'House Girl' jela kwa kuiba mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'House Girl' jela kwa kuiba mtoto

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Apr 20, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  'House Girl' jela kwa kuiba mtoto


  Na Rehema Maigala

  MSICHANA wa kazi za ndani Khadija Athumani (27), mkazi wa Kimara amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kuiba mtoto wa kiume jina
  Victory Charles (4).

  Kabla ya hukumu hiyo, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Bw. Mtani Magoma mbele ya Hakimu Bw. Athumani Nyamlani kuwa Februari 18, 2009 mshitakiwa alimuiba mtoto wa mwajiri wake Charles Aloyce.

  Mshitakiwa anadaiwa kumuiba mtoto huyo alipomfata kituo cha basi ili kumrudisha nyumbani kutoka shule.

  Shahidi wa pili ambaye ni dereva wa basi la shule alidai kuwa alimshusha mtoto huyo kama ilivyo kawaida na alimkuta pale kituoni dada wa mtoto huyo akiwa amesimama na wavulana wawili ambao ni wauza viatu.

  Alidai kuwa kwa kuwa wao walikuwa wanamsubiri mzazi mwingine kwa ajiri ya kumchukua mtoto wake, walimuona mshtakiwa anaongea na vijana hao huku na mtoto huyo akiwa hapo hapo.

  Mshitakiwa huyo alisema alimfata mtoto kituoni ambako pia walitokea vijana wawili wakamwambia kuwa wanamuomba mtoto huyo.

  'Waliniambia kuwa wanamuomba mtoto ili wanipe pesa lakini mimi niliwakatalia kwani nilikuwa siwaelewi, baada ya muda mfupi mtoto aliomba anataka kwenda kujisaidia nilimruhusu baada ya hapo sijamuona tena," alidai mshitakiwa huyo.

  Baada ya Hakimu kusikiliza usahahidi wa pande zote mbili alimuuliza Mwendesha Mashtaka kama mshtakiwa anakosa linginenaye akajibu kuwa hakuwa nalo, lakini apate adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

  Baada ya hukumu hiyo kusomwa ilisikika sauti za ndugu yake mtoto wakilia kwa uchungu wakidai kuwa, haisaidii kitu hata angefungwa kifungo cha maisha ni bora tungeona maiti yake kuliko kusoma misa ya wafu bila ya kujua mtoto wetu amekufa au la.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mchezo mwingine wa kuigiza, kwa maoni yangu polisi walifanya papara kupeleka hii kesi mahakamani. Polisi walitakiwa kufanya upelelezi wa kina kubaini kama mtoto ameibiwa kweli au ameuwawa kama mtoto kauwawa nini kitaendelea kwa mfungwa huyo? Na kama kuna watu waliomuiba kama mtuhumiwa alivyosema sio kwamba huyu binti atakuwa ameonewa.

  Ningekuwa mimi huyu binti ndio angekuwa shahidi muhimu kwani aliwaona waliomchukua.
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kesi hii inanikumbusha rafiki yangu aliyeibiwa mtoto wake 2001. Mtoto yule alikuwa na miaka 2 na house girl alipatikana tu njiani na akajenga mahusiano ya kutosha na yule mtoto na baadaye akamuiba. leo hii imepita miaka 10 na mtoto hajapatikana. Hali hii ilisambaratisha ndoa ya yule rafiki yangu.
  Kwa ujumla polisi wetu wanamatatizo saana. Bado tuko nyuma saana kwenye upelelezi. Yaani wanamfunga halafu? Zipo unsolved cases hata developed countries lakini jamaa huwa wanahangaika. Pia inawezekana huyo msichana alitapeliwa vinginevyo angesema alipo mtoto kwa namna tunavyojua polisi walipo. Kuna watu wanaweza mazingaombwe. Nakumbuka mtu mmoja yeye alienda kutoa vitu vyoote vya ndani na hakutaka kumsikiliza mtu mpaka wezi wake walivyoondoka.
   
Loading...