House Cleaning

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
541
Eti jamani, kama tumejaliwa tuna kanyumba kako compicated kiasi, tuseme kama ka EL kule monduli, tukiajiri house cleaners kadhaa, wakisafisha nyumba nzima akuwa vibaya?
namaanisha vyumba vyote hata cha baba na mama.
au mama kusafisha chumba chao ni mila ya vijumba vidogo?
naomba ufafanuzi mwenzenu
 
no no no no ! chumba chenu "wandani" nafikiri kinatakiwa kiwe strictly kwa ajili yenu, usafi nyinyi, uroda nyinyi.... huo uvivu ni wa aina gani dada yangu ?
 
utasafishiwa hadi mwenza wako..oh hoooo kwani wadhani wenzio hawapendi kufaidi unayofaidi weye ndani ya nyumba??tena ndo watajitahidi kuyarudi hadi wahakikishe weye watoka humo ndani wao wanaingia...achaga uvivu huo kabsaaa wakat waolewa kwani ulikua wasafishiwa??si ndo ulikua busy kila siku kungarisha ili tu mapenzi yazidi??sonow uko ndani ushazoea waona ni kibarua cha wasafishaji ehh???haya bidae usije tuletea malalamiko umekuta unasafishiwa mwenzi wako ndani hiyo chumba chenu
 
Eti jamani, kama tumejaliwa tuna kanyumba kako compicated kiasi, tuseme kama ka EL kule monduli, tukiajiri house cleaners kadhaa, wakisafisha nyumba nzima akuwa vibaya?
namaanisha vyumba vyote hata cha baba na mama.
au mama kusafisha chumba chao ni mila ya vijumba vidogo?
naomba ufafanuzi mwenzenu

Mazoea mazoea mbwa aliingia hadi msikitini,
Chumba ni sehemu ndogo sana ya nyumba ambapo mama au baba anaweza akasafisha bila kuhutaji msaada wa house cleaner(girl/boy).Bedi room ni sawa na ikulu,Hata nyumba iwe simple au complicated,chumba cha baba na mama ni mahali patakatifu ambapo hadi uhakikishwe ndipo uingie
 
usafi wa chumba chenu ni wewe mwenyewe mwenzangu, chumba kinabeba siri nyingi na aibu nyingi pia .... zako na za mume wako ... mtu wa nje anaweza akakudharau kwa kitu kidogo tu akiingia chumbani kwako .. huenda mathalan umezidiwa au unaumwa ukaacha kufuli chafu chini, au hata mumeo kahifadhi hela kwenye kabati lenu ... akiiba mfanyakazi mumeo huenda akakushuku wewe ... na tena hao ma hausigeli wa kuokota anaweza hata akakutilia uchawi chumbani maana kila moja ana malengo yake na roho yake ... ukajikuta ndoa inayumba au kuvunjika kabisa... na hata kila kukicha akitandika kitanda ujuwe kuna siku nae anatamani akilalie .. akifanya juhudi tena kidogo tu anafanikiwa maana .. sikuhizi wanaume hawaeleweki akili zao zimekaa kwenye zipu.

Kuna wanawake wengine fyatu kweli, awapo chumbani au kitandani na mumewe tayari hanyanyuki kwa uvivu uliyokidhiri kama kasahau kitu atamuita housegeli aje amletee huku kajikunyata kitandani kama kakomelewa msumari.

Hata watoto wako, dada zako au mtu mwengine yeyote mfundishe kukugongea ... maana you make it out of bounds for everyone .... kama hata unaweza tembea na funguo kila ukitoka jifunze kufunga mlango wako

... enough for today
 
sikuhizi wanaume hawaeleweki akili zao zimekaa kwenye zipu.

Ahahahahah,naima hapo umenifurahisha, akili zimehama ziko kwenye zip, u cdnt have said it better!!! wananume nanyi mujitahindi kurudisha akili kwenye normal residence!

the bedroom MUST be out of bounds kabisa, hsegal kazi yake siyo kuja kukutandikia kitanda, ukimfumania na mumeo usijemlaumu yeyote. heri hicho kitanda ukitandike ukirudi kutoka kazini kama huna tme asubuhi etc.....
 
usafi wa chumba chenu ni wewe mwenyewe mwenzangu, chumba kinabeba siri nyingi na aibu nyingi pia .... zako na za mume wako ... mtu wa nje anaweza akakudharau kwa kitu kidogo tu akiingia chumbani kwako .. huenda mathalan umezidiwa au unaumwa ukaacha kufuli chafu chini, au hata mumeo kahifadhi hela kwenye kabati lenu ... akiiba mfanyakazi mumeo huenda akakushuku wewe ... na tena hao ma hausigeli wa kuokota anaweza hata akakutilia uchawi chumbani maana kila moja ana malengo yake na roho yake ... ukajikuta ndoa inayumba au kuvunjika kabisa... na hata kila kukicha akitandika kitanda ujuwe kuna siku nae anatamani akilalie .. akifanya juhudi tena kidogo tu anafanikiwa maana .. sikuhizi wanaume hawaeleweki akili zao zimekaa kwenye zipu.

Kuna wanawake wengine fyatu kweli, awapo chumbani au kitandani na mumewe tayari hanyanyuki kwa uvivu uliyokidhiri kama kasahau kitu atamuita housegeli aje amletee huku kajikunyata kitandani kama kakomelewa msumari.

Hata watoto wako, dada zako au mtu mwengine yeyote mfundishe kukugongea ... maana you make it out of bounds for everyone .... kama hata unaweza tembea na funguo kila ukitoka jifunze kufunga mlango wako

... enough for today

Dada Naima akili zetu bado ziko mkichwa...:)...Shishi usiniulize swali tafadhali naona umekaa chonjo kunirushia swali....:) lakini wengi hatupendi kufuliwa, kusafishiwa chumbani kwetu na hata kupikiwa na house girl au house boy!! Ni uvivu wa hali ya juu kutaka kufanyiwa hata vitu kama hivyo na mfanyakazi wa ndani
 
Eti jamani, kama tumejaliwa tuna kanyumba kako compicated kiasi, tuseme kama ka EL kule monduli, tukiajiri house cleaners kadhaa, wakisafisha nyumba nzima akuwa vibaya?
namaanisha vyumba vyote hata cha baba na mama.
au mama kusafisha chumba chao ni mila ya vijumba vidogo?
naomba ufafanuzi mwenzenu

Good question...
Kama ulisoma kuhusu usafi ktk kitabu cha darasa la nne cha kiswahili kuhusu ile familia ambayo ilimpoteza dada kwa malaria yaliyotokana na uchafu, na maamuzi ya wanafunzi kujitolea kusaidia usafi wa nyumba utakuwa umepata somo hapo. Kama mwenye nyumba haoni uchafu halafu uvundo unasumbua hadi kwa jirani itabidi wanajamii waisafishe nyumba ile au hata kuiweka karantini ili maradhi yasisambae..... Imekuwaje hadi nyumba iwe chafu na iachwe chafu????

KadaMpinzani said:
no no no no ! chumba chenu "wandani" nafikiri kinatakiwa kiwe strictly kwa ajili yenu, usafi nyinyi, uroda nyinyi.... huo uvivu ni wa aina gani dada yangu ?

Mkuu hawaoni kama uchafu ni kero kwao..... dawa ni kuwaingilia na kufanya usafi au la kuwatenga na jamii mpaka wawe wasafi na wastaarab....

Nimeiona hii ipo kama pilitrick vile....
kwa hiyo tusiinyooshee ccm vidole ikiwa inanuka??? hata shuleni mwanafunzi mchafu hurudishwa home akaoge
 
Eti jamani, kama tumejaliwa tuna kanyumba kako compicated kiasi, tuseme kama ka EL kule monduli, tukiajiri house cleaners kadhaa, wakisafisha nyumba nzima akuwa vibaya?
namaanisha vyumba vyote hata cha baba na mama.
au mama kusafisha chumba chao ni mila ya vijumba vidogo?
naomba ufafanuzi mwenzenu

...hakuna ubaya, hasa ukiajiri cleaners wakike, tena wale vigori wabichi wabichi... hao ndio hard workers tena wana nidhamu sana!
 
Ukiweka house gyal hesabu umeleta mke wa pili.
Na hivi huwa wamama wenye nyumba huwa hamuwajali kwa mavazi au kwa maradhi.
Basi akiwa na nguo zake zile hivyo hovyo au khanga kwa kuwa hana nguo nzuri ya kumsitiri.Huwa anaacha utamu wote nje....

Na mnapenda kuwaleta wale wototo kwa kuwa mnaweza hata kuwachapa na kuwafukuza,sasa hao mnao sema akili ziko kwenye zipu ndio hapo sasa wataka.
(Just kuwatisha ila wawe wachapakazi house gal chumbani kwenu kwanini?)
 
wengine hawatandaki hivyo vitanda na hawana house girl pia, kutandika kitanda yaweza kuwa kazi ya mwenzi yeyote inategemea na makubaliano yenu.

Jumba complicated la nini? kwa nini kutokuwa na nyumba simpo ambayo ni rahisi kuimudu bila kutaka msaada! hii inakuwa kuendekeza kauvivu fulani. Ikibidi sana kuwa na msaidizi kwa nini usitafute yule anayeweza kuja kukusaidia na kuondoka? say anakuja mara mbili kwa wiki, jumatano na jumamosi may be kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa na unamlipa kwa siku.
 
lakini wengi hatupendi kufuliwa, kusafishiwa chumbani kwetu na hata kupikiwa na house girl au house boy!! Ni uvivu wa hali ya juu kutaka kufanyiwa hata vitu kama hivyo na mfanyakazi wa ndani

Sometimes sio kwamba ni uvivu bali kuchoka na ratiba za kazi/biashara. Let say mke anafanya kazi pia, na anakuwa na ratiba ngumu ambapo kurudi kwake nyumbani jioni sana labda mbili usiku, sidhani kama atakuwa na nguvu tena za kuingia jikoni na kuanza kuandaa chakula, mbali tu ya kuchoka, muda pia utakuwa umeenda sana na kula chakula usiku zaidi sidhani kama ni vema. Of course, akiwa off days, hayo yote yanawezekana. The point is sio uvivu ama kwamba hatupendi kuwajibika kihivo, ila ratiba za kazi/biashara zinatubana sana na hatupendi kukaa nyumbani (Goal keepers).

Call me Lizy.
 
Lizy ukirudi mbili usiku uko nyeng'e bin nyeng'e unataka uoge, ule na ukalale au uangalie vipindi vyako kwenye TV labda mpaka saa tano ya usiku. Njemba, ikikugusa...inaambiwa not tonight sweetie, I am very tired. Hii inakuwa order of the day Monday to Friday, kama ndio unafanya biashara/kazi na weekend mambo ndiyo yanakuwa mazito zaidi. Njemba inatafuta nyumba ndogo na kwenda kupumzika huko. Nakumbuka mwanaJF mmoja aliwahi kulalama kuhusu maisha kama haya, na akasema anachat sana na wanawake mbali mbali kwenye mtandao maana mamsap hana muda naye ama kachoka au anaangalia 'vipindi vyake' alivyorekodi. Mnaendelea hivi kwa muda, halafu mnakuja kugundua kwamba pamoja na kuwa mnaishi nyumba moja lakini mnaishi separate lives kila mtu kivyake vyake, na mara nyingi mkija kugundua it is too late!!.

Hmmmm! Maisha ya ndoa tangu zamani yalikuwa magumu, lakini sasa hivi ugumu umeongezwa zaidi na vitu kama TV, internet n.k.
 
Mh, hii sasa sina neno best.

May be I should put my point clear. Ni kwamba kwa suala la kupika sometimes wamamme wanatakiwa wawaelewe wake zao wenye ratiba ngumu kwamba sio kila siku wataweza kuwaandalia chakula.
Suala la usafi (nyumba, kufua, kunyoosha nguo) vile sio la kila siku, hizo kweli we can manage (we have to do).

Hilo suala la "akiguswa na responce ya Sweet not today, Im tired", then kutakuwa na kitu hakiko sawa hapo and should be discussed in details.
 
mhm things somehow ni too funny...wakati mwanamke huyo huyo anaolewa alikua na kazi na bado alikua anashughulika ipasavyo...au wakati wakiwa wachumba..yu radhi hata akubembeleze aje akupikie...lakini akishaolewa keshaingia ndani ya nyumba ndo leo anaanza kulalamika kuchoka why shudnt the two of u set namna za kusaidiana ndani ya ndoa?!!?sio kupangiana zamu lakini i think hata mwanaume kukusaidia kata vitunguuu tuu wil giv courage mwanamama ku do more jobs za ndani if the two of them love each other
 
MwanaJF aliyelalama juu ya maisha hayo alidai anasaidia kazi nyingi za ndani, lakini alikuwa haoni kama msaada wake unathaminiwa. Ni kweli kabisa mwanamama huyu 'aliyechoka' angekuwa ana boyfriend basi angepata nguvu za kumfanyia chochote ili amridhishe mpenzi wake, ndiyo maana wengine wanadai there is a magic touch when you have a boyfriend and girlfriend relationship and the magic is lost once you decide to promote your relationship to another level...I dunno why, but it is true!!!!
 
kwani kuna ubaya gani mwanaume akawa ndiye mtandikaji kitanda?

mimi wala sioni haya kujitaja, natandika kitanda, nampangia nguo kabatini mamsap wangu, na chumba nakipanga kama nitakavyo mimi, mwenyewe mamsap anaridhiika!

hamna utamu kama kum-spoil mwanamke wa...!

and especially if she shows you her appreciation.
 
MwanaJF aliyelalama juu ya maisha hayo alidai anasaidia kazi nyingi za ndani, lakini alikuwa haoni kama msaada wake unathaminiwa. Ni kweli kabisa mwanamama huyu 'aliyechoka' angekuwa ana boyfriend basi angepata nguvu za kumfanyia chochote ili amridhishe mpenzi wake, ndiyo maana wengine wanadai there is a magic touch when you have a boyfriend and girlfriend relationship and the magic is lost once you decide to promote your relationship to another level...I dunno why, but it is true!!!!

mhm i have got an idea then i think itakua a better utatuzi wa hili tatizo...tusi upgrade rel zetu from stage ya uchumba tudumu hapo hapo always..as inaonekana watu wakioana tu ndo matatizo huanzaga!!
 
Sometimes sio kwamba ni uvivu bali kuchoka na ratiba za kazi/biashara. Let say mke anafanya kazi pia, na anakuwa na ratiba ngumu ambapo kurudi kwake nyumbani jioni sana labda mbili usiku, sidhani kama atakuwa na nguvu tena za kuingia jikoni na kuanza kuandaa chakula, mbali tu ya kuchoka, muda pia utakuwa umeenda sana na kula chakula usiku zaidi sidhani kama ni vema. Of course, akiwa off days, hayo yote yanawezekana. The point is sio uvivu ama kwamba hatupendi kuwajibika kihivo, ila ratiba za kazi/biashara zinatubana sana na hatupendi kukaa nyumbani (Goal keepers).

Call me Lizy.

Lizy, we women arent their servants they also have to cook and wash as well if i can do it why not him ... its another way of expresing love and care for your spouse kwanini usubiri mpaka I do it ... kama they cant .. sawa bedroom we take care but others house girl can manage ... Hey Girl! you are giving them breathing space here wazidi kutukandamiza
 
interesting stuff!!
tukiacha mambo ya kitandani, je ladies mnapenda mfanyiwe nini na wenzi na mnadhani wao wanapenda muwafanyie nini?
Na gents mnapenda kuwafanyiwa nini na nyie mnadhani wao wanapenda kufanyiwa nini na nyie?
Mimi kwa kuanzia
Napenda nisaidiwe kazi, huwa najisikia raha sana pale baba nanihii anaponisaidia labda kubeba japo glasi yake maji akaipeleka jikoni akaisuuza, au kama napasi akabeba ile nguo ilio tayari akaipeleka mahali pake. yani nampenda mnoo saa hiyo, ni kama vile ananiapproach tena.
Na mimi nadhani anafurahi pale anaponikuta napika (sio kila siku) au nahangaika na nguo zake, kama kushona kifungo nk.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom