House Girl / House maids wanavyouzwa mtandaoni nchi za mashariki ya kati

mcshonde

Member
Jul 15, 2022
66
152
Kuna App inaitwa 4SALE. Humo unauza/nunua kitu chochote ikiwemo mtu.

domesticworkers.jpg


Kwa miaka kadhaa imetumika sana kuwauza kina dada mtandaoni. Kinachotokea ni kwamba; mabinti/dada walioenda nchi za mashariki ya kati kufanya kazi za ndani wanauzwa mtandaoni kama watumwa. Ukimtaka mfanyakazi unaingia kwenye App na kuchagua mtu na bei yake. Yaani bosi wako akikuchoka anakupiga picha na anaweka bei yako kama unavyopost bidhaa. Kama kakuchoka kabisaaa ataweka bei chee ili ununuliwe fasta. Kwa staili hiyo house maids wamekuwa wakihama nyumba moja hadi nyingine bila kujua nini kinaendelea.

Kwa kuwa wamenunuliwa kama bidhaa, ubinadamu haupo tena ndio maana huyo dada aneleza kuwa familia ilisafiri na walipofikia yeye aliambiwa alale kwenye zizi la ng'ombe...kwa miezi 3.

Kibaya ni kwamba hawawezi kukimbia mana bosi wako ana passport yako ...Lakini kwa wengine kwa wale walioingia nchini humo bila utaratibu. Yani walipitia chocho ukikimbia na ukakamatwa basi polisi wanakuweka ndani. Hiyo App imepigiwa kelele sana nchi za Mashariki ya kati kwamba imeondoa utu wa binadamu lakini bado wengi wanaendelea kunyanyaswa sana.

 
Inasikitisha, kuna binadamu bado hawana ubinadamu.

Waarabu washenzi saana ndio maana katika fikra zangu 2 juu ya mitume kupelekwa kwao, moja wapo hwa ni mitume wakapewa wao kwa ushenzi wao uliokithiri.
 
Ni ujinga uliokubuhu kwenda nchi za mashariki ya kati kufanya kazi.
Bara la Asia limejaa washenzi
 
Waarabu washenzi saana ndio maana katika fikra zangu 2 juu ya mitume kupelekwa kwao, moja wapo hwa ni mitume wakapewa wao kwa ushenzi wao uliokithiri.
Na hao maajenti waafrika pia ni washenzi waliokithiri kwani wao wanajua yanayoendelea na bado wanawapeleka ndugu na jamaa zao kwa tamaa ya fedha.
 
Halafu kuna waarabu wa kibiti wanavyowahusudu hao washenzi..huwa nashangaa sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na hao maajenti waafrika pia ni washenzi waliokithiri kwani wao wanajua yanayoendelea na bado wanawapeleka ndugu na jamaa zao kwa tamaa ya fedha.
ma agent nao hawana utu..kuna binti kigamboni alienda oman akakaa miezi 3 tu akataka kujiua. Huwezi amini agent wake alikuwa mjomba wake kabisa.

Pona pona ya binti ni jumuiya ikamchangia nauli na gharama za kumlipa mwenye nyumba ili ampe passport yake. sio poa.
 
Kuna App inaitwa 4SALE. Humo unauza/nunua kitu chochote ikiwemo mtu.
View attachment 2416250

Kwa miaka kadhaa imetumika sana kuwauza kina dada mtandaoni. Kinachotokea ni kwamba; mabinti/dada walioenda nchi za mashariki ya kati kufanya kazi...
Tanzania tunaye ajenti mbunge mmoja wa CCM aliyeruhusiwa na serikali kusafirisha wafanyakazi wa ndani japo jambo hilohilo linakatazwa mikoani!
 
Back
Top Bottom