Hotuba za Rais Magufuli za kichwani zinakera, asome hotuba anayoandaliwa

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
18,394
16,387
Speech za Rais Magufuli zinashida kidogo, Rais akizungumza anazungumza kama mtu aliyejaa visasi na sifa nyingi, hana utaratibu mzuri katika kupangilia kile anachokisema.

Kama Rais anapaswa kuzungumza kwa utaratibu na mpangilio hata kama ni sehemu anasisitiza jambo, vijembe kwa walio chini yake ni kutafuta tu kick kwa wananchi ambao mwenyewe keshatujua na amejawa na sifa tunazompa kila siku.

Rais ni reflection ya watu alionao.


Kumekuwa na kauli za kukinzana za Mh. Magufuli pale anapokuwa anahutubia wananchi kwa hotuba za Kichwani.

Mfano: Nimejitoa Mhanga kutumbua majipu. Hatachomoka mtu.

Baadae, Nitawalinda wastaafu wote, waishi kwa amani.

Nataka watanzania wawe na maisha bora.
Baadae, Nitawashusha wanaoishi kama Malaika waishi kama shetani.

Ni marufuku kuagiza Sukari toka nje.
Baadae, Serikali imeagiza sukari ili kufidia upungufu wa Sukari nchini.

Hii ni mifano ya kauli tata, alizowahi kutamka Mh. Magufuli anapotoa Hotuba toka Kichwani.

Ushauri: Mh. Magufuli, achana na hotuba za kutoa Kichwani, anza kusoma hotuba. Usipofanya hivyo utaendelea kujichanganya na kuwachanganya wananchi.
 
Hiyo mipangilio ndio imetufikisha hapa, nyingi zenye mipangilio huwa hazijajaa uhalisia.

Anachotaka watu wake wajue ni kuwa chini ya magufuli wanaoption mbili. Kuwa msafi au kuondoka.

Nakumbuka hotuba za ben za mwisho wa mwezi hata ukiulizwa alikuwa anaongelea nini watu wengi walisha sahau wanakumbuka misamiati maalufu kama MICHAKATO na TIJA
 
Kwani sifa tunazo mpa sio za kweli?

Hizo speech zake za muda mfupi tu watumishi wamebadilika kupita maelezo wengi wao wameanza kujua wajibu wao nidhamu kazini na uwajibikaji umeanza kurudi.

Hizo speech unazo zitaka ww na ulizo zizoeya ndio zilizo haribu watz.

Watz wa leo hawataki speech laini laini na ukumbuke tumechelewa sana tuko nyuma ukilinganisha na dunia ilipo.

Leo unatoka boko unaenda mjini unatumia dakika 120 wakati tungekuwa tunaenda kama dunia inavyo kwenda tulitakiwa tutumie dakika zisizo zidi 30 tu.

Leo darasa moja lina watoto zaidi ya 50 na tulitakiwa darasa 1 lisizidi watoto 30 mpaka 35.
Leo dr mmoja anatibia wagonjwa zaidi ya 100 kwa masaa 8.

Acha MH RAIS ashughulike apunguze uvivu tulio kiwa nao tuache tabia ya kuishi kwa mazoeya na ujanja ujanja.

Tunapaswa kufanya kazi na tuishi kwa mujibu wa jasho letu.

Muda wa kucheka cheka umekwisha muunge mkono MH RAIS.
 
Sasa huoni kuwa jamaa wa NIDA keshahukumiwa na akipelekwa mahakamani jaji lake ni moja tu, kumfunga?

Kimsingi Magu asiwe anatoa hukumu kwani anawanyima wanasheria uwezo wa kufanyakazi kwa kuwaingilia.

Hebu awaachie wenye kazi yao kwani watatoa hukumu za kumpendeza yeye na hii ni kinyume cha haki.
 
Watanzania wenzangu mnatia hasira na mnakera mpaka basi.

Zile hotuba za Kikwete za masaa manne tumezichoka, mpaka anamaliza ni kucheka huondoki na chochote. Anatoa hutoba tangu anaingizwa theater mpaka anatiwa ganzi huu ni usanii. Hajawahi kuzungumzia maslahi ya Taifa kama huyu sasa hivi.

Muacheni rais anaejielewa na kuitumia nafasi yake kwa ufasaha kabisa. Ile nafasi haitakiwi kupembejeana mwisho wa siku tutarudi hapa kumlaumu hajafanya kitu.

Amri zitumike na mikwara zaidi ya pale. Namkumbuka Karume miaka ya 67 alipokuwa Rais, Leo tunafaidi matunda yake huku Zanzibar mpk Leo na hakuna kiongozi aliewahi kufikia aliyoyafanya. Alisaidiwa sana na kuwa ujasiri, alikuwa anawahi kufika sehemu za kujenga Yale majumba kuliko mafundi, amefanya mambo makubwa alikua na nia nzuri sana ya Maendeleo Leo namfananisha na Magufuli.
 
Sasa huoni kuwa jamaa wa NIDA keshahukumiwa na akipelekwa mahakamani jaji lake ni moja tu, kumfunga? Kimsingi magu asiwe anatoa hukumu kwani anawanyima wanasheria uwezo wa kufanyakazi kwa kuwaingilia. Hebu awaachie wenye kazi yao kwani watatoa hukumu za kumpendeza yeye na hii ni kinyume cha haki.
Yeye ndo mkuu hakuna, jaji kamteua yeye lazima jaji alipe ili aendelee kuwa pilato,
 
Back
Top Bottom