House girl awawekea sumu familia ya kihindi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
21,995
Familia ya kihindi ya watu 5 imelazwa hospitalini baada ya
housegirl kuwawekea sumu na kuondoka na mali kadhaa
habari zaidi zinasema hadija binti ambae alikuwa akiwapikia
chakula wahindi hao aliamua kuwawekea sumu watu hao na hivi sasa
aijulikan sababu za kufanya hivyo na polisi bado wanamtafuta
habari zaidi zinasema baba mama na watoto waliolazwa wameanza kufungua
macho lakini kuongea bado wanasua sua...polen sana
aen vizuri na hao watu ndio walioshikilia maisha yetu sasa mkiamua mnavyotaka ninyi mtaisha..natumain aikuwa sumu mliwekewa aweze kuchukua anavyotaka
 
Inapaswa HGs muwapende, kuwathamini na kuwajari kama watoto/ndugu zenu - wameshikilia maisha yenu.

Kama house girl ni mtu wa kuamshwa saa 9 alfajiri, kulala saa 6, matusi na kejeri za ovyo ovyo, ipo siku utatoka job na kumkuta mwanao ndani ya freezer.

Be warned ndugu
 
inapaswa hgs muwapende, kuwathamini na kuwajari kama watoto/ndugu zenu - wameshikilia maisha yenu.

Kama house girl ni mtu wa kuamshwa saa 9 alfajiri, kulala saa 6, matusi na kejeri za ovyo ovyo, ipo siku utatoka job na kumkuta mwanao ndani ya freezer.

Be warned ndugu

kabisa ndugu zanguni hawa wameshikilia maisha yetu baadaa ya mungu wao;kama amuamini angalia walivyokula watuwatano
kirahisi wahsukuru mungu na nantumain aikuwa sumu...kingine muwe makini na hili la kula vyakula tofauti
kuna familia nyingi hapa tanzania sijui ni dharau ama wanakula chakula tofauti na hawa watu..ati wao wanapikiwa
wali na kuku na wao wanaambiwa wapike ugali na maharage kila siku wao wana fangus za koo jaman kuku aiingii????
Ama nyie ndie mmeandikiwa kuku...jaribuni kuwau=tunza kama ndugu mtaona furaha yake..m nasema hivi nina kijana aliletwa
toka uchagan ana miaka miwili naishi nae kama ndugu mpka nafurahi nikiacha nyumba najisikia iko salama...tukila anachopika tunachokula
maji anayochota tunayooga...msijitenge nao mtaumia...m nafikiri kabla ya kuhukumu polisi wakimpata waulize sababu..angekuwa na nia mbaya wangekufa ati we sumu kuanzia saa tano usiku mmpaka asbh mnabaki kukoroma mkiongeleshwa hoi..mshukurun akuwa na roho
ya kihehe angwamaliza....ama kuwalisha mbwa kabisa
 
Hawa wahindi tuwaone tu wakitembea barabarani ila kati ya watu waonevu, wanyanyasaji, wadhalilishaji ni hawa viumbe, dada wa watu naona uvumilivu ulifikia kikomo, alichokifanya ni namna moja ya kupinga maonevu,,,liwe ni fundisho kwa nyie wahindi msijifanye kama mko Mumbai wachukulieni watanzania kama binadamu pia lasivyo wakichoka wanaweza fanya lolote( Inawezakana huyo dada alikuwa anawapikia wafulia kuwashikia watoto - mshahara wake unaweza kuwa ni elfu kuninatano na matusi na manyanyaso juu
 
Ni kweli kabisa tuwapende hawa na kuwathamini ..moshi kuna mmoja aliwasha jiko na kuweka sufuria kubwa
kwenye moto kwa nini asimweke mtoto ndan akaanza kulia jiran kuja n aibu mtoto ashaungua upande akuaishi mungu amrehemu...walipomkamata akadai ajalipwa mshahara miezi sita anaambiwa mambo s mazur sikujua kesi iliishaje
kama m ni hakimu namweka ndan mfiwa na h/girl ...mfiwa atabeba nusu ya adhabu ya hgirl ka kusababisha kifo
so wakati mwingine sisi ni chanzo..tubadilike
 
Inapaswa HGs muwapende, kuwathamini na kuwajari kama watoto/ndugu zenu - wameshikilia maisha yenu.

Kama house girl ni mtu wa kuamshwa saa 9 alfajiri, kulala saa 6, matusi na kejeri za ovyo ovyo, ipo siku utatoka job na kumkuta mwanao ndani ya freezer.

Be warned ndugu
Wahindi ni wanyanyasaji sana. Wanaweza kumfanya mtu akapata kichaa cha muda na kufanya lolote lile. Si kwa housegirls peke yao bali hata kwa wafanyakazi wazawa kwenye ofisi au viwanda vyao. Labda binti manyanyaso yamezidi akaamua kuwakomesha na kujiondokea. Sasa kama waathirika hawajitambui wala kuongea mmejuaje kwamba amewaibia? Bwana, fanya kazi nyingine yoyote lakini si kwa muhindi.
 
Alichoshwa na kazi na maisha ya uhindini huyo, nafahamu the way wanavyowatreat mahouse girls, huyu alidhamiria kupoteza ushahidi na kupata cha kuanzia maisha........
Ila ni mbaya sana , inatisha coz hawa watu hawakawii kuiga na kufanya kazi kwa history.
Tuwe makini kwa wale tunaoacha watoto na wafanyakazi
 
Hawa wahindi tuwaone tu wakitembea barabarani ila kati ya watu waonevu, wanyanyasaji, wadhalilishaji ni hawa viumbe, dada wa watu naona uvumilivu ulifikia kikomo, alichokifanya ni namna moja ya kupinga maonevu,,,liwe ni fundisho kwa nyie wahindi msijifanye kama mko Mumbai wachukulieni watanzania kama binadamu pia lasivyo wakichoka wanaweza fanya lolote( Inawezakana huyo dada alikuwa anawapikia wafulia kuwashikia watoto - mshahara wake unaweza kuwa ni elfu kuninatano na matusi na manyanyaso juu

MKUU, hapa sikubaliani na ww kabisa.
Huyu housi geli ni muuaji tu, hatakama angekuwa kwako angefanya hivo tu (kisingizio mkeo anamnyanyasa). mwaka jana haus geli aliwekea sumu watoto wawili wakafa, mama yao alipopewa habari na akapatwa na mstuko akafa! habari nyng za hausgeli kuwatendea visivyo watoto wa wenye nyumba...! nao ni wahindi.
kikubwa unapochukua hausigeli uwe mwangalifu, umjue atokako na hata background yake, mwingine unaweza kumpenda kama mwanao ukamkuta vichochoron akikusema maneno mabovu kwa majirani!
 
Ni kweli kabisa kwa mfano unaweza kupata kazi ya udereva kwa Muhindi lakini kuwa tayari kufanya kazi yoyote ile mfano Kufua nguo, Kudeki, Kupika, Kutumwa sokoni, kupeleka watoto shuleni. Pia pale kama nyumba ina wahindi 10 basi wote unariporti kwao sasa inakuwa kero tupu. Kwa hiyo mimi sishangai huyu mfanyakazi alivyoamua kuwatendea kitendo kama hiki may be alikuwa matesoni bila malipo.

Nafikiri itakuwa fundisho kwa wahindi wengine tabia zao za kufanya wenzao si binadamu.
 
Inapaswa HGs muwapende, kuwathamini na kuwajari kama watoto/ndugu zenu - wameshikilia maisha yenu.

Kama house girl ni mtu wa kuamshwa saa 9 alfajiri, kulala saa 6, matusi na kejeri za ovyo ovyo, ipo siku utatoka job na kumkuta mwanao ndani ya freezer.

Be warned ndugu

Ni kweli usemayo ila tu kwa kifupi mabinti wa kazi na house boy pia kuna ambao ni majambazi wanaoibukiwa. Siku hizi wanatumwa kwa matajiri ili kuchora ramani na kuwakabidhi wenye mitutu!!! Kuna kesi nyingi za namna hii, mfano ile ya Balozi Mutalemwa binti wa kazi alikuwa ni jambazi japo hakutumia silaha lakini aliiba mali nyigi sana akishirikiana na watu wengine na alifungwa miaka 15 jela, kuanzia January 2009. Kuna wengine wengi wa aina hii pia hasa wahindi. Kumbuka kuna binti alishirikiana na majambazi na kuwaibia wahindi ambapo waliua, sijui ile kesi iliishia wapi!!! Kuna mabinti wengine pia wanatumwa kuwamaliza mama wenye nyumba ili wapate kuwachukua waume zao, kuna mfano hai huko Arusha!!! Kwa hiyo siku hizi si suala la kuwa wakorofi kwa hawa house boys/girls bali wao wamekuwa ni watu wasioaminika tu. Kinachotakiwa sasa kwa wale ambao mna uwezo ni heri muanze kushi kama ulaya!!! No maid, wazazi mnapeana zamu kuhudumia watoto ikiwemo kuwafuata na kuwapeleka shuleni. Sema miundo mbinu yetu ni mibovu ula kuna baadhi ya maeneo sasa kuna Day Care Facilities ambazo unampeleka mtoto mdogo kushinda. Inasaidia kuliko hata kumuacha mtoto wako na House gilr ambaye ukitoka tu naye anatoka kufuata mabwana huku akiwa amemtinga mtoto wako mgongoni au analeta wanaume varieties ndani mwako na yule mtoto wako anashuhudia kila ushenzi anaofanya binti huyu!!! It is very complicated when addressing domestic workers!

House girl anashika nafasi kubwa kwa mama hasa katika muda mama anapokuwa katika mihangaiko na baba ya kutafuta riziki
na wana uwezo mkubwa sana wa kukatiri maisha ya family hasa pale atakapohisi family inamchukulia kama sio sehemu ya jamii
Tuwapende na kuwathamini kama ndugu!
 
Mhh sijui nimuhukumu nani!!

siyo kazi yako. unadhani wafanyakazi wa tz wangekuwa mahausigeli wa mkuu. siku ya hotuba waambie wamwandalie chakula na wawe na access ya vichupa vya sumu ingekuwaje?
 
MKUU, hapa sikubaliani na ww kabisa. Huyu housi geli ni muuaji tu, hatakama angekuwa kwako angefanya hivo tu (kisingizio mkeo anamnyanyasa). mwaka jana haus geli aliwekea sumu watoto wawili wakafa, mama yao alipopewa habari na akapatwa na mstuko akafa! habari nyng za hausgeli kuwatendea visivyo watoto wa wenye nyumba...! nao ni wahindi. kikubwa unapochukua hausigeli uwe mwangalifu, umjue atokako na hata background yake, mwingine unaweza kumpenda kama mwanao ukamkuta vichochoron akikusema maneno mabovu kwa majirani!

Mhesimiwa Amoeba, house girls ni watoto wa kawaida wanaotoka kwenye ndani ya jamii zetu. Sio sio wauaji kama unavyosema. Sina uhakika huko kwenye familia yako unaye na ninamna gani unahusiana nae. Jaribu kufanya utafiti uone jinsi mahausi girls wanavyo teswa. Wanachukuliwa kama watumwa , hawana haki yakujisikia kama wanaishi. Wanakupikia kuku halafu wakula ugali kwa maharage, chai ya rangi daima wakati unauza maziwa.
Ujue hakuna mtu anayependa kumtumikia mwingine, tunawapata hawa ili kututumikia sikwasababu wanataka bali kwasababu ni maskini na hawaji jinsi yakujikimu. Hivi unadhani kunamzazi anapenda mtoto wake akawe house girl? Jiweke kweny hiyo nafasi, binti yako anafanya kazi kwa mtu, anaamka saa 10 usiku, kulala mpaka saa 6 usiku tena. Harusiwi kukaa sebuleni, akionekana anaanglia TV ni matusi. Hali mpaka mbosi washibe na chakula anachokula bosi kikibaki ni cha mbwa, haruhusiwei kukionja, wake ni ugali tu. Niambie ungejisikiaje? Kama hupendi binti yako atendewe hivyo, usijaribu kwa wamwenzio. Kumbuka hakupenda kuwa maskini. Tukishawatesa sana inafikia hatua wakishachoka wanaweza kufanya mabo ambayo huwezi kuamini. Wakifanya hivyo tunawalaani nakusema mahause girls ni wanyama, tunasahau kwmba unyama huo tumeutengeneza sisi wenyewe. Tuwe makini sana jinsi tunavyoishi na wawatoto wa watu. Tuwapende nakuwafanya wajione kwamba na wao wko duniani.

Sijui hao wahindi wliamfanyaje, lakini hukuna jema litokalo kwa muhindi. Kumbuka wahindi kimila zao wanamatabaka ya watumwa na Untachable huko kwao, unategemea wamfanyie nini mtoto na tena wanajua ni maskini??? Wacha wajifunze kidogo. Huyo binti wala asitafutwe, na akipatikana aulizwe kwa upole aeleze kulikoni na sio kuhukumiwa tu eti kwasababu waliolishwa sumu ni wahindi. Watanzania tunaabudu wageni, Hata wahindi. Nendeni India mkawaone walivyo ndo mtawadharau.
 
Duuuuh!!!!Wengi mnashangalia wahindi kutaka kuuwawa?Kisa ni wahindi?Hivi njia ya kuwaadhibu hao wahindi ni kuwawekea sumu wafe kisa wananyanyasa ma house girl?
 
...Umenena Vyema. Ukute huyo Bint Pamoja na kuhenyeshwa koote, hajapewa mshahara wake kwa miezi! true, Unyama wa hawa mabinti mara nyingi tunautengeneza sisi wenyewe tunaojifanya tumeenda shule!
 
naona tunampa loop hole mtia sumu kwa kuwa alikuwa akifanya kazi kwa wahindi! labda wangetiliwa sumu watu wa watu wa ngoz nyeusi ndio tungesema mtia sumu kafanya makosa!

hata kama wahindi walimuonea, hana haki ya kuwatilia sumu, alikuwa aondokea mapema au akimbilie kwenye vyombo vya sheria.
 
...Vyombo vya Usalama? Vipi? hivi vya Bongo?? Good luck to her! Mkuu, sio kwamba tunampa loophole mtia sumu kwa sababu waliofanyiziwa ni wahindi, la hasha. Na ndio maana mimi nimekazia kuwa wote sisi, wahindi kwa wabantu, mara nyingi Tunautengeneza wenyewe unyama wa wafanyakazi wetu!
Kubwa ni kwamba there is an element of madness in all of us waiting for a sababu to surface. Inawezekana kwa binti huyu ilikuwa ni kutemewa mate na mwajiri wake. Inawezekana wewe na mimi ni siku tukimkuta mtu anajituma juu ya kifua cha tuwapendao. Your Madness may want to you to run to the Vyombo vya Usalama but I know for sure that my Madness will tell me to take out my Gun and end the matter there and then....!:rofl:
 
Back
Top Bottom