Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Kusema ukweli nafarijika sana kusikiliza hotuba za baba yetu wa Taifa ila kwa masikitiko makubwa nashindwa kupata fursa hata ya kujua historia yake, je hivi serikali au Familia inaweza kufungua akaunti katika social network na Youtube channel ili waweze ku post maneno ya hekima ya mwalimu jk mfano Nelson Mandela, bob marley, 2pac shakur japo hatunao tena lakini bado tunapata quotes zao
 
Hili hata mimi huwa nalishangaa, kwanza ilitakiwa iwepo Library au center maalum ya Mwalim Nyerere na itangazwe, walitakiwa wawe na offical social network accounts , wana tupia vi picha hapo na ishu mbali mbali.
Cha kushangaza utaskia kuna taasisi ya mwalim Nyerere na kabisa wapo watu wenye Masters zao wana fanya kazi hapo, ndio ujinga wa wobongo.
Nyerere jina kubwa sana yet watu wanao simamia kumbu kumbu zake hawafanyi kazi ya maana kuiendeleza historia yake nzuri.
Wajifunze hata kwa mzee Mohammed said mbona wajomba zake walisaidia kupigania uhuru japo kidogo lakini jamaa ana wapa promo kubwa tu.
Yaan inasikitisha hatuna bunifu kwenye kumuenzi Rais Nyerere yaani hata Mugabe anatushinda kwenye kumkumbuka rais wetu wenyewe.
 
Nimekuwa nikifuatilia hotuba za viongozi wakuu wa nchi hii na nimegundua kuwa hotuba za Mwl Nyerere zina mvuto na uwezo wa kudumu au kutumika muda wote,yaani hotuba zake za miaka ya sitini au sabini bado ikirudiwa ni kama inaongelea kitu kinachofanyika leo au hata kukataza/kukemea kitu kinachoweza kufanyika kesho au miaka ijayo.Hii ni tofauti na warithi wake ambao hotuba zao zinaonekana ni za kukidhi haja ya muda mfupi tu kwani zikirudiwa baada ya mwaka mmoja hazionekani kuwa na uzito wala mvuto wowote.Nini siri ya mwalimu na hotuba zake?
 
Sasa kama hawa wengine horuba zao zina vibwagizo vya maneno

"Malofa na wapumbavu"
"Mwafwaaa"
"Ukitaka kula shurti nawe uliwe"

Unategemea nini???
 
Umeshindwa Kuandika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Hivi wewe ni Mtanzania kweli ?

inatakiwa ufungwe au unyongwe kabisa!
 
Poleni na miangaiko ya kutwa nzima. Wapi naweza kudowload hotuba za Baba wa Taifa nimemis sana mawaidha ya mhasisi wetu.
Natanguliza shukrani.
 
1. Ujinga
2. Ubinafsi Na Ufisadi
3. Ubepari
4. Ukabila Na Usehemu
5. Ubinafsishaji Holela Wa Mali Za Umma
6. Kuongozwa Kwa Rimoti Na Nchi Matajiri
7. Ubabe Na Vitisho Katika Uongozi
8. Umangimeza Na Ukiritimba
9. Usiri Wa Mikataba Na Makampuni Ya Kigeni
10. Rushwa
11. Uchu Wa Madaraka
 
Sasa haya yote watoto zake wa CCM wanayafanya walaaniwe fisiemu wote hawa watu walipaswa kuwa magerezani au kuzimu sio kuwa serikalini
 
Kama hii clip ni ya kweli, basi laiti viongozi wanao jinadi kumuenzi mwalimu wangefanya hivyo kwa vitendo; laiti wale wenye dhamana ya kuongoza Bunge wangetambua ukuu wa viapo walivyokula vya kuongoza mhimili huo; laiti wabunge wote bila kujali vyama vyama wangetambua kuwa wanabeba dhamana ya mamilioni ya wa Tanzania na sio maslahi kiduchu ya vyama vyao au maslahi binafsi ya viongozi wao!
 

Attachments

  • VID-20170730-WA0002.mp4
    1.1 MB · Views: 31
A. Umekumbuka zama zake?
B. Unatamani wayaishi maneno yake?
C. Nyumbani kunavurugwa?

Chagua jibu sahihi kisha ujaze kwenye nafasi iliyo wazi................
 
Ungesikiliza,ungetuwekea katika maandishi hiyo speech ya msimamo wa Hayati Mwl.
 
Back
Top Bottom