House girl au mgeni wa muda mrefu asiruhusiwe kwako bila kupima HIV, Hepatitis B na C, VDRL, H. PYL

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
653
Napenda kutoa ushauri kwenu wadau,

Kumekuwa na ongezeko la magonjwa haya kwenye jamii. ukimwi umekuwa ukipungua ingawa kwenye baadhi ya mikoa umekuwa ukiongezeka na prevalence iko kwenye 5.1% (mfano kilimanjaro, njombe nk) homa ya ini inayoenezwa na virus au Hepatitis B na C vimekuwa vikiongezeka sana njia za ueneaji wa haya magonjwa ziko sawa ingawa kunaweza kuwa na tofauti kidogo najua njia hizi zinafahamika lakini mimi nitazungumzia njia moja tu ambayo wengi wemekuwa wakiiacha

Unakuta mtu ana pesa ya kutosha, anamwajili house girl nyumbani kwake na anamwacha kwa muda mrefu na mtoto yapo mambo mengi sana kwenye malezi, kuna wengine huwatafunia chakula watoto na kuwapa, wapo wangine hushirikiana na mtoto kwa ukaribu sana na njia nyingi ambazo inawezakana hatuzifahamu.

Mazingira haya ya house girl yanaweza kuahatarisha afya ya mtoto kama yeye mwenyewe hayuko salama serikali kwa nia njema imeruhusu maabara binafsi za afya na vituo binafsi vya afya kwa ajili ya kuvuta huduma kwenye jamii na kuwaondolea watu usumbufu wa foleni nendeni mkawapime hawa watu kama wako salama kukaa na watoto wenu au la. yapo magonjwa mengi yanayoweza kupimwa kwa haraka na kuwasaidia watu wengi kwenye maabara binafsi, hospitali binafsi na makongamano mbali mbali.

Naombeni tubadilishe utamaduni wa upendo wa mshumaa na kuwa na tahadhari na kuwakinga watoto wetu dhibi ya magonjwa tunayoweza kuwakinga kazi kubwa na takatifu ya mzazi ni kuhakikisha usalama wa familia kwa gharama yoyote hili linakuja kwa ndugu pia, usiwapende kiasi cha kuwaamini kwa kila kitu kama atakaa muda mrefu ni vyema kuwapima na kujiridhisha ili kama kuna shida uchukue tahadhali.

Wapo watu wengine walioathrika huwa na nia mbaya ingawa sio wote wapo wengine anaweza kutumia tooth pick na akairudisha kwenye kopo, pia wapo unakuta anaamua tu kushare mswaki na watoto wakati anajua au mwingine unakuta hajui najua wote tutakufa lakini hatutakiwi kuamua kufa either kwa uzembe wetu namna nyingine ni vyema kuwakinga tuwapendao na kujitahidi kwa kadri ya uwezo wetu na pale tunaposhindwa tumwachie Mungu huo ni ushauri kwa wanajamvi na michango zaidi kuelimishani inakaribishwa.
 
Hivi siri ya mgonjwa na daktari (taarifa za mgonjwa) ina nafasi gani hapo?
 
kama ni mwajiri wake nina haki ya kujua afya yake.hata serikali inapokuajiri lazima uwe na medical examination form
medical examination report lazima iwepo ili uweze kupata ajira, hii imewekwa kwa lengo zuri kabisa
 
Hlo neno tena la maana sana kwa sababu kumekuwa na taarifa nyng sana hasa za wafanyakaz wa ndan kuwaambukiza magonjwa watoto wa mabosi wao kwa makusudi
Nlisikia moja hyo house girl kajikata wembe akamkata na mtoto
Na kiukwe ugonjwa wa HOMA YA INI kwa ss katika jamii yetu upo kwa kiwango kikubwa sana ingawa jamii haina uelewe kabisa kuhusu kitu hk
 
Na mama mkwe wako utaenda kumfanyia medical exam? Shuleni vipi utadai cheti cha daktari cha mwalimu, matron, mpishi, na watoto wenzake wote? Maana nakumbuka tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunapeana pipi hata ya mdomoni, tunamegeana ashkrim (ice cream iso na cream) kwa mdomo etc. Acha kazi ulee mwenyewe watoto, home school them mpaka wapate akili aka paranoia ya germs kama yako. Ikibidi wafungie kwenye sterile room tuone hiyo immunity yao itavyokuwa.
 
Kitu kizuri ni kuweka msisitizo hasa kwa chanjo ya hepatitis maana muingiliano hauepukiki..watu wanachepuka hawatumii kinga Waikati uezekano wa kuleta hiyo hepatitis nyumbani.Kitu kizuri serikali imeweka hiyo chanjo kwa watoto itafika mahali kutakuwa na free generation ya hepatitis..ngoma nayo ni shughuli maana waweza kumpima wakati anakuja afu akapatia huo ukimwi akiwa kwako.. Cha msingi ni kumfundisha ustaarabu na kuelekeza watoto tabia hatarishi
 
Na wao wana haki ya kukupima? Maana wao wana wasiwasi na wewe kuliko unavyofikiri.!!!
 
Na mama mkwe wako utaenda kumfanyia medical exam? Shuleni vipi utadai cheti cha daktari cha mwalimu, matron, mpishi, na watoto wenzake wote? Maana nakumbuka tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunapeana pipi hata ya mdomoni, tunamegeana ashkrim (ice cream iso na cream) kwa mdomo etc. Acha kazi ulee mwenyewe watoto, home school them mpaka wapate akili aka paranoia ya germs kama yako. Ikibidi wafungie kwenye sterile room tuone hiyo immunity yao itavyokuwa.
kwa hiyo unamaanisha waendelee kumungunya na kupokezana pipi. utampima tu tena ni rahisi zaidi. serikali imeona umuhimu wahili na ndio maana imeamua kuwapa chanjo wafanyakazi wote wa afya.hata mkwe ni njemaapime kama anatafunia watoto chakula.swala ni kukinga watoto. tuna watu wana ukimwi na waliathirika kwa kukaa na watu waliothirika sababu ya kuto kupata elimu sahihi. house girl apimwa kama inavyofanya serikali kupima waajiriwa wake.pia utofautishe zama.kila zama ina mambo na majanga yake. mimi nimeyaona na kuyashuhudia. nikazi ndogo sanakumpima mtu. medical examination kwa watu ni kitu cha kawaida sana. homa ya iniinaongezeka sana. pia ni ushauri na mjadala.kama wewe unaona huwezi its ok wala usihangaike. ila kama unaweza fanya
 
pia mw
Na mama mkwe wako utaenda kumfanyia medical exam? Shuleni vipi utadai cheti cha daktari cha mwalimu, matron, mpishi, na watoto wenzake wote? Maana nakumbuka tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunapeana pipi hata ya mdomoni, tunamegeana ashkrim (ice cream iso na cream) kwa mdomo etc. Acha kazi ulee mwenyewe watoto, home school them mpaka wapate akili aka paranoia ya germs kama yako. Ikibidi wafungie kwenye sterile room tuone hiyo immunity yao itavyokuwa.
kuhusu shuleniwalimu wa watoto sheria inasema hawatakiwa kuwagusa watoto kama hawajapimwa.huwa wanatakiwawapimwe wakati wa kuajiliwa. kama wameathirika na haya magnjwa kuna namna ya kuwashauri na kuwaelimisha na kuwatibu. pia ni vyema kujitahidi kufanya yale yanayowezekana kwenye uwezo wako na mengine tusiyo weza Mungu anajua
 
Na wao wana haki ya kukupima? Maana wao wana wasiwasi na wewe kuliko unavyofikiri.!!!
pia ana haki. kanisa la TAG hata ndoa haifungishwa mkikutwa mmoja ameathirika na mwingine hajaathirika. haya ni mambo ya msingi mno
 
Hlo neno tena la maana sana kwa sababu kumekuwa na taarifa nyng sana hasa za wafanyakaz wa ndan kuwaambukiza magonjwa watoto wa mabosi wao kwa makusudi
Nlisikia moja hyo house girl kajikata wembe akamkata na mtoto
Na kiukwe ugonjwa wa HOMA YA INI kwa ss katika jamii yetu upo kwa kiwango kikubwa sana ingawa jamii haina uelewe kabisa kuhusu kitu hk
ni rahisi sana kupima.nashindwa kuelewakwa niniwatu wanona ni ishu. moja ya kigezo cha kumwajili mtu ni kujua afya yake. mtu anakwenda kukaa na watoto wako alafu hutaki kujua afya yake
 
Solution ni kuwachanja watoto kwa ajili ya kinga ya Hepatitis B & C. Ni sindano 3 tu ndani ya miezi 5 umemaliza dose. Kwa sisi health practitioners ni lazima kuchanja chanjo hii kwa sababu ya interaction na wagonjwa. Kila mara mkuu alikuwa anatutangazia & Nilikuwa napuuzia, lakini baada ya daktari mmoja kufa kwa Hepatitis C, ilinibidi nichanje mwaka jana & nilimaliza sindano zote 3. Sasa, sina woga kuwakaribia wagonjwa.
safi sana kaka.nakupongeza kwa hilo kabisa.nijambola maana.nasisitiza hata house girl apimwe na watu wengine ukiwezauwapime HIV na hepatitis
 
You bush lawyers. Ukitaka kuhalalisha hoja unasema sheria inasema. Ipi? Taja na kifungu. Uwongo wa mitandaoni unasemwa mpaka unafanana na ukweli. Shame on you
 
Unapoelekea sasa utaanza kuwacheki hadi HVS, Pelvic USS, Rct Swab & UPT ili ujiwekee guaranteed rate ya kujiselfisha taratiiibu.
 
Back
Top Bottom