Hotuba za Rais zimejaa Hofu na hazina Matumaini

Hafai kwa sab ni mmoja kati ya mafisadi papa wa ccm kwahiyo hakuna tofauti na ccm iliyopo madarakani. Tunataka mtu ambaye hana harufu ya ccm.
Waweza uza nyumba ya mzazi wako bila ya yeye kujua? Fatilia majbu ya lowasa katba htuba yake kwenye campaign ndo upate majbu
 
Hotuba za JPM hazina matumaini kwa mwananchi wa kawaida.
Sioni rais akiongelea kitu ambacho hajawahi kukiongelea, ndege ameshaongea.
Kuna mambo Muhimu ambayo wananchi wana hamu ya kuyasikia ila wakimuangalia rais kiukweli huyu hana msaada kwa maisha ya sasa ya watanzania.
Ajira zilizositishwa. Hapa rais anachukulia mzaha ila kuna kundi kubwa sana linaumia.
Uhuru wa vyombo vya habari, tulitegemea rais agusie kidogo kwenye hotuba zake ila hana time .

Maisha kuwa magumu.
Hapa ndio tatizo liko hapa, huyu JPM ni kama yupo Kenya, anayoyaongea na anachokiamini na uhalisia ni kama mbingu na bahari.
Ninachokiona kundi kubwa la watanzania hawana matumaini kabisa.
Kilichobaki tu wanaomba sasa hivi siku zikimbie ifike mwaka 2020.

Ni mtizamo wangu naweza kupingwa.
Ameniacha hoi alipisema ndege Ni miongoni mwa vipaumbele vya taifa! Kweli watu wanahitaji ndege kuliko maji, madawa, elimu nk. Nakulilia tz, nini kimekusibu viatu vya mwalimu ukamvalisha jpm?
 
Mkuu wa nchi anasema ukweli toka moyoni. Hapendi siasa za unafiki.
Huyu mkuu wako wa nchi kama ni msemakweli na hapendi siasa za Unafiki mbona hakutuambia mapema kabisa kua Tuchange pesa za maafa lakini zitafanya kazi ya kujenga miundombinu? mbona kanyamaza na Baada ya pesa kujaa mfuko wa Maafa ndio anakuja na Lafudhi ya kisukuma eti Serekali haiwezi kujengea waanga kweli inakuingia akilini?Magufuli mnafiki sijawahi kuona mnafiki kama huyu Baba.
 
Kwa kweli Lugha ya matumaini inahitajika!. Pamoja ya kwamba tunaisoma namba lakini Lugha za kufoka na vitisho zingepunguzwa kupunguza Msongo wa mawazo usio wa LAZIMA
Asa mbona amewaambia wale matajiri aliowambia ni mashetani walioahidi misaada kwa waathirika lazima watoe ahadi zao na kamwambia mkuu wa mkoa awafatilie ipatikane bil 4 ndo atengeneze miondo mbinu ya serekale.
Nashangaa hivi hii misaada imekuwa ni ya lazima?
 
Hakuna kitu,Hiyo sheria anataka afatage yeye tu, watendaji wengine kama Wakurugenzi n.k.z wanapotekeleza majukumu yao kwa mjibu wa sheria zilizopo katika ofisi zao Anawatumbua. A government full of contradictions.!!!
 
Ni kama anakopi na kupesti. Hotuba zake,popote anapozitoa,hujaa mikwara;ahadi za kutowaangusha wasikilizaji wake; kuonesha maguvu yake ya Urais na kadhalika.

Hotuba zake hazina jipya. Yanayozungumzwa ni yaleyale;anayezungumza ni yuleyule na hata wasikilizaji ni walewale. Hotuba zake hazina uchambuzi wa kisera kuhusu Ilani au ahadi zake. Hotuba hupaswa kubeba mwelekeo wa Serikali

LA NYONGEZA: Kwa maandalizi yaliyofanyika Kagera kuhusu ziara ya Rais,kwanini Rais hakujimwaga Uwanja wa Kaitaba badala ya kujibana kwenye kakiwanja ka Shule ya Sekondari Ihungo?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hivi wale matajiri walioahidi kusaidia waathirika SIZONJE kasema lazima wafatiliwe ahadi zao wazitoe.. je kwani ni lazima kutoa ulichoahidi?
 
Back
Top Bottom