House boy na House girl wanatafutwa,wawe tayari kufanyishwa kazi kama watumwa!

funduku

Senior Member
May 2, 2013
131
36
Wakuu kuna raia mmoja wa kigeni anatafuta msichana na mvulana wa kumfanyia kazi zake za nyumbani kwa muda wote atakaokuwa hapa nchini(miezi mitatu) kabla ya kurudi nchini kwake ujerumani, wanahitajika wafanyakazi ambao wavumilivu sana, kwa sababu huyu jamaa ni mkatili sana,ana hasira na wakati mwingine huwa anapiga kwa mjeredi wake maalum, tena anakufanyisha kazi kama mtumwa wake, kuna watu kama wa2 hivi niliwapeleka ndani ya siku tatu wakaacha, kwa hiyo kama unahitaji inabidi ujipange sana na ndio maana nimekuwa mkweli ili ufahamu hali halisi. kuhusu mshahara ni laki moja na nusu kwa mwezi. Kama upo tayari ni pm au acha contact zako hapo chini.
 
ILO wanafahamu hilo?
 
Huyo mjerumani anathubutuje kuhukumu watanzania katika nchi yetu?mimi nipo tayari ni pm mkuu nikamshikishe adabu
 
Misosi ipo lakini? Ukinihakikishia hilo hata kesho naanza mimi ni mvumilivu mno hapa nilipo nipo na mhindi ye mwenyewe kanikubali nina uzoefu wa kulala stoo,kufinya watoto wa boss etc
 
House boy na House girl wanatafutwa,wawe tayari kufanyishwa kazi kama watumwa
Pole mtanzania mwenzetu usiyejua utu wako na kufanya human traffic!
Right ungekuwa na uchungu na mateso waliyopata hao waliofanyiwa utumwa huu awali nadhani unge-report hapa kwa maana ya kukemea utumwa huu!
 
uyo jammaa naona anataka kukumbushia enzi zao walivyotufanya watumwa, mwambie watamuua, sasahivi watanzania ni watu wengine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom