Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Ninaandika nikiamini bila shaka yoyote kuwa hotuba za baba wa taifa zinafaa sana kutumika katika kufundisha somo la uraia katika shule zetu za msingi, sekondari na vyuo.
Hotuba za Nyerere zinapenya na kuleta msisimko wa kupenda nchi. Zinajenga na kuelekeza watanzania kufanya mema kwa ajili ya nchi yetu. zinaleta moyo wa umoja badala ya utengano. Ni wakati muafaka kwa wizara ya elimu kulifanyia kazi wazo hili ili kuandaa watanzania wenye uzalendo na nchi badala ya kutengeneza mafisadi. Hotuba zichambuliwe na kuamua zitakazotumika shule ya msingi, sekondari na ikiwezekana vyuo vya cheti. Najua kutakuwa na changamoto ya vifaa vya kufundishia lakini maandalizi yakifanyika inawezekana.
Kwa vile wanachama wa JF tunauwezo wa kuunganisha nguvu za ushawishi, basi tunaweza kufanikisha suala hili kwa manufaa yetu ya sasa na vizazi vijavyo.