House girl anapomuua mtoto! Wewe ndiyo chanzo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

House girl anapomuua mtoto! Wewe ndiyo chanzo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Profesa, Apr 27, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Familia moja ilikua na House Girl, alikua haruhusiwi kukalia sofa sebleni, haruhusiwi kula meza moja na familia ya mwajiri wake japo chakula kapika yeye, alilalia godoro jembamba la nchi 1.2 lililotumika kumpumzishia mtoto hapo kale,chumba chake kilikua ni choo cha nje kilichojaaga zamani,na kuzibwa kwa mbao, wakati wa kuangalia tamthilia, aliruhusiwa lakini akae mbali sana tv,jukumu lake ni kusafisha nyumba ya room 4, sebule, jiko na vyoo 3,kupika,kufua,kulisha mifugo,kumpeleka mtoto shule na kumchukua jioni na kuosha mabanda ya mifugo. hakuwahi kuitwa kwa jina lake, kila mtu kwenye nyumba alimwita kwa jina la msichana. alipewa mshahara wake wa Tsh 20,000 mara mbili tu kati ya miezi 8 aliyofanya kazi.aliambulia matusi na makofi. hasira yake ilikua ya moyoni kila kukicha kwake ni mwanzo wa mateso mapya. Kwahali hiyo msichana yule alirudisha hasira zake kwa mtoto.kilichotokea ni mauti kwa mtoto...

  Huu ni mfano nilioukuta kwenye Face Book, in reality tunapoingia mjini tunaishi na ndugu, wengi nilioishi nao, hii stodi sio ngeni maana, versions za stori zinatofautiana ila mantiki ni ileile unyanyasaji ambao mimi nimeshuhudia live. Hawana aibu, dini wala utu wanaowafanyia wasichana wa kazi hivi. Binadamu wenzao wanaoithaminisha nyumba yao na kuweka watoto wao na mali zao salama miaka yote. Siwezi kuamini.
   
Loading...