Hotuba za Rais kuongea na wananchi kila baada ya kipindi fulani zimeisha wapi?

Xolani

Member
Oct 26, 2017
84
122
HOTUBA ZA MARAIS KUONGEA NA WANANCHI KILA BAADA YA KIPINDI FULANI ZIMEISHA WAPI?

Wadau na wazalendo wa nchi hii ya Tanzania mimi kama mmoja wa wapenda maendeleo katika taifa letu la Tanzania naomba kufahamu ama kufahamishwa, ule utaratibu wa Marais waliotangulia kwa vipindi tofauti kuongea na wananchi kupitia luninga na radio kila baada ya miezi au mwezi zimeisha wapi?

Kwangu mimi nilikuwa naona ni jambo la busara na hekima kama kiongozi mkuu wa nchi kuongelea matatizo ama maendeleo ya wananchi kupitia njia tajwa hapo kuufamisha umma nchi ilipofikia na inapoelekea na juu ya maendeleo yao pamoja na ahadi zilizotolewa kupitia ilani ya chama husika.

Wazo langu ningemuomba Mh John pombe magufuli arudishe utaratibu wa kuongea na wananchi kola mwezi kuwapa hamasa na kuwaondolea uchovu wa kuichoka nchi Yao maana hakuna siku ambayo Mh Rais amegongwa na wananchi wake kupitia njia hizo zaidi ya kuongea kwenye mikutano.

Mh rais nakuomba urudishe utamuduni wa kuongea na sisi kupitia LUNINGA na RADIO
 
Vijembe haviwezi kuwa hotuba. Bora kuacha asiwaudhi watu.
2018 ni mwaka wa furaha. Sisikilizi wala sitazami chochote toka kwa mtu aliyejaa kiburi na majivuno.
 
Aaah , kama ni huyu tu afadhali aache kabisa.Hana weledi wa hotuba . Ni afadhali nimsikilize Zembwela kuliko kutafuta stress za 2018.
 
Bombadia zilizompeleka Lissu mwenye bonde la mauti zimeshatua town kama tuluvo ahidiwa bai dec?
 
Mbona Magufuli anaongea na wananchi mara kwa mara akiwa kwenye ufunguzi wa visima vya maji , ofisi za mabenki au akiwa anapokea ripot za kamati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom