HOTUBA za Bajeti Mbadala na Hali ya Uchumi nchini kutoka Kambi ya Upinzani Bungeni

Wewe CHADEMA ni wapiga kelele tu na watu walioshindwa na wanataka kutoka kwa mgongo wa siasa. no way hakuna kitu. CHADEMA.
Mbona hatuelewani kwani serikali ya ccm Haijawahi kusaini mikataba ya madini au yote ilsainiwa kabla ya ccm jibu hoja mkuu naona unakwepa kiccm tu kwi kwi kwi ah ha ha!!!!!!
 
Mbona hatuelewani kwani serikali ya ccm Haijawahi kusaini mikataba ya madini au yote ilsainiwa kabla ya ccm jibu hoja mkuu naona unakwepa kiccm tu kwi kwi kwi ah ha ha!!!!!!

Nimekupa mfano Mwadui Mine ilisainiwa kabla hata ya CCM. je wewe unaongela mgodi upi? au unaongea kitu ambacho haukijui? na utoe ufafanuzi je hiyo kulipa walimu, police madaktari nk mara hamsini itakuwaje sio kupayuka tu.
 
Zitto kabwe kazi imefanyika ni nzuri but its Silly Season akina Nchemba watalaaniwa tu na dharau hizi kwa umma wawatanzania
 
kwa hiyo hatujui kusoma?,tumeisoma kwa makini imekaa vizuri,hata katiba mpya walisema cyo muda wake na aiwezekani
 
Nimekupa mfano Mwadui Mine ilisainiwa kabla hata ya CCM. je wewe unaongela mgodi upi? au unaongea kitu ambacho haukijui? na utoe ufafanuzi je hiyo kulipa walimu, police madaktari nk mara hamsini itakuwaje sio kupayuka tu.
Kahama, buzwagi mererani na mingine ni serikali ya Chama gani ili saini?
 
Annael acha dhiaka na unacheka uoni ata aibu,hee jamani cjui ujawahi kushida njaa au ujasikia watz wanaoshinda njaa..pole sana
 
Nimekupa mfano Mwadui Mine ilisainiwa kabla hata ya CCM. je wewe unaongela mgodi upi? au unaongea kitu ambacho haukijui? na utoe ufafanuzi je hiyo kulipa walimu, police madaktari nk mara hamsini itakuwaje sio kupayuka tu.
Tanzania has become one of the fastest-emerging gold producers in Africa, and is now the contient's third-largest gold-producing country after South Africa and Ghana. Annual production of gold has increased from around 43.2 t in 2002 to about 48.0 t in 2003. Based on ongoing projects and developing mines, Tanzania's estimated gold reserves have been calculated at a conservative total of Tanzania now has proven gold reserves in excess of 36 Moz (1000 t). In 2003 Tanzania reported a 20% increase in gold exports from US$414 million to US$504 million and accounted for more than 62% of total export revenues, compared with 49% in 2002. There was a tremendous increase in gold exports which resulted in the signing of another gold-mining contract, this time between the Government of Tanzania and Pangea Minerals Ltd. The contract will pave the way for mining at Tulawaka in the Biharamulo District, Kagera Region, in the Lake Victoria goldfields. The Tulawaka mine is expected to come on stream in early 2005. It will be the sixth large-scale gold mine to come into production in Tanzania within six years.
Each year since 1998, a new gold mine has been opened in Tanzania. The mines are owned by Resolute Ltd; Ashanti Goldfieldsin joint venture with AngloGold; Barrick Gold Corp; Placer Dome Inc; Meremeta Ltd; and Pangea Goldfields Inc in joint venture withMiniere du Nord.
AgloGold Ashanti owns 50% of the Geita mine in Tanzania. The mine which started production in August 2000 produced a record 661,045 oz at a cash operating cost of US$170/oz in 2003, compared with 579,043 oz at US$163/oz in 2002. The upgrade of the crushing and leach tank sections of the processing plant was successfully commissioned in the first quarter of 2003 and the capacity of the plant was increased from 4 Mt/y to 5.6 Mt/y.
 
Hii bajeti mbadala iliyoandaliwa na Kambi ya upinzani bungeni ambayo inaongozwa na Chama cha Chadema ambacho kinatazamwa kama Chama mbadala chenye nguvu kuchukua dola nchini hii ni dalili kwamba wanajiandaa vema kama Nyerere alivyosema kazi ya kujandaa kuchukua nchi ni bungeni kwanza.
 
WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe jana aliwasilisha bungeni bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani kwa mwaka wa fedha 2012/2013, huku akibainisha kasoro lukuki katika bajeti ya Serikali ilioyowasilishwa Alhamisi iliyopita.Bajeti ya Zitto ilitanguliwa na hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Rais – Mipango, Christina Mughwai ambaye pia aliweka wazi kile alichokiita udhaifu wa Serikali katika kuitekeleza mipango yake ya kiuchumi, hali ambayo inasababisha umaskini kwa wananchi.

Hotuba zote mbili, ya Zitto na Lissu, zilisema licha ya Serikali kutangaza kwamba bajeti ya 2011/12 ilikuwa ya kupunguza makali ya maisha, hakukuwa na nafuu yoyote kwa wananchi kwani maisha yameendelea kupanda.

Pamoja na kupendekeza njia kadhaa za kupanua wigo wa mapato ya Serikali, wapinzani wametaka kufanywa kwa ukaguzi wa deni la taifa, ili kubaini chanzo cha Serikali kukopa na kuweka wazi jinsi fedha hizo zilivyotumika hadi kufikia Sh22 trilioni.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni katika hotuba yake alisema mapato ya Serikali yanaweza kuongezwa kwa Sh2.885 trilioni, hivyo kupunguza utegemezi wa mikopo ya kibiashara ambayo imekuwa ikiligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha.

Vyanzo vya kodi na kiasi cha fedha kwenye mabano alivyopendekeza ni marekebisho ya kodi za misitu ikiwamo mkaa (Sh130.8 bilioni), Kupunguza misamaha ya kodi, kuzuia ukwepaji kodi na udanganyifu wa biashara ya nje (Sh742.74 bilioni), Mauzo ya hisa za Serikali (Sh415.55 bilioni), Marekebisho ya kodi Sekta ya Madini na asilimia 25 ya Mauzo ya Madini Nje (Sh578.36 bilioni) na Marekebisho ya Kodi na Usimamizi bora wa Mapato Kampuni za Simu (Sh502.26 bilioni).

Mapendekezo mengine ni Marekebisho ya Kodi ya Tozo ya Kuendeleza Stadi (Sh243.52 bilioni), mapato ya wanyamapori (Sh61.64 bilioni), kuondoa msamaha wa ushuru wa mafuta kwa kampuni za madini (Sh44.9 bilioni), Usimamizi wa mapato ya utalii (Sh51.75 bilioni), Kuimarisha biashara Afrika Mashariki (Sh 114.15 bilioni).

Zitto alisema kama wapinzani wangekuwa madarakani wangekusanya kiasi cha Sh15 bilioni sawa na ile ya Serikali, lakini tofauti ni hatua ya kutenga asilimia 35 ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi wa bajeti kutoka asilimia 42.37 za Serikali hadi asilimia 21.3.

Deni la Taifa

Kuhusu deni la Taifa, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema Serikali haipaswi kuendelea kukopa, kwani taarifa rasmi za kibenki na ukaguzi wa hesabu zinaonyesha kwamba deni hilo linakua kwa kasi tofauti na maelezo ya Serikali kwamba linahimilika.

"Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kuongezeka kwa asilimia 38 kutoka Sh10.5 trilioni mwaka 2009/2010 hadi Sh14.4 trilioni 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Deni la Taifa limefikia Sh20.3 trilioni mpaka ilipofika mwezi Machi mwaka 2012,"alisema Zitto na kuongeza:

"Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia Sh22 trillion. Suala hapa sio ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikali, bali ni kwamba tunakopa kufanyia nini?"

Alisema hesabu za bajeti ya Serikali ya 2012/13 inayopendekezwa zinaonyesha kwamba Serikali bado ina mpango wa kukopa kwa ajili ya kugharamia matumizi ya kawaida ambayo hayazalishi wala kutozwa kodi.

"Hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari n.k. Tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi," alisema.

Kuhusu mfumuko wa bei, Zitto alikosoa hatua zinazopendekezwa na Serikali kukabiliana nao, kwamba ni zile zilizoshindwa katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka huu.

Source: Mwananchi. ([url]www.mwananchi.com)[/URL]
 
thx kwa kuiweka bujeti mbadala,ngoja niisome kwa umakini kisha nifanye comparison na ya mgimwa then nitarudi kutoa maoni yangu baadae
 
kweli hii ndio bajeti ya Wananchi.. watoe majibu ya vingele vya maswali waliyoulizwa kabla hatujaanza kuijadili hasa fedha zilizotengwa kwenye maendeleo na hazikufika.
 
Ni wazi CUF hawakubaliani na bajeti ya kambi ya upinzani make mbunge wao mmoja kasema wanayo ya kwao kaandaa prof Lipumba na kaomba waruhusiwe kuiwasilisha.

Ile iliyosomwa na Zitto inaonekana ni yake na wabunge wachache sana wa CDM, nasema hivo make ukisikia wachangiaji wa CDM walio wengi hawafanyi reference kwenye bajeti yao zaidi wanaponda ya serikali na kutupiana vijembe vya kisiasa.

Zitto anaonekana hakuwashirikisha wenzake wengi, alijikalia tu na marafiki wakaja na bajeti yake, pengine ndo maana hata ilikuwa na makosa mengi yaliyomlazimisha kurekebisha.
 
Rafiki yangu Mzee Mwanakijiji tofauti iko kwenye vyanzo vya mapato; bajeti mbadala imeondoa kabisa mikopo ya kibiashara na kuongeza makusanyo ya kodi ili kugharamia miradi ya maendeleo.

I know that lakini bajeti zote zina assume kuwa nchi yetu inaweza kupiga hatua ya haraka ya maendeleo kwa bejeti ya trilioni 15 (iwe ni matumizi ya kawaida na ya maendeleo). Katika hili CDM inaonekana wanaamini kama CCM kuwa bajeti ya trilioni 15 inaendana na mahitaji yetu kama taifa. Nilitarajia bajeti mbadala ingekuwa inagusa kwenye trilioni 50 hivi!!
 
Wakuu,nilikuwa napitia bajeti ya kambi ya upinzani,nikaona nisiwe mchoyo kuwapongeza kwani wameangalia pato la mnyonge!
 
Siku mliobandika hili bandiko, mkipitia huko juu, niliwaainishia kuwa mbona kuna mapato "0", mkashindwa hata kurudia kuitafakari japo kidogo post yangu, mgeifanyia kazi mkaenda kutengenezaa addendum, msingeumbuka kama mlivyumbuliwa leo na Mheshimiwa Ngeleja, mkaumbuliwa na huu ushauri wenu uchwara usio na mapato.

Na leo, Mbowe akaadhiriwa akiitetea na kusoma ukurasa wa 35 wakati anaambiwa hayo yamo kwenye ukurasa wa 34, dah, mkuu wa upinzani bungeni anapojaribu kuchakachuwa!, akakuta kastukiwa hapo hapo, ni aibu kubwa sana sana mpaka Lissu akaamuwa kusimama na kumtetea bosi wake kwa kukiri kuwa sisi tunachotoa ni maoni tu, lakini bajeti ni hiyo ya Serikali. Wabunge wa CCM wote wakashangilia, akaoneshwa Lissu anacheka na Mbowe anacheka kwa fedheha ya kustukiwa.

Sasa jamani, haya ni maoni? hivi mnashauri nini wakati hamjui hata mapato yaliopo?

Wapinzani msiwe hivi, tunategemea nyie ndio muwe vivuli lakini kwa huu ushauri wenu mmekuwa "0" Kiza kitupu. Poleni sana.
 
Nimeipitia, juu huko inasema tunataka fedha za wahisani ziwekeze sio zitumike kwa matumizi ya kawaida, chini kwenye jedwali pesa za wafadhili kwenye maendeleo ni 0.

What a contradiction.

Ulinishutumu bure, kiko wapi? inabido uniombe msamaha nauamini kuwa "bichwa" langu linafanya kazi kuliko lako:

quote_icon.png
By Kaa la Moto

Bichwa lako kabla halijafikiri na mimacho yako kabla ya kusoma umeweka komenti. Una uji kichwani wewe.
Ngoja wengine tusome na kudadamvua kabla ya kuja na komenti.

Nikakujibu Hivi:

Nimeipitia, juu huko inasema tunataka fedha za wahisani ziwekeze sio zitumike kwa matumizi ya kawaida, chini kwenye jedwali pesa za wafadhili kwenye maendeleo ni 0.

What a contradiction.

Yaliyojiri ni kuwa siku ya pili tu hilo kosa likatumiwa vilivyo na CCM mpaka ikabidi waziri kivuli aombe radhi eti kosa la "taipu" (nayo ni uongo vile vile na ushahidi nnao). Msingenishutumu mkalifanyiia kazi haraka haraka mngewahi kufanya addendum siku hiyo hiyo na kuiwasilisha bungeni mapema, kabla mjadala wa bajeti haujaanza, siku zingine msiwe mnapinga tu kila kitu, kuna mi "bichwa" mingine ina uzoefu.
 
hii bajeti ya upinzani iliyosomwa na zitto nzuri sana ndo maana wassira alikimbilia kusema zitto kaiba point kwa mgimwa
 
Back
Top Bottom