House Boy aliyekomba Mamilioni ya Mbunge yamkuta Mazito

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mahakama ya Mwanzo , Maromboso jijini Arusha imemkuta na kesi ya kujibu mtuhumiwa wa kesi ya wizi wa sh, milioni 7 inayomkabili Kijana wa kazi (house boy) William Mlewa(22) akituhumiwa kumwibia Mwajiri wake, Anjela Charles ambaye ni Mbunge wa zamani wa bunge la Afrika mashariki (EALA).

Hakimu wa mahakama hiyo, Neema Mchomvu alidai kuwa ushahidi wa upande wa mashtaka umekamilika kwa mashahidi sita kuwasilisha ushahidi wao hivyo mahakama imemkuta mshtakiwa na kesi ya kujibu na kumtaka kujipanga kwa ajili ya utetezi.

Hakimu alimsomea mshtakiwa vipengele vitatu vya utetezi na kumtaka kuchagua kimoja wapo kati ya kujitetea binafsi,Kuwa na mashahidi au kukaa kimya jambo ambalo mtuhumiwa alianza kuangua kilio akiomba ahurumiwe yeye bado ni mdogo na baadaye alichagua kukaa kimya na kuiachia mahakama iendelee.

Ndipo hakimu alipodai kuwa hukumu ya kesi hiyo itatolewa Juni 19 mwaka huu na kumtaka mtuhumiwa na Mlalamikaji kufika bila kukosa.

Awali Shahidi wa Tano ,katika kesi hiyo iliyounguruma mwishoni mwa wiki iliyopita,James Joseph ambaye ni mtunza mazingira kwa mlalamikaji,alidai kwamba alimsikia mtuhumiwa akimwambia Mlalamikaji kwamba yeye ndiye alikuwa akichukua fedha hizo chumbani kwa boss wake baada ya kumvizia akiwa jikoni.

Alieleza mahakama hiyo kwamba siku ya tukio akiwa nyumbani kwa Mlalamikaji alikuja William akitokea nje na kuwauliziamama (Mlalamikaji) alipo na baada ya kumfahamisha kwamba yupo stoo ndipo alipomfuata na kumwambia kwamba amsamehe yeye ndiye ameiba fedha hizo.

Alisema kuwa alimwona Mlalamikaji akitokea kwenye chumbani cha stoo akiwa ameongozana na mtuhumiwa huku Mlalamikaji akimtaka Wiliamu kueleza maneno aliyomwambia.

Ndipo nilipomsikia mtuhumiwa akimwomba msamaha Mlalamikaji akidai kwamba yeye ndiye ameiba fedha hizo na ghafla nilimwona mtuhumiwa akiinama na kutumbukiza kichwa kwenye Sufuria la uji wa Moto na kuunga vibaya.

Hata hivyo mzee mmoja wa baraza alimuuliza Shahidi iwapo alishuhudia Mtuhumiwa akiiba fedha hizo,jambo ambapo shahidi alishindwa kuthibitisha.

Naye shahidi wa sita, Amon Ngairo(32)ambaye ni fundi bomba alieleza kuwa alimsikia Mtuhumiwa akimweleza Mlalamikaji kuwa yeye ndiye amekuwa akiiba fedha hizo kwa kumvizia akiwa ametoka chumbani kwake.

Kesi hiyo imeahitishwa hadi juni 19/mwaka huu siku ambayo mahakama hiyo itatoa hukumu.


Ends....
IMG_20200605_145112.jpeg
 
Kama kuna walakini akate rufaa aombe na wanasheria wamsaidie. Hata mimi hili la kusema alijiunguza mwenyewe kidogo linanipa wasiwasi.
Maromboso ni kwikwi miaka yote, unaweza kumkamata mtuhumiwa akapelekwa pale na kusomewa hukumu siko hiyohiyo, nimeshashuhudia mara 2
 
Kijana mwingine anajipotezea/ anapotezewa future yake kwa tamaa au dhuluma...

Ngoja niwe wa mwisho kuamini.
 
Ushaiba pesa kama hizo jap[o si nyingi sana ila kwake angefanya chochote cha maana,alitakiwa awe amefika kijijini kwao siku nyingi sana na kujichimbia kusiko julikana.ona sasa kesi tayari.

Ukiiba hela usiangalie nyuma,subiri utafutwe siyo kujisalimisha kama umeua kumbne hata hujajeruhi,huyu hata ufisadi hauwezi.
 
Mama mbunge hebu kamata msaafu useme maneno haya...

"Nasema kweli mbele za Mungu ya kuwa sikummwagia uji usoni kijana huyu ila alitumbukiza kichwa mwenyewe kwenye sufuria la uji, eeh mwenyezi Mungu nisikie"

Vinginevyo tuache udanganyifu wa kusema uongo kisa kijana hana uwezo wa kuweka mwanasheria.
 
"ghafla nilimwona mtuhumiwa akiinama na kutumbukiza kichwa kwenye Sufuria la uji wa Moto na kuunga vibaya."

🤗🤗🤗🤗🤗🤗
 
Mbona hata huo ushaidi wenyewe umekaa kimagumashi "eti nilimsikia mtuhumiwa akimwambia mlalamikaji yeye ndio alkua akichukua pesa chumbani kwa boss" mara paaaap mtuhumiwa kazamisha kichwa kwenye sufuria ya uji

Kweli pesa ndio inaamua kesi na mkono mtupu haulambwi.
 
Back
Top Bottom