Hotuba ya Zitto Kabwe, katika mkutano wa Halmashauri kuu ya taifa ya ACT Wazalendo, 02 Machi 2020 katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada Dar

Suphian Juma

Verified Member
Apr 2, 2019
67
400
HOTUBA YA KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO NDUGU ZITTO ZUBERI RUYAGWA KABWE, MB KATIKA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA TAREHE 2 MACHI 2020 KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA LAMADA JIJINI DAR ES SALAAM.

Ndugu Mwenyekiti wa Mkutano,
Ndugu Mshauri Mkuu wa Chama,
Ndugu Naibu Kiongozi wa Chama,
Ndugu Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mkutano huu wa Halmashauri Kuu ya Chama Taifa unakutana kwa sababu maalumu chache katika kutekeleza Katiba ya Chama chetu. Ni wajibu wa kikao hiki kuandaa Mkutano Mkuu wa Chama ambao tayari umetangazwa kuwa utafanyika tarehe 14-16 Machi mwaka 2020.

Pamoja na mambo mengine ya kikatiba kikao hiki kitafanya uteuzi wa wagombea wa ngazi za kitaifa katika Uchaguzi Mkuu wa Chama kwani uongozi wa sasa wa Chama unamaliza muda wake wa miaka mitano mwiwshoni mwa mwezi huu wa Machi, 2020.

Vile vile Mkutano huu utapokea Taarifa ya Azimio lake la kupitia upya Katiba ya chama chetu ili kufanyia marekebisho iendane na kwanza sheria mpya ya Vyama vya Siasa na pili mazingira ya sasa ya kisiasa nchini ikizingatiwa ukuaji wa kasi wa cham chetu Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Ninawaomba wajumbe wa Mkutano huu wa Halmashauri Kuu ya Chama Taifa kutimiza wajibu huu kwa weledi mkubwa na kwa kuzingatia maslahi mapana ya chama chetu na nchi zetu zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chama chetu ni chama kikubwa sasa, ndio chama pekee cha Siasa cha Upinzani nchini ambacho kina uhakika wa kuwa kwenye Serikali katika moja kati ya Serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – ama kama Chama kiongozi katika Serikali hiyo au Chama mshiriki. Hivyo ni muhimu sana maamuzi yetu tunayoyafanya kuanzia sasa yazingatie kuwa Sisi sio Chama tu, bali ni chama kitakachoongoza Serikali katika kuleta mabadiliko ya maisha ya Wananchi.

Mkutano huu utajadili mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Chama chetu kutokana na Azimio la Halmashauri Kuu ya chama. Kikao cha Kamati Kuu tayari kimetafakari maboresho ya Katiba na wajumbe wa Kamati Kuu kwa umoja wao watatetea hoja zao mbele yenu leo.

Ninawaomba wajumbe wa Halmashauri Kuu kutafakari kwa kina mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na Katiba bora itakayoweza kuhakikisha kuwa chama chetu ni kimoja na kinatimiza shabaha yake ya kuunda Taifa imara, lenye demokrasia na Tanzania yenye uchumi unaopaa na yenye watu wenye Raha na Furaha. Ninawasihi sana Wajumbe muwe makini kuhakikisha kuwa Katiba yetu inazingatia kujenga taswira ya Chama kinachozingatia uwiano wa kijinsia na uongozi wenye sura ya kitaifa.

Katika mazingira ya sasa ya Siasa ya Dunia huwezi kumweka pembeni Mwanamke hivyo ni muhimu Katiba yetu kuweka mazingatio ya Uwiano wa kijinsia katika uongozi wa ngazi zote za Chama. Vile vile ni muhimu sana Katiba yetu kuweka mazingatio ya kuwa na chama chenye Sura ya Kitaifa ili kila Mtanzania na kila Mzanzibari ajione kuwa anawakilishwa na Chama hiki.

Mkutano huu utafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za juu za Uongozi wa Chama. Huu ni wajibu mzito kwetu. Ninawahisi sana muongozwe na misingi ya Haki na Demokrasia. Ni muhimu sana chama chetu kijenge utamaduni wa kushindana kwa misingi ya kidemokrasia. Mpaka sasa zoezi la uchaguzi limekwenda vizuri na linatia moyo sana. Hakuna mgombea ambaye amenyimwa fomu za kugombea, aliyetengwa na watendaji wa chama wala aliyezuiwa kwa namna yeyote. Tuendelee hivi. Kila nafasi ya Chama ni lazima igombewe ilimradi tu wagombea wawe na sifa stahiki, wasio na tabia za kugawa chama na wenye dhamira ya dhati ya kukipeleka chama kwenye ushindi katika uchaguzi.

Narudia nasaha zangu kuwa nyakati za sasa za Siasa za dunia zinataka vyama kuzingatia uwiano wa kijinsia katika uongozi. Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa Wanawake wanachukua nafasi za Uongozi wa Chama. Nirudie kusema kuwa, kama Kiongozi wa Chama hiki, nisingependa kuona wagombea katika uchaguzi wa ndani ya chama wanabaguliwa, wananyanyapaliwa au kuwekewa mazingira magumu.

Kila mwanachama wa chama atakayepitishwa na vikao vya chama kuwa mgombea anafaa kuwa Kiongozi wa Chama chetu, hivyo kila mgombea apewe nafasi sawa na kuwe na uwanja sawa na haki itamalaki. Demokrasia tunayoihubiri nje tuanze kuitekeleza ndani ya Chama.

Hata hivyo, usalama wa Chama lazima uzingatiwe. Kwa hiyo mgombea yeyote atakayefanya kampeni zinazojenga chuki miongoni mwa wanachama, zinazokigawa chama kwa maeneo, dini, upande wa muungano, jinsia, kabila nk hafai kuwa kiongozi wa chama chetu. Kama kuna mgombea ambaye anafanya haya niliyoyataja dhamira yake imsute kwani huwezi kufanya kampeni kwa kuwagawa wanachama halafu utegemee kuongoza chama kwa kuwaunganisha wanachama. Ukifanya kampeni kwa ubaguzi, utaongoza kwa kubagua.

Tuondoke hapa na kaulimbiu kuwa TUCHAGUE MMOJA, TUBAKI WAMOJA. #TuchagueMmmoja #TubakiWamoja

Ndugu wajumbe, baada ya maelezo hayo kuhusiana na wajibu wenu wa kikatiba niseme machache ya jumla lakini muhimu sana.

Huu ni Mwaka wa Uchaguzi – Kampeni ya Tume Huru ya Uchaguzi ni Lazima

Tulipokutana mara ya mwisho tulikuwa tunajiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Nyote mlishuhudia namna gani mchakato wa uchaguzi ule uliporwa na wananchi kupokwa haki yao ya kuchagua viongozi wao. Mazingira yale yale ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio tunayokabiliana nayo kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwa chaguzi zote mbili, Uchaguzi wa Muungano na Uchaguzi wa Zanzibar.

Tunakabili vipi vikwazo hivi vya Uchaguzi ni jambo muhimu kwa Halmashauri Kuu kutafakari kwa kina na kushauri Uongozi wa Chama kufanya. Hivi karibuni nimefanya ziara ya awamu ya kwanza kwa mataifa mbalimbali duniani nikiwa na Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Fedha Ndg. Nassor Mazrui. Tumeyaeleza mataifa mpango ambao watawala wa Tanzania wanao wa kugeuza nchi yetu kuwa ya Chama kimoja. Hata hivyo Mataifa ya Nje hayawezi kusaidia kama sisi wenyewe hatujajiandaa kujisaidia.

Ninashauri Halmashauri Kuu ya Chama iazimie kuwataka wanachama wetu kote nchini kuongeza juhudi katika kampeni ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi. Bila Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa ni vigumu sana sana kuhami demokrasia yetu. Sisi Viongozi tutaendelea kutumia kila jukwaa tupatalo kupigania Uchaguzi wa Huru, Haki na unaoaminika. Ninyi Viongozi wa mikoa pia tumieni majukwaa huko mikoani na majimboni na kuendeleza kampeni hii ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi.

*Dunia imekumbwa na Virusi vya COVID19 ( Virusi vya Korona ):*

Tangu mwanzoni mwaka huu dunia imekumbana zahma ya virusi vya korona ambavyo sasa vimesambaa nchi nyingi duniani. Mpaka sasa Tanzania haijapata mtu ambaye ameambukizwa lakini kuna maelfu ya Watanzania wanaoishi nchini China na kwengine Duniani ambao wapo hatarini. Kuna Wanafunzi wa Kitanzania nchini China ambao wanaishi katika tahadhari kubwa. Kwanza kama Chama tunawaombea kwa Mungu awaepushe na mtihani huu na pili kuitaka Serikali iendelee kuwa na mawasiliano ya karibu na Watanzania hawa ili kuweza kuwapa msaada pale itakapohitajika.

Halmashauri Kuu ya Taifa iazimie kuitaka Serikali kujiandaa kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu kwani ni hatari na kwa nchi zetu zinazoendelea zenye mifumo goigoi ya afya ni muhimu sana KINGA kuliko kukabaliana na changamoto za TIBA.

Jambo ambalo halitazamwi kwa sasa ni madhara ya uchumi yatakayotokana na virusi hivi. Nchi ya China ambayo imeathirika sana na virusi hivi ni Uchumi wa pili Duniani kwa ukubwa ikiwa na GDP ya USD 12 Trilioni na ikiwa nchi ya tatu kwa wingi wa mauzo Nje (exports ). China inauza bidhaa na huduma nje sawa na 10% ya bidhaa na huduma zote zinazouzwa duniani. Kwa vyovyote vile madhara ya virusi hivi katika uchumi wa Dunia ni makubwa sana.

Kwa Tanzania madhara yaweza kuwa kwenye Mapato ya fedha za kigeni kupitia utalii na mapato ya Serikali kwenye kodi. Tanzania inaagiza kutoka China 27% ya bidhaa zote inazoagiza kutoka nje.

Mwaka 2019 Tanzania iliagiza bidhaa zenye thamani ya USD 10 bilioni kutoka nje na katika hizo bidhaa zenye thamani ya USD 2.68 Bilioni zilikuwa ni kutoka China. Kodi za bidhaa kutoka nje ( taxes on imports ) zinachangia 40% ya Mapato ya Kodi kwa Serikali.

Hivyo madhara ya virusi vya korona yataonekana katika mapato ya Serikali. Ni muhimu Serikali kufanya uchambuzi wa kina wa madhara ya kiuchumi kufuatia virusi hivi na kuandaa mikakati ya kukabiliana na hali hiyo ili kulinda uchumi wa Tanzania. Halmashauri Kuu ya Chama iazimie kuitaka Serikali kufanya uchambuzi huo na kuwaeleza wananchi hatua wanazopaswa kuchukua kudhibiti madhara hayo.

Ndugu wajumbe,

Baada ya maelezo hayo nawatakia kila la kheri katika Mkutano huu wa Halmashauri Kuu ya chama.

ACT WAZALENDO,TAIFA KWANZA LEO NA KESHO.

Asanteni sana.
IMG_20200302_142445_983.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
3,780
2,000
Bado CDM inakubalika zaidi ni vyema tukawa na vyama vingi imara kwa checks and balance.CCM wanahaha wakijua wapo Watanzania makini na vyama wanafatilia 24/7 kila jambo.Hongera ACT kujipanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Zitto 2020 Uchaguzi atasumbua sana, na kama akipata "BACK UP" kutoka kwa Bernad Membe na vyama vya upinzani (Lissu akiwa miongoni mwao) basi CCM wana kazi si ya kitoto.

Kwanza ndio kiongozi pekee wa upinzani kwasasa anaeeleweka, ana strategy nzuri ya kupambana na CCM. Viongozi wengine wa upinzani wanakazania kupiga kelele za kuonewa na wanasahau strategy nyingine.

Zitto anapambania "UONEVU" nje ya nchi kwenye mataifa yalioendelea na kuweka diplomasia ya ACT vizuri nje, halafu ndani ya nchi anapambania "KUREKEBISHA WATAWALA KWA UTENDAJI KAZI WAO MBOVU NA MAENDELEO YA TAIFA".

CCM (Utawala Huu) hawajahangaika kuweka maelewano na mataifa ya nje vizuri, na wanazidi kuharibu diplomasia na nchi za nje kila kukicha. Na hawajali. Hili ni kosa kubwa miongoni mwa waliofanya utawala huu ki-strategy. Likifuatiwa kuharibu vibaya sana "TASWIRA NA IMANI "YA RAIA/WAFANYA BIASHARA/WAWEKEZAJI/WALIMU" VS "SERIKALI").

Mgombea yoyote wa CCM hatoweza kuwashawishi WALIMU/WAWEKEZAJI/WAFANYA BIASHARA kwenye uchaguzi huu wamuelewe, sambamba na raia wa hali ya chini. Hana jinsi zaido ya kuja kutumia "NGUVU au WIZI" wa kura (Kama hatobanwa na usimamizi wa UN, MAREKANI, UK, CANADA, SWEDEN - Ila akibanwa uchaguzi ufanyike wa huru na haki, basi kaumia vibaya sana).

CCM wasije wakapata wazo la kimfungulia mashtaka ya "UHUJUMU UCHUMI" Zitto wala Membe ili wawasweke ndani kipindi cha Uchaguzi Mkuu. Wataharibu vibaya sana nje na ndani ya nchi. Ni bora wapambane nao kwa hoja za msingi (Sio hoja zenye TB zinazotolewa na Profesa Polepole).

#Zitto 2020
#Bernad Membe 2020
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
4,653
2,000
Huyu ni failure wa kisiasa, hana mvuto! Mwaka huu yabidi ACT iinuke kwa mgongo wa Maalim!
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,420
2,000
Wazalendo Tanzania, Bara na Zanzibari
Haki tutapigania, kuleta yalo mazuri
Usawa haki na sheria ,kwa tajiri na dhalili
Nchi tunatarajia ,ACT kuongoza

Viongozi Madhubuti,Kubali kukosolewa
wanahimili mikiki, Jiwe alo tuletea
Hii nchi yetu sisi, Wewe watutumikia
Nchi tunatarajia ,ACT kuongoza

wako wasopenda haki,Ubaya kututakia
Zitashindwa zao laki, Mambo tawageukia
Ni mingi yao mikiki, Hatimae watalia
Nchi tunatarajia ,ACT kuongoza

Usawa sheria haki,iwe kwa wote raia
Uchumi kutamalaki ,Bila ya kubaguliwa
Elimu,biashara haki,Kilimo cha kumwagia
Nchi tunatarajia ,ACT kuongoza

Tanzania nchi yetu, kweli imebarikiwa
madini gesi misitu,bahari pia maziwa
Ni wapole watu wetu, Na wazuri wa Tabia
Nchi tunatarajia , ACT kuongoza

Dini zote zipo kwetu, bila ya kubagua
Huwajuwi watu wetu, Ipi dini kachagua
Utadhani wote ndugu, kumbe wamejitambua
Nchi tunatarajia , ACT kuongoza

Heri ninawatakia, Viongozi wote pia
Mola tawabarikia, Taifa kutuongozea
Mutuondeshee jua , kivuli kutuletea
Nchi tunatarajia , ACT kuongoza

Taifa liko hoi sana ,raia wote twalia
Si wakubwa si vijana, Hakuna alobakia.
Maisha yametubana, Hali zimenyog'onyea
Nchi tunatarajia ,ACT kuongoza

kalamu naweka chini, Mkutano kazi kwenu
Macho yote nchini , ACT yako kwenu
Wazalendo chagueni ,Kuongoza chama chenu
Nchi tunatarajia ,ACT kuongoza
 
LadyRed

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
8,148
2,000
Zitto 2020 Uchaguzi atasumbua sana, na kama akipata "BACK UP" kutoka kwa Bernad Membe na vyama vya upinzani (Lissu akiwa miongoni mwao) basi CCM wana kazi si ya kitoto.

Kwanza ndio kiongozi pekee wa upinzani kwasasa anaeeleweka, ana strategy nzuri ya kupambana na CCM. Viongozi wengine wa upinzani wanakazania kupiga kelele za kuonewa na wanasahau strategy nyingine.

Zitto anapambania "UONEVU" nje ya nchi kwenye mataifa yalioendelea na kuweka diplomasia ya ACT vizuri nje, halafu ndani ya nchi anapambania "KUREKEBISHA WATAWALA KWA UTENDAJI KAZI WAO MBOVU NA MAENDELEO YA TAIFA".

CCM (Utawala Huu) hawajahangaika kuweka maelewano na mataifa ya nje vizuri, na wanazidi kuharibu diplomasia na nchi za nje kila kukicha. Na hawajali. Hili ni kosa kubwa miongoni mwa waliofanya utawala huu ki-strategy. Likifuatiwa kuharibu vibaya sana "TASWIRA NA IMANI "YA RAIA/WAFANYA BIASHARA/WAWEKEZAJI/WALIMU" VS "SERIKALI").

Mgombea yoyote wa CCM hatoweza kuwashawishi WALIMU/WAWEKEZAJI/WAFANYA BIASHARA kwenye uchaguzi huu wamuelewe, sambamba na raia wa hali ya chini. Hana jinsi zaido ya kuja kutumia "NGUVU au WIZI" wa kura (Kama hatobanwa na usimamizi wa UN, MAREKANI, UK, CANADA, SWEDEN - Ila akibanwa uchaguzi ufanyike wa huru na haki, basi kaumia vibaya sana).

CCM wasije wakapata wazo la kimfungulia mashtaka ya "UHUJUMU UCHUMI" Zitto wala Membe ili wawasweke ndani kipindi cha Uchaguzi Mkuu. Wataharibu vibaya sana nje na ndani ya nchi. Ni bora wapambane nao kwa hoja za msingi (Sio hoja zenye TB zinazotolewa na Profesa Polepole).

#Zitto 2020
#Bernad Membe 2020
Upinzani sijui wanakwama wapi
The only way watatoka is if they unite
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
10,309

pecking order huko twitter electorate:

20200302_211732.jpg
 
Top Bottom