchoma kisu kifuani mara mbili marehemu.

Mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Hapiness ameshikiliwa na polisi huku mwili wa marehemu ukiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi.
 
angemwambia tu sura yako nzuri kelvin atakuoa angekula had makoko siku hyo

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
Unapoenda kwa watu unatakiwa uwe na adabu na unachoongea
Pili kwenda kwenda kwa watu napo sio vizuri kila mtu akae kwake
Unaenda kwa mtu unaomba chakula na kutoa maneno hovyo si ungekaa kwenu au kwenda kutafuta vibarua huko ufanye
 
Hayo maneno aliyoyatamka marehemu nani aliyasikia? Au mtuhumiwa ndio alielezea?

Btw, Mtu unapoenda kwa watu jaribu kua mpole na kufata taratibu husika, house girl ni mfanyakazi anayeishi kwa kufata kanuni na sheria za mahali pake pa kazi, ujuaji unapaswa uuache getini huko sio uje umuharibie binti wa watu kazi kwa ujuaji wako.
 
Hayo maneno aliyoyatamka marehemu nani aliyasikia? Au mtuhumiwa ndio alielezea?

Btw, Mtu unapoenda kwa watu jaribu kua mpole na kufata taratibu husika, house girl ni mfanyakazi anayeishi kwa kufata kanuni na sheria za mahali pake pa kazi, ujuaji unapaswa uuache getini huko sio uje umuharibie binti wa watu kazi kwa ujuaji wako.
Mkuu hukusikia ile Story kuwa Shetani alienda Mbinguni akamuomba Mungu amjaribu Ayubu na Mungu Akakubali ila asimtoe roho tu na Shetani akakubali... Je Wajua nani aliwasikia tunayoambiwa hadi leo hii?
 
Back
Top Bottom