kinyoba
JF-Expert Member
- Jun 2, 2011
- 1,267
- 718
Wadau mi huwa nazisikia hotuba za Nyerere mara kwa mara kwenye TV. Kinachonishangaza ni inakuwaje mtu amefariki miaka 12 iliyopita lakini hotuba zake ni kama amezitoa mwaka huu tena hata unaweza kusema ni mwezi huu? Hasa ukizingatia hali ya siasa nchini hivi sasa! Wakati mwingine unaweza kudhania anamsema mtu fulani au kikundi cha watu fulani.