Hotuba za Mwalimu Nyerere zinaishi kizazi hadi kizazi

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Tarehe 14 October tutaadhimisha siku ambayo Mwa Nyerere alitutoka duniani kwa wanainchi wa Tanzania kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kuchangia damu, kufanya usafi, kuwatembelea yatima na wajane, kufanya midahalo na makongamano n. k.

Lakini ukisikiliza kwa makini hotuba za Mwl Nyerere toka Uhuru mpaka anafariki hotuba zake zote zinaishi mpaka leo.

Kipaji cha hotuba kama hiki cha Mw Nyerere ni muhimu sana kwa viongozi wa leo kwani Hotuba za Mwa Nyerere zinafundisha, zinatoa maono,zinaonya,zinafurahisha na hata kutoa historia na hadithi na kujenga imani, mshikamano, utaifa na zaidi ulinzi wa mali za umma kupiga vita ukabila na udini.
 
Nyerere alikuwa akifika mahali anasema "sikupanga kuongea nanyi ila nitaongea huku ninafikiri"

"NITAONGEA HUKU NINAFIKIRI"
 
Back
Top Bottom