Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Jamani naomba mwenye audio au dvd ya hotuba ya Mwl. Nyerere aliposema CCM si chama cha baba yangu au mama yangu. Naomba uiweke hapa mtandaoni au kwenye youtube. Naomba yeyote anayefahamu naweza kuipata katika link gani basi anifahamishe.
 
Wana JF - Habari,
Ninaomba msaada kwa yeyote mwenye hotuba za mwalimu J.K Nyerere anipatie tafadhali. Au kama kuna link inayoweza kuwa na hizo speech. Please help.
 
Unaweza kuzipata kwa jamaa wa taasisi ya mwalimu Nyerere. DVD moja wanaiuza kwa sh 10,000=. Ninazo copy chache. Ni pm kama unataka nikutengenezee kopi.
 
YouTube unazipata nyingi sana. Bandika neno "Hotuba za Mwalimu" utazipata.
 
Maneno haya yalizungumzwa Kiongozi fulani ambae sasa ni Waziri.Aliyashusha kutoka kifuani mwake kuonyesha Msimamo wake wa kuwatumikia wananchi.Wananchi na Watanzania ndo watu wapekee wa kumfanya acheke,afurahi au akose furaha.

Mimi nawakumbusha Wana jamvi humu[CCM],Pamoja na Wengine kuwa kwa Mtu mwenye Utimamu sawia Hawezi kutetea Chama chake bali atawatetea Wale wanaopinga Dhuruma,wanaopinga Matumizi mabaya Ofisi za serikali,Wanaopinga Wizi wa tunu za taifa hili kwa maslah ya wachache ambao wako ndani ya vyama vyenye mkusanyiko wa Wazalendo wa kweli na Walafi.
Mtetee yule Mwenye msimamo na taifa hili,mtetee yule mwenye Maono ya kulibadili taifa,hakuna atakaezikwa na chama hapa,ila utazikwa na ujasiri wako,utetezi wako na N.k.

Nawakumbusha pia siasa za kupandikisha chuki kwa njia ya udini zitatugharimu sana....Na siku tukianza kuchinjana wenyewe Hakuna atakae toka ndani ya nchi hii.
Narudia tena hakuna aliezaliwa na chama wa kulelewa na chama,kila mtu amelelewa kwao.
By
CCM DAMU
 
Niko namsikiliza, anasema: "Rais wa Tanzania ni lazima atakuwa aidha Mtanganyika au Mzanzibar, na atachaguliwa kwa kuzingatia katiba ya Tanzania, na ataapa ili tuweze kumshitaki kama atavunja au kukiuka katiba. Hatutaki Rais anayeona haya kuitetea na kuilinda katiba yetu, huyu hatufai. Nchi zinaongozwa na watu kwa kuzingatia kanuni na sheria. Siyo mtu anapata ushauri kwa mkewe halafu kesho tunakuta jambo fulani linatokea, maana hamtaelewa kesho mkewe atamwambia nini. Zamani tulikuwa na vitu vinaitwa miiko ya uongozi , mojawapo ni rusha ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa". Mzee huyu utafikiri ni mnajimu
 
asante!
kwa keli nammis sana
enzi zile kwenye matamasha ilikuwa tunasubira hotuba ya Rais
sasa ikikaribia kunazima TV
 
I wish vigogo wote wangekuwa wanatazama na wanafanya kwa matendo hiki anachokisema.
Mungu atujalie cku moja tuwe tena na mtu kama Mwalimu Nyerere.Hivi tumbo la mama Afrika ndo halizai tena watu wa aina hii?Tutafakari!
 
"Watu wanaongelea majina, badala ya kusema matatizo yanayokabili nchi yetu, halafu baadaye ndio muangalie majina ya nani anaweza kutatua hayo matatizo ya nchi yetu"

"Ingekuwa ni majina tu basi tungekusanya majina tu halafu akachaguliwa kipofu mmoja achague jina lolote, halafu ampe mtu anayejua kusoma atusomee hilo jina"

-Nyerere
 
Very sad,
mali ndio kigezo
kwa sasa tunaogopa wagombea masikini kwani watakuwa na njaa sana,
roho imeniuma sana,
 
Anaendelea kwa kueleza: "Hapa Tanzania kwa sasa rushwa haina aibu, nchi inanuka rushwa. Tunataka kiongozi anayejua, kuamini na kufanya hivyo; na aweze kuwaambia kuwa Ikulu ni mahali patakatifu, sikuchaguliwa na watanzania kuja kupageuza pango la walanguzi!!! Uchaguzi siku hizi uchaguzi unakumbatia matumizi ya pesa.

Kutokusanya kodi ni sifa moja ya serikali zinazokula rushwa, serikali corrupt haikusanyi kodi, itabaki kufukuzana na watu wadogo. Huwezi kutumikia mabwana wawili, Mungu na Fedha. Siku hizi kulisemea azimio la Arusha inabidi uwe na moyo kama wa mwendawazimu. Azimio lile liweka miiko ya uongozi, lakini wenzetu wameenda huko Zanzibar wameliua, na hawajaweka mbadala, na matokeo yake mambo yanakwenda kiholela tu. Ameongeza kwa kusema hakuna serikali popote duniani inayoendeshwa bila miiko, na huwezi kupewa kaz
i ya nchi halafu unaendesha maisha ya kihuni".
 
ile hotuba ya mwl Nyerere ya masaa matano nani anayo, iko kwenye youtube? aliitoa chimwaga na komba alitunga wimbo
 
"zamani wakati wa uchaguzi mali zilikuwa ni disqualifications, lakini sasa kwenye uchaguzi mali ni qualifications" -Nyerere
 
Back
Top Bottom