Hotuba zenye maneno kama haya hazitapatikana tena kwenye tanzania hii.....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Nyerere.jpg

Moja ya maneno yenye hekima yanayopatikana kwenye hotuba za mwalimu Nyerere............

"Safari moja Mgiriki mmoja alipitapita humu humu anajitapatapa anasema Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni mwangu, nikasema Mshenzi sana huyu, Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni ana mfuko mpana kiasi gani, nikajua anahonga watu, hawezi kusema hivyo bila kama hahongi watu, lakini vigumu sana kumpata, nikaona lakini hata hivyo nitamfundisha tu, nikamtia ndani. Nikatiwa misukosuko, nikatiwa zogozogo hapa Mwl muachieee nikawaambia Simuachi hana Adabu huyu.

Kuna kiongozi gani anayeweza kusema maneno kama haya leo? Tutaendelea kusikia hotuba kama za jana za Jakaya Kikwete...upupu mtupu...

oldonyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
549
86
sasa wana lugha zao za kifisadi fisadi.mfano jk anakamsemo ambako katakumbukwa sana(we unataka kula tu afu utaki uliwe unatakia kuliwa kwanza afu ndo ule)huyo jei cent.
 
Madcheda

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
422
68
Hahaha yan pata picha hapo rostam anasema ivyo halaf eti kikwete ndo anasema anamtia ndani,hahahaha nazan ndo itakua mwisho wa dunia huo
 
ebrah

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
397
50
kama j50 anashindwa hata kuwaambi waache wizi anashindwa ataweza kuwa na uwezo wa kuwa na misemo kama hiyo!
 
Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
217
65
View attachment 38158

Moja ya maneno yenye hekima yanayopatikana kwenye hotuba za mwalimu Nyerere............

"Safari moja Mgiriki mmoja alipitapita humu humu anajitapatapa anasema Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni mwangu, nikasema Mshenzi sana huyu, Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni ana mfuko mpana kiasi gani, nikajua anahonga watu, hawezi kusema hivyo bila kama hahongi watu, lakini vigumu sana kumpata, nikaona lakini hata hivyo nitamfundisha tu, nikamtia ndani. Nikatiwa misukosuko, nikatiwa zogozogo hapa Mwl muachieee nikawaambia Simuachi hana Adabu huyu.

Kuna kiongozi gani anayeweza kusema maneno kama haya leo? Tutaendelea kusikia hotuba kama za jana za Jakaya Kikwete...upupu mtupu...

Ndugu yangu zama hizi za wanaharakati na haki za binadamu hata Nyerere hawezi fanya hivyo alivyo fanya pengine angefanya kwa njia nyingine sio huu udikiteta.
 
mwacheni77

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
763
209
Ndugu yangu zama hizi za wanaharakati na haki za binadamu hata Nyerere hawezi fanya hivyo alivyo fanya pengine angefanya kwa njia nyingine sio huu udikiteta.
Nakuunga mkono mkuu,wangesema rais katukana aombe radhi,hiki ni kipindi cha utandawazi unatakiwa uwe makini sana na unachozungumza na kufanya,mfano hii leo mtandio wa mkuu wa wilaya umekuwa issue na mtaji wa kisiasa igunga,kipindi kile kulikuwa hamna nafasi ya kuhoji hotuba ya rais na ilikuwa zidumu fikra za mwenyekiti tu,not this time cha jf
 
Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
217
65
Nakuunga mkono mkuu,wangesema rais katukana aombe radhi,hiki ni kipindi cha utandawazi unatakiwa uwe makini sana na unachozungumza na kufanya,mfano hii leo mtandio wa mkuu wa wilaya umekuwa issue na mtaji wa kisiasa igunga,kipindi kile kulikuwa hamna nafasi ya kuhoji hotuba ya rais na ilikuwa zidumu fikra za mwenyekiti tu,not this time cha jf

Umesema vizuri kiongozi. Kosa kubwa tunalolifanya sisi waTz ni kumchukulia Nyerere kama mtu asiye kuwa na makosa wala mapungufu. Tunge kuwa tunaangalia mapungufu yake pengine tungekuwa tumejifunza mambo mengi sana na tuenge epuka kurudia makosa yale yale. Lazima tukubali kwamba Nyerere kama mwanadamu alikuwa na mambo mengi mazuri lakini alikuwa na mapungufu mengi tu. viongozi wetu wa leo bado wanayatumia mapungufu yake kwa vile hatuja amua kuyaweka wazi kuwa haya yalikuwa ni mapungufu. Moja ni hili la kumuweka mtu kizuiizini bila ya kumfungulia mashitaka ya kutoa rushwa. Ukitumia akili kidogo tu utajiuliza kwa enzi ya zama za Nyerere alishindwa vipi kumtia hatiani kwa tuhuma za rushwa. Tubadilikene jamani vinginevyo nchi hii haitatoka hapa ilipo.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,771
74,420
View attachment 38158

Moja ya maneno yenye hekima yanayopatikana kwenye hotuba za mwalimu Nyerere............

"Safari moja Mgiriki mmoja alipitapita humu humu anajitapatapa anasema Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni mwangu, nikasema Mshenzi sana huyu, Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni ana mfuko mpana kiasi gani, nikajua anahonga watu, hawezi kusema hivyo bila kama hahongi watu, lakini vigumu sana kumpata, nikaona lakini hata hivyo nitamfundisha tu, nikamtia ndani. Nikatiwa misukosuko, nikatiwa zogozogo hapa Mwl muachieee nikawaambia Simuachi hana Adabu huyu.

Kuna kiongozi gani anayeweza kusema maneno kama haya leo? Tutaendelea kusikia hotuba kama za jana za Jakaya Kikwete...upupu mtupu...

Hayo maneno tu hayana utendaji wala hayana maana sana wla hayajatuletea jema lolote Tanganyika zaidi ya kututumbukiza kwenye lindi la umaskini.

Nyerere alikuwa ni mpiga porojo mzuri lakini utendaji na uongozi wa kuiendeleza nchi ulikuwa patupu. Ndio maana mpaka leo tunalalamika kuwa eti ni maskini, ukweli ni kwamba Mungu katupa kila utajiri Tanzania lakini katunyima akili, moja wapo ni hili la kushabikia mtu aliyetuweka kizani mpaka leo. Huu ni umaskini wa akili.

Nawaonea huruma sana, mnaomshabikia Nyerere, kwa lipi zaidi? lakini hakuna cha kuwaeleza kwani hamtouona ukweli kwa kuwa akili zenu zimefikia kikomo cha kuona, hizo ndio Fikra Pevu.
 
Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
348
191
Teh teh teh teh teh eeeeeeee..... Hapo kwa Jcent ndo pamenikuna sana
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Hayo maneno tu hayana utendaji wala hayana maana sana wla hayajatuletea jema lolote Tanganyika zaidi ya kututumbukiza kwenye lindi la umaskini.

Nyerere alikuwa ni mpiga porojo mzuri lakini utendaji na uongozi wa kuiendeleza nchi ulikuwa patupu. Ndio maana mpaka leo tunalalamika kuwa eti ni maskini, ukweli ni kwamba Mungu katupa kila utajiri Tanzania lakini katunyima akili, moja wapo ni hili la kushabikia mtu aliyetuweka kizani mpaka leo. Huu ni umaskini wa akili.

Nawaonea huruma sana, mnaomshabikia Nyerere, kwa lipi zaidi? lakini hakuna cha kuwaeleza kwani hamtouona ukweli kwa kuwa akili zenu zimefikia kikomo cha kuona, hizo ndio Fikra Pevu.

Foxy hapa mtazamo sio NYERERE na kuwa yuko hai au hayuko hai na kama tutamuona tena au la...Mtazamo ni uwezo wa kiongozi katika ngazi ya nchi kuweza kuwa na mamlaka ya kusimamia uhuru (sovereignity) wa nchi yake bila kutetereka.

Ni kweli kuna swala la utandawazi na uhuru utokanao na haki za kibinadamu lakini bado haunyang'anyi mamlaka ya dola huru katika kusimamia mambo yake ya msingi hasa inapoonekana kuna kuna kudhalilishwa kisa tu "nchi masikini"......

Nilimkumbuka sana kiongozi mwenye msimamo kama huu wakati yule mshenzi mwingine alipomtemea mate askari wetu wa barabara halafu akaonekana shujaa na tukafyata mkia kama vijibwa koko na kumuachia kwa kisingizio cha immunity wakati wanzetu wanaojua nini maana ya sovereignity yao (wakti nyie mnang'ang'ani hofu ya haki za binadamu) Wamarekani walimtia ndani balozi wa Ukraine aliegonga mwananchi na kumuua kwa kuwa aliendesha gari amelewa na kuwataka Ukraine kutoa hiyo immunity kabla hawajazuia misaada kwa serikali.....

Hii ndiyo inayotufanya tuendelea kuwa "minyani" na kuendelea kukumbatia upuuzi kwa hofu ya kukosa "vithuti"
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,169
10,331
View attachment 38158

Moja ya maneno yenye hekima yanayopatikana kwenye hotuba za mwalimu Nyerere............

"Safari moja Mgiriki mmoja alipitapita humu humu anajitapatapa anasema Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni mwangu, nikasema Mshenzi sana huyu, Serikali yote ya Tanzania ipo mfukoni ana mfuko mpana kiasi gani, nikajua anahonga watu, hawezi kusema hivyo bila kama hahongi watu, lakini vigumu sana kumpata, nikaona lakini hata hivyo nitamfundisha tu, nikamtia ndani. Nikatiwa misukosuko, nikatiwa zogozogo hapa Mwl muachieee nikawaambia Simuachi hana Adabu huyu.

Kuna kiongozi gani anayeweza kusema maneno kama haya leo? Tutaendelea kusikia hotuba kama za jana za Jakaya Kikwete...upupu mtupu...

Hayo maneno tu hayana utendaji wala hayana maana sana wla hayajatuletea jema lolote Tanganyika zaidi ya kututumbukiza kwenye lindi la umaskini.

Nyerere alikuwa ni mpiga porojo mzuri lakini utendaji na uongozi wa kuiendeleza nchi ulikuwa patupu. Ndio maana mpaka leo tunalalamika kuwa eti ni maskini, ukweli ni kwamba Mungu katupa kila utajiri Tanzania lakini katunyima akili, moja wapo ni hili la kushabikia mtu aliyetuweka kizani mpaka leo. Huu ni umaskini wa akili.

Nawaonea huruma sana, mnaomshabikia Nyerere, kwa lipi zaidi? lakini hakuna cha kuwaeleza kwani hamtouona ukweli kwa kuwa akili zenu zimefikia kikomo cha kuona, hizo ndio Fikra Pevu.

Angalau mpiga porojo anaweza kumtia jambajamba fisadi/mwizi kama lile giriki na kuonyesha his authority kama rais..kuliko mpiga porojo wa sasa ambae hata kutia jambajamba hawezi..yeye anajua kuchekacheka tu....
 
only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Hayo maneno tu hayana utendaji wala hayana maana sana wla hayajatuletea jema lolote Tanganyika zaidi ya kututumbukiza kwenye lindi la umaskini.

Nyerere alikuwa ni mpiga porojo mzuri lakini utendaji na uongozi wa kuiendeleza nchi ulikuwa patupu. Ndio maana mpaka leo tunalalamika kuwa eti ni maskini, ukweli ni kwamba Mungu katupa kila utajiri Tanzania lakini katunyima akili, moja wapo ni hili la kushabikia mtu aliyetuweka kizani mpaka leo. Huu ni umaskini wa akili.

Nawaonea huruma sana, mnaomshabikia Nyerere, kwa lipi zaidi? lakini hakuna cha kuwaeleza kwani hamtouona ukweli kwa kuwa akili zenu zimefikia kikomo cha kuona, hizo ndio Fikra Pevu.

Acha upunguani wewe..kwahiyo mtendaji ni Kikwete? Hivi katika maraisi wapiga porojo walipata kutokea Tanzania zaidi ya Kikwete ni nani? Acha kuleta ushabiki wa kijinga hapa....Tatizo wa watanzania CCM imewafanya mmekuwa wavivu hata kufikiri na kuchambua mambo,kazi yenu ni kulamba miguu ya wakubwa tu...Unasema Nyerere hakuwa mtendanji sawa nakubali,nitajie raisi mtendaji aliyewai kutokea hapa Tanzania..Yaani mawazo yako yanafanana na jina lako "FOXY".......................
 
only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Umesema vizuri kiongozi. Kosa kubwa tunalolifanya sisi waTz ni kumchukulia Nyerere kama mtu asiye kuwa na makosa wala mapungufu. Tunge kuwa tunaangalia mapungufu yake pengine tungekuwa tumejifunza mambo mengi sana na tuenge epuka kurudia makosa yale yale. Lazima tukubali kwamba Nyerere kama mwanadamu alikuwa na mambo mengi mazuri lakini alikuwa na mapungufu mengi tu. viongozi wetu wa leo bado wanayatumia mapungufu yake kwa vile hatuja amua kuyaweka wazi kuwa haya yalikuwa ni mapungufu. Moja ni hili la kumuweka mtu kizuiizini bila ya kumfungulia mashitaka ya kutoa rushwa. Ukitumia akili kidogo tu utajiuliza kwa enzi ya zama za Nyerere alishindwa vipi kumtia hatiani kwa tuhuma za rushwa. Tubadilikene jamani vinginevyo nchi hii haitatoka hapa ilipo.

Hatumaanishi Mwl Nyerere alikuwa hana matatizo,lakini katika matatizo yake alikuwa na mazuri mengi kuliko mabaya...kinyume na hawa jamaa zetu wa sasa...uchovu asilimia 99.9 mazuri 0.1...Huu ni upuuzi!!
 
Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,617
Nyerere ni rais pekeee aliyejenga viwamda vingi zaidi ya wote kumbukeni alichukua nchi ikiwa na wasomi 13 tuu wenye degree.
 
Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
217
65

Hatumaanishi Mwl Nyerere alikuwa hana matatizo,lakini katika matatizo yake alikuwa na mazuri mengi kuliko mabaya...kinyume na hawa jamaa zetu wa sasa...uchovu asilimia 99.9 mazuri 0.1...Huu ni upuuzi!!

Kutuingiza kwenye muungano ambao uliridhiwa na watu wawili na maridhiano yenywe yakiwa yanahang.
 
takeurabu

JF-Expert Member
Jul 23, 2011
255
38
Hayo maneno tu hayana utendaji wala hayana maana sana wla hayajatuletea jema lolote Tanganyika zaidi ya kututumbukiza kwenye lindi la umaskini.

Nyerere alikuwa ni mpiga porojo mzuri lakini utendaji na uongozi wa kuiendeleza nchi ulikuwa patupu. Ndio maana mpaka leo tunalalamika kuwa eti ni maskini, ukweli ni kwamba Mungu katupa kila utajiri Tanzania lakini katunyima akili, moja wapo ni hili la kushabikia mtu aliyetuweka kizani mpaka leo. Huu ni umaskini wa akili.

Nawaonea huruma sana, mnaomshabikia Nyerere, kwa lipi zaidi? lakini hakuna cha kuwaeleza kwani hamtouona ukweli kwa kuwa akili zenu zimefikia kikomo cha kuona, hizo ndio Fikra Pevu.
tafadhali mama msalie mtume, tz mimi sijawahi kuona kiongozi mzuri aliyewahi kutokea kama hayati nyerere(RIP)!! KUMBUKA MISINGI YAKE NDIYO INAKUFANYA HATA WEWE FF SASA HIVI UWE UNAVAA HIJABU! OTHERWISE PASINGE KALIKA HAPA BONGO!!!
 
Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
217
65
Nyerere ni rais pekeee aliyejenga viwamda vingi zaidi ya wote kumbukeni alichukua nchi ikiwa na wasomi 13 tuu wenye degree.

Huo ni ukweli usio pingika ingwa viwanda vingine vilijengwa kwa kuangalia political motives na sio economical motives.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom