Hotuba za Mwalimu Nyerere ziwe zinatangazwa wakati wote, siyo wakati wa kumbukumbu ya kifo chake pekee

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,685
2,000
Imezoeleka kusikia hotuba za baba wa Taifa wakati wa kumbukumbu ya kifo chake, tarehe 14/10 ya kila mwaka na wala siyo vinginevyo.

Kwa kweli unaposikia hotuba za Mwalimu, huwa hazichuji kabisa na wakati wote utapenda kuzisikiliza, kwa manufaa ya nchi yetu ya kipindi hiki na kijacho.

Hotuba za Mwalimu Nyerere zimekuwa tofauti Sana na hawa wazee wengine wastaafu, ambapo hawa wazee wengine wamekuwa wakiweka mbele ukereketwa wao kwa chama tawala na kuwa "mabubu" bila kukemea matendo maovu yanayoendelea nchini, wakati Mwalimu Nyerere amekuwa akiweka mbele maslahi ya Taifa hili, kuliko kitu chochote kile na amekuwa akikenea waziwazi maovu yoyote yanayofanyika nchini, bila kujali yanafanywa na chama chake tawala cha CCM au wapinzani.

Hivi unategemea ni kiongozi gani mstaafu, angeweza kuya na ujasiri wa kuyatamka maneno kama aliyoyatamka Mwalimu Nyerere, kuwa angeweza kutoka CCM, iwapo tu chama hicho hakitasimamia Haki kwa watanzania wote, kwani huo ndiyo msingi wa chama hicho, toka uanzishwaji wake na anaendelea kusisitiza kuwa chama hicho siyo mama yake mzazi, ambaye Maisha yake yote hawezi kumkana, lakini kwa chama kuendelea kuwa mwanachama wake, ni kutokana na chama hicho kutoacha misingi yake.

Tujiulize kwa hawa wazee wastaafu waliopo hivi sasa, hivi hawaoni namna nchi inavyokwenda mrama, kwa namna inavyoendeshwa, kwa upendeleo wa waziwazi kwa wanaccm kupewa upendeleo na wapinzani wa nchi hii kuwa "treated" kama wahaini ndani ya nchi yao?

Hivi hawa wazee wastaafu hawaoni kuwa kwa watawala wetu kuzuia kufanyika shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani na kuruhusu chama tawala cha CCM kifanye shughuli zake za kisiasa bila bughudha yoyote ni ukiukwaji wa hali ya juu wa Katiba ya nchi yetu, ambayo inaeleza wazi kuwa nchi yetu itaendeshwa Katika mfumo wa vyama vingi?

Hivi kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai hivi leo, angekaa kimya kweli bila kukemea vitendo vya watawala wetu kuendesha nchi yetu kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?

Mwalimu Nyerere Katika moja ya hotuba zake amewahi kusema kukosolewa ndiyo njia pekee za watawala kujua pale wanapokosea ili wajirekebishe.

Hivi Katika nchi yetu hivi sasa kiongozi wa upinzani kukosoa mambo yanavyokwenda nchini, unakamatwa na kubambikiwa kesi ya ugaidi ndiyo utawala bora na unaozingatia sheria kweli?

Nchi yetu hivi sasa inazihitaji Sana hotuba za baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuliko wakati wowote uliopita.
 

inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
6,795
2,000
Zinaboa,porojo nyingi,matumaini kibao on field nothing,watu wanatumia sukari guru,majani ya mpapai Kama sabuni,gwanji,unga foleni
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
6,281
2,000
Kuna wosia wa baba kila siku alfajiri tbc radio. Kuwa mzalendo kwa kusikiliza radio ya taifa
 

Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,693
2,000
Mwalimu ndie msingi wa yote hayo nani wakosoaji wake aliwashughulikia kisiasa kwa kuwaweka kizuizini.Alifuta vyama vya upinzani.
Hotuba zake nyingi ni baada ya kustaafu na zilikuwa zikiuponda Utawala wake kwa mambo aliyoyafanya so zilikuwa zokitoa majibu ya Yale aliyofanya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom