only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,525
Moja ya maneno yenye hekima yanayopatikana kwenye hotuba za mwalimu Nyerere............
"Safari moja Mgiriki mmoja alipitapita humu humu anajitapatapa anasema Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni mwangu, nikasema Mshenzi sana huyu, Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni ana mfuko mpana kiasi gani, nikajua anahonga watu, hawezi kusema hivyo bila kama hahongi watu, lakini vigumu sana kumpata, nikaona lakini hata hivyo nitamfundisha tu, nikamtia ndani. Nikatiwa misukosuko, nikatiwa zogozogo hapa Mwl muachieee nikawaambia Simuachi hana Adabu huyu.
Kuna kiongozi gani anayeweza kusema maneno kama haya leo? Tutaendelea kusikia hotuba kama za jana za Jakaya Kikwete...upupu mtupu...