Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Hotuba za wafanyakazi zimejaa malalamiko na makasiriko dhidi ya serikali, zimejaa uzuni na maumivu. Wanasoma hotuba Kama hizi kwa mara ya Kwanza toka mwaka 2016 ndoto zakuandika uhalisia wa Watumishi zilipozimwa rasmi.
Kwa namna zilivyoandaliwa ni Kama wanamategemeo makubwa na Rais mpya bila kujua malalamiko yao yanahitaji zaidi fedha kuliko kitu kingine.
Kwa Hali ilivyo na namna alivyoeleza Mhe. Rais ni wazi kimeumana. Walijiwekea matumaini makubwa ila ukweli ni kwamba uwezo ni mdogo ukizingatia idadi ya wafanyakazi na idadi ya Watanzania wenye mahitaji mbalimbali..
Niwashauri tu kwa wakati mwingine hotuba Kama hizi wawe wanazisoma mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi, kipindi hicho wanasiasa huwa wepesi kutoa ahadi nakuzitekeleza ila kwa Sasa 2021 kinachofanyika nikuruhusu malipo ya madeni yao, ongezeko la kisheria (annual increment) na malipo ya posho chache zilizokatazwa na awamu iliyopita.
Shime wafanyakazi, msilaumu kwa kiu yenu kutokatika. Hali ya uchumi ni mbaya na Mhe. Rais amesema kweli tupu kulingana na uwezo wa serikali yake kulipwa.
Cha mwisho, wakati ninyi wachini mliolalamika na kubeba mabango mkiongezewa 20,000 to 30,000 mabosi wenu watalipwa ngongeza zaidi ya laki mbili kwa sababu ya ukubwa wa mishahara. Ninyi mmepambana wao wakajificha lakini manufaa yake ni makubwa kwa waliojificha kuliko walioandamana na mabango juu