Hotuba za JK Bana

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Miundombinu pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya njia ya Reli ya Kati kwa kipindi cha muda mfupi ujao ili kuwezesha huduma za treni kuanza kazi mara moja.

Pamoja na kuagiza ukamilishaji wa kazi hiyo, amesema serikali italijenga tuta la mto Mkondoa ili kuwawezesha wakazi wa Kilosa kuendelea kuishi kwa usalama na kazi hiyo itaanza mara moja baada ya taratibu kukamilishwa.

Rais Jakaya Kikwete alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Mji wa Kilosa, wakiwemo na waathirika wa mafuriko wanaoishi kwenye kambi ya Mazulia, baada ya kukagua uharibifu wa miundombinu ya reli likiwemo daraja kubwa la reli katika Kijiji cha Mkadage, kilometa 10 kutoka mjini Kilosa.

“Nimekuja hapa kuwapa pole pamoja na kuangalia maisha yenu juu ya chakula, matibabu, maji na makazi ya muda mnayoishi. Lakini baada ya kukagua maeneo ya mafuriko ni kweli yamekuwa ni makubwa, hivyo serikali imeamua kulijenga tuta upya ili wananchi wa Kilosa muendelee kukaa kwa usalama na nitakaa na wenzangu kuona namna ya kuifanya,” alisema Rais Kikwete.

Kwa upande wa reli, alisema maji yasipungue ama kupungua, lazima njia ya reli ijengwe na treni ifanye kazi yake mara moja ili kuwanusuru wananchi wa maeneo mbalimbali ya nchi. Kwa sasa, wasafiri wa reli hiyo wanalazimika kuanza safari zao za kwenda Bara kuanzia Dodoma.

Rais Kikwete alisema wanaoweza reli kufanya kazi yake ni wanajeshi, hivyo aliiagiza Wizara ya Miundombinu pamoja na JWTZ kushirikiana kwa karibu zaidi kujenga reli na madaraja hayo ndani ya kipindi kifupi kijacho cha wiki mbili.

“Reli lazima ipitike kwa muda mfupi ujao na katika mto huu (Mkondoa), daraja litengenezwe haraka kwa kuwa tayari serikali yote ipo hapa mjini Kilosa kuanzia Jeshi, Kitengo cha Maafa ya Waziri Mkuu, Red Cross (Msalaba Mwekundu) na wadau wengine, hivyo lazima kazi ifanyike,” alisema Rais Naye Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alisema Wizara yake itajitahidi kurejesha huduma za reli na barabara kwa kipindi kifupi kijacho ili kuwezesha usafiri uanze mara moja.

Tayari serikali imetenga zaidi ya Sh bilioni nane kwa ajili ya kurejesha miundombinu ya reli iliyoharibiwa na mvua za mafuriko yaliyotokea mkoani Dodoma na Morogoro, Desemba na Januari mwaka huu. Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amekiagiza Kitengo cha Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, kununua magodoro ya kutosha na kuyagawa kwa waathirika wa mafuriko wanaoishi katika makambi ya muda ya Mji Mdogo wa Kimamba, Kondoa na Mazulia, kutokana na kulala chini kwa muda mrefu bila ya magodoro.

Agizo hilo ni baada ya waathirika hao kumlalamikia Rais kuwa pamoja na kupata huduma mbalimbali zikiwemo za chakula, matibabu na maji, wamekuwa wakilala chini kwenye mikeka ama nailoni tangu wahamishiwe kwenye makambi ya muda na katika kambi maalumu zilizotengwa kutokana na ukosefu huo.

“Hapa tatizo lenu ni nini …yupo wapi Mwenyekiti wenu wa Kambi hii ya Kimamba…nielezeni ili nijue mnakabiliwa na tatizo lipi ili serikali iweze kulitatua,” alihoji Rais.

Hivyo kutokana na kuelezwa tatizo hilo ambalo ni karibu kwa makambi zote za muda ya Mazulia, Kondoa na Kimamba, Rais alimwagiza Ofisa Mratibu wa Ukame na Usalama wa Chakula, Harrison Chinyuka, ambaye yupo mjini Kilosa, kuhakikisha magodoro yanapatikana mara moja hata kwa kukopa kutoka kwa wenye viwanda vya utengenezaji wa magodoro hayo.

“Serikali haiwezi kushindwa kulipa …nendeni mkazumgumze na wenye viwanda vya kutengeneza magodoro, ingieni mkataba nao kwa ajili ya kulipana taratibu na yawafikie waathirika wote waliopo kwenye makambi haya,” aliagiza Rais Kikwete aliyefika Morogoro juzi kwa ziara ya siku mbili maalumu kutembelea Kilosa.

Pia alikitaka Kitengo hicho kuhakikisha wanawagawia mablanketi waathirika hao, wakati serikali ikiangalia uwezekano wa kununua vitanda ili wavitumie hadi wakatakapohamishiwa kwenye makazi ya kudumu.

Hata hivyo, aliagiza uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Kilosa, kutowahamisha waathirika waliopo katika eneo la Kondoa ambao wamejenga vibanda vyao kwa kutumia makuti na ifanye juhudi za kuwaboreshea maeneo yao hadi watakapogawiwa viwanja vya kujenga nyumba za kudumu.

Rais pia aliutaka uongozi huo kuwajengea mahema karibu na shule za sekondari wanafunzi ambao wanaishi kwenye makambi ya muda ili waishi karibu na shule zao kwa upande wa wasichana na wavulana sambamba na kuhakikisha usalama wao wa kimasomo.

Awali, Ofisa Mratibu wa Ukame na Usalama wa Chakula, Harrison Chinyuka alimwambia Rais kuwa Kitengo cha Maafa kimetenga bajeti ya Sh bilioni 18 kununulia vyakula, ujenzi wa nyumba na mahitaji mengine.

Alisema kwamba bajeti ya ununuzi wa magodoro na maji haikuingizwa awali, lakini kutokana na mahitaji ya mara ya pili, ofisi hiyo imepokea magodoro 1,000 na mahema 336 pamoja na vitu vingine muhimu.

Hivi redcross ni serikali nayo?Hotuba za JK bwana
 
HII kWELI NI KAZI YAKE JAMANI?
 
sielewi tatito nini kuna viongozi wengi ambao wangeweza kufanya kazii lakini wanamsubiri mpaka rais wa nchi aje achukue maamuzi
 
tunamheshimiwa mkuu wa nnchi ambae ameshindwa kuzigusa nyoyo zetu, hutuba zake zimejaa vijineno ambavyo kwa waenda taarabu ni maarufu kama mipasho.....aaah JK bana.
 
sielewi tatito nini kuna viongozi wengi ambao wangeweza kufanya kazii lakini wanamsubiri mpaka rais wa nchi aje achukue maamuzi

Pengine labda serikali nzima ina kiongozi mmoja tu. Waliobaki ni wenye vyeo tu lakini uongozi hakuna. Vinginevyo isingekuwa rahisi kwa kazi za mjumbe wa nyumba kumi kumi kufanywa na Rais wa nchi.
 
“Hapa tatizo lenu ni nini …yupo wapi Mwenyekiti wenu wa Kambi hii ya Kimamba…nielezeni ili nijue mnakabiliwa na tatizo lipi ili serikali iweze kulitatua,” alihoji Rais.

Alikuwapo Mkullo,RC,DC,DED...mpaka iwe yeye?huyo mwenyekiti wa kambi anaripoti kwa nani?
 
Ukisikia watu wasiokuwa nazo "Up-Stairs" huyu ni mmojawapo.

Mimi nilifikiri "RITES" ndio wamiliki wa TRC kwa sasa with 51%?

Wanajeshi na Miundo Mbinu wanaingiaje hapa?
 
This is very interesting, may be we review the contract terms on unforeseeable events like this.
 
Back
Top Bottom