House girl kufua boxer zangu ni sawa kweli?

Kwa muda mrefu nimekua nikijiuliza swali hili kutokana na utaratibu uliopo nyumbani kwangu. Juzi nilikuta kuna ugomvi kati ya wife na house maid wetu, ambapo yule binti alikua amefura kwa hasira, kasimama katika mlango wa Chumba chetu akidai apewe pesa zake asepe usiku huo huo na alikua tayari ana begi mkononi.

Nikambembeleza, nikamuomba asiondoke usiku huo asubiri asubuhi, wife akatoka chumbani kama mbogo na kunigeuzia kibao kwamba kwanini nambeleleza kwamba nimwache aende na hapati hata senti, ukawa ugomvi mkubwa sana, ambapo binti kwa hasira akamjibu wife kuwa "" kama wewe ni mke bora usingeshindwa kumfulia mmeo hata boxer hadi unaleta kwangu, hufai""" kwa kweli sikuwahi kujua huwa anampa maid afue boxer zangu.

Huwa naona zimeshafuliwa na kupigwa pasi mimi navaa tu, juzi ndio niligundua hili suala, anyway yule binti alingangania kuondoka usiku ule kwamba yeye ni mtu mzima anajua anakoenda, tukaenda kwa Mjumbe nikampa nusu ya pesa anazodai zingine atarudia kama laki tatu hivi, kumbe siku zote nikitoa mshahara wife hampi anadai anamtunzia kwamba ataharibikiwa akimpa monthly.

Jana nikawa namuuliza wife kuwa kumbe boxer pia huwa unampa afue? Badala ya kunijibu kajikasirisha uongo na kweli ili tuiache hiyo mada, kwamba inakuaje nina mtetea housegirl hadi kufikia hatua kumbembeleza asiondoke, anyway hayo yakaisha.

Ila tu nikajiuliza swali hivi ni jambo la kawaida kwa maid kufua boxer zangu? Mimi ndio sielewi inavyokua maana wakati mwingine pale mbele ya boxer huwa panatengeneza miduara ya mabaki ya mbegu mara baada ya tendo usiku, yale matone huwa yanaendelea usiku na kukaukia pale.

Sasa ni sawa kwa housegirl kuifua nguo hiyo?

Kama vip piga tu
 
mmmmmm jamani simlaumu huyu mkaka kwakutokujua nani anafua boxer zake,lakini kwamtazamo wangu mimi au nisema kwa malezi na mapenzi yangu kwa mume na familia yangu,Boxer,flana za ndani niwajibu wangu mimi mke kufua kupiga pasi nakuziweka sehemu husika na mpaka usafi wa chumba changu choo changu nifanye mwenyewe kama mke, sasa mpaka H/G anafikia kufua boxer ya Mume wangu imebakia nini hapo zaidi ya kulala nae?

Mvivu kweli sikatai au nachoka na kazi lakini chakula chake na chochote kinacho muhusu yeye mimi ndio ntafanya sio dada wa kazi.....

Unajua wajibu wako.
 
Ni kazi kama kazi zingine hapo home... alafuu nini kinawafanyaga mshndwe kujifulia hizo makitu wenyewe au wewe na mkeo mnapeanaga zamu sasa zamu yake anampa maid?
 
Kuna wanawake wana roho ngumu, hata nguo za mume wangu nazifua na kuzinyoosha mwenyewe. Ni uvivu na kutokujua majukumu ya mke wako, kama umeona mkeo tabia yake ni hiyo sio mbaya ukawa unajifulia mwenyewe boxer zako kuliko kujidhalilisha kwa mdada wa kazi
 
Huyo mkeo kilaza, na wewe pia kilaza coz siku zote hujawahi kumuona anafua na mnalala wote one room. Housegirl anakaa mda mrefu hajalipwa na wewe hujui. Tell me again, we ndo kiongozi wa house? Halafu unakaa unalaumu viongozi wengine?
Na hapa ni kwa sababu mada ni hiyo ila inaonesha mambo mengi ya kwako hujui. Kwa mfano huyo house girl inaezekana ni mzuri sana wa kazi kiasi kwamba ni msaada lakini coz hujui u just let her go. Utapata tabu sana mbeleni brother!
OOh! +ndoa yako siyo strong. Kitu binafsi sana kama boxer kama mwanamke (hawa nnaowajua mimi) yuko tayari kushare na mwanamke mwenzie! Hakupendi kweli huyo
 
Boxer ni chupi..chupi ni nguo ya ndani tena veery sensitive..nnanzaje kumpa hg...lol...mkeo kilaza

mm naona mleta mada alisha mgeuza hg kuwa kama mkewe, nikiwa na maana kwamba anawagegeda wote, kwa hiyo hg naye anajiona ni mke!!!!
 
Asanteni wooote kwa kuchangia uzi huu.. cha muhimu tar 25 oct kapigeni kura halafu mrudi majumbani mwenu.
 
wewe ni mwanaume.com. tatizo ulipooa ulifikiri hadi chupi zako utafuliwa na mke na sio wewe mwenyewe. bahati mbaya mkeo ndio dot.com kuliko wewe hapendi kufua uchafu wako naye anapeleka kwa housegirl. matokeo yake ndio haya ya kuaibishwa na kudhalilishwa na housegirl na wewe tena unakuja kujiabisha na kujidhalilisha jamii forum
 
Mawazo potofu hayo, angalia michango mingi ya wanawake yanapingana na dhana yako, wengi tunaamini na ndivyo ilivya kwamba, mke ndie anapaswa kufua nguo za baba hasa za ndani, nguo zingine za baba ni sawa zinaweza kufuliwa na hg kutokana na mama kuwa busy na utafutaji, lakini nguo za ndani mama atazifua zake na za baba
Ndivyo ilivyo kwenye familia nyingi

Wale wanaodai baba ajifulie mwenyewe nguo za ndani, ni dhahiri kuwa sio wanandoa, nenda kwenye kitchen party zote utaambiwa straight away nguo za ndani za baba zinafuliwa na mama
Labda kosa la huyu bwana ni kutojua yanayoendelea nyumbani kwake
Hata hivyo ukirudi nyuma baba hapaswi kujihusisha na mambo ya hg, labda mambo ya watoto na sio Yale ya hg
 
  • Thanks
Reactions: Kig
Maskin house maids wanapitia magumu sana
Kwa mwanamke anayejitambua vizuri haitakiwi house maids kujua chumba chako na mumeo kikoje
kuanzia shuka unayolalia nguo za mumeo na usafi wa chumba chako asifanye yeye
Yule ni mumeo its responsibility to take of him
Nyie wanawake uvivu muache ukichapiwa na house girl usilie
 
Kwa muda mrefu nimekua nikijiuliza swali hili kutokana na utaratibu uliopo nyumbani kwangu. Juzi nilikuta kuna ugomvi kati ya wife na house maid wetu, ambapo yule binti alikua amefura kwa hasira, kasimama katika mlango wa Chumba chetu akidai apewe pesa zake asepe usiku huo huo na alikua tayari ana begi mkononi.

Nikambembeleza, nikamuomba asiondoke usiku huo asubiri asubuhi, wife akatoka chumbani kama mbogo na kunigeuzia kibao kwamba kwanini nambeleleza kwamba nimwache aende na hapati hata senti, ukawa ugomvi mkubwa sana, ambapo binti kwa hasira akamjibu wife kuwa "" kama wewe ni mke bora usingeshindwa kumfulia mmeo hata boxer hadi unaleta kwangu, hufai""" kwa kweli sikuwahi kujua huwa anampa maid afue boxer zangu.

Huwa naona zimeshafuliwa na kupigwa pasi mimi navaa tu, juzi ndio niligundua hili suala, anyway yule binti alingangania kuondoka usiku ule kwamba yeye ni mtu mzima anajua anakoenda, tukaenda kwa Mjumbe nikampa nusu ya pesa anazodai zingine atarudia kama laki tatu hivi, kumbe siku zote nikitoa mshahara wife hampi anadai anamtunzia kwamba ataharibikiwa akimpa monthly.

Jana nikawa namuuliza wife kuwa kumbe boxer pia huwa unampa afue? Badala ya kunijibu kajikasirisha uongo na kweli ili tuiache hiyo mada, kwamba inakuaje nina mtetea housegirl hadi kufikia hatua kumbembeleza asiondoke, anyway hayo yakaisha.

Ila tu nikajiuliza swali hivi ni jambo la kawaida kwa maid kufua boxer zangu? Mimi ndio sielewi inavyokua maana wakati mwingine pale mbele ya boxer huwa panatengeneza miduara ya mabaki ya mbegu mara baada ya tendo usiku, yale matone huwa yanaendelea usiku na kukaukia pale.

Sasa ni sawa kwa housegirl kuifua nguo hiyo?
Duuh aisee huyo wife balaa....yawezekana either anatoka kazini usiku khy hapati muda au labda ana kiburi...mara nyingi wanawake ambao wako private companies au wafanyabiwashara hawapatagi muda wa kukaa home hivyo kufanya vitu viende mrama...dawa yake kaeni mzungumzee aisee...wanakuaga bize kiasi cha kwamba hata unyumba hawatoii
 
Boxer sio ustaarabu maid akifua, mke ndiyo kazi yake, mimi hata kuanika nje huwa siruhusu maana nikukosa dira ya ustaarabu... All in all mkanye mkeo haraka kuacha hiyo tabia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom