Hotuba za Rais Magufuli za kichwani zinakera, asome hotuba anayoandaliwa

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,460
2,000
Leo nmemsikia anavyoongea, aibu naona mimi!!
hivi tangu mwanzoni tulikuwa hatumuelewi rais wetu alivyokuwa anasema "Tanzania ninayoitaka Mimi","hii ndiyo Tanzania ninayoitaka"hapa haijalishi km watanzania wanaitaka au la maadam bwana mkubwa anaitaka yeye then na iwe hvy.
 

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,460
2,000
tatizo la rais wetu mpendwa na mwema sana,anaongoza kwa kutumia hisia sana,kwa kiongozi mkubwa km yeye anatakiwa kutambua yapo maeneo ya kutumia hisia na yapo maeneo ya kutumia akili,once unapojichanganya ktk moja ya maeneo hayo athari yake inakuwa mkubwa mno.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,602
2,000
Kuna vipindi wanafiki wa kitanzania walikuwa wakimlaumu Rais Kikwete kuwa anadanganywa na watu wake anasoma tu alichoandikiwa bila kujua ukweli wa jambo analolizungumzia kwahiyo anapotoshwa na yeye anapotosha, kama kawaida yetu kutoka Rais dhaifu anayechekacheka hovyo, hayupo serious kabisa, tunataka Rais mwenye sauti na dikteta na anayechukua hatua on spot!
Mwambieni Rais kuwaongoza watanzania kunahitaji moyo wa subra, sisi raia tuna akili nyingi hata za kukwamisha maendeleo, asishangae kuwaona watanzania wakifurahia matatizo na kuchukia maendeleo, na kwa miaka yake mitano muambieni avumilie kwani anaongoza watu tofauti na dunia nyingine.
Kuna eneo wananchi walirudisha madawati baada ya kugundua aliyetoa msaada huo ni diwani wa ccm.

Siyo ajabu hata wakiipa kisogo amani kwa kuwa wakikaa kimya ni sawa na kujaribu kusema ili utumbuliwe nyama maana wewe huna jipu na wala wewe sii jipu.
 

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
12,021
2,000
Watanzania kweli haitapita miaka mitatu lazima tutajuta! Raisi kote duniani ni Alama na Nembo ya Taifa husika kwa kuwaunganisha wananchi! Ila Hapa kwetu naona mkulu amekuwa nembo ya tungo tata na kutugawa kwa misingi ya sisi tuna madaraka wao hawana!
Nakuna majitu mapumbavu yanarukaruka humu kwa shangwe
 

machoalbi

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
339
250
Kuna watu wanadhani wengine wana chuki na Rais hakuna mwenye chuki nae,yeye ndio anajichanganya mno,kama kweli yeye ni mtendaji mzuri basi bora angeendelea kufanya kazi tu bila kuongea afanye vitendo tu,hapo wengi tungemuelewa lakini sasa haeleweki anataka kufanya kitu gani,kila siku kauli zake zinaleta utata tu

Kumbe hafanyi vitendo?
 

HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,183
2,000
Kuna eneo wananchi walirudisha madawati baada ya kugundua aliyetoa msaada huo ni diwani wa ccm.

Siyo ajabu hata wakiipa kisogo amani kwa kuwa wakikaa kimya ni sawa na kujaribu kusema ili utumbuliwe nyama maana wewe huna jipu na wala wewe sii jipu.
Huenda huyo aliyepeleka alianza kuleta siasa za vyama kwenye jambo lisilohitaji siasa, hivi kama madawati ni shule na mmiliki ni serikali wananchi wanapata wapi ujasiri kugomea serikali kuleta madawati kama huyo diwani hakuleta siasa na jutaka kusifiwa labda kwa ajili ya chama chake?
Tuna tatizo kubwa la kutojua nini tunataka na wakati gani
 

machoalbi

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
339
250
Nafasi ya urais ni Tasisi sio one man show.ukisikiliza hotuba za JPM hazionyeshi kama anasoma alichokiandaa/kuandaliwa.anatililika alivyovikusanya na kuviweka moyoni.kila kukicha anaacha maswali kuliko majibu kutokana na speech zake!
Sijawahi ona Rais wa hivi hapa nchini.labda nchi zingine.Rais anakazi za kuli shape taifa kwa kauli zake.sasa anapotawaliwa na mihemuko na kutoa point kichwani nahisi tutaingia Chaka/potezwa huko mbele.hatujui kipi tukiweke kwenye library kama kumbukumbu yenye mashiko.Time will tell.

Hizo hotuba laini ndio zilizolifikisha taifa hapa lilipo,
Kuna changamoto nyingi sana za kutatua katika taifa hili maskini, sidhani Kama "hotuba" Ni mojawapo
Hotuba ya rais inaweka chakula mezani pako?
 

HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,183
2,000
Mabadiliko.............mabadiliko...............zungusha mikono........tena......
Hotuba hii nani kamuandalia huyu kiongozi wetu
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,602
2,000
Huenda huyo aliyepeleka alianza kuleta siasa za vyama kwenye jambo lisilohitaji siasa, hivi kama madawati ni shule na mmiliki ni serikali wananchi wanapata wapi ujasiri kugomea serikali kuleta madawati kama huyo diwani hakuleta siasa na jutaka kusifiwa labda kwa ajili ya chama chake?
Tuna tatizo kubwa la kutojua nini tunataka na wakati gani
Serikali ndio hao watu.
Wala rais sio serikali kama magufuli anavyosema "serikali yangu"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom