Hotuba ya Zitto iliyozaa hoja ya kura ya Kutokuwa na imani na waziri Mkuu Pinda. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Zitto iliyozaa hoja ya kura ya Kutokuwa na imani na waziri Mkuu Pinda.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Apr 20, 2012.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  MHE KABWE Z. ZITTO – MWENYEKITI WA KAMATI YA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA:

  Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote ambao wamechangia katika hoja hii na kutokana na muda sitoweza kuwataja majina wote kwa sababu inahitaji tupate muda wa kutosha kuweza kuzijibu hoja zote pamoja na majibu ambayo baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri wameyatoa.

  Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jambo moja ambalo Waheshimiwa Wabunge wamependekeza tuboreshe mapendekezo ya Kamati, pendekezo namba 7.2.7 kuhusiana na ukodishaji wa ndege wa Air Bus ambao ulifanywa na ATCL tarehe 27 Oktoba, 2007 na baadae Serikali ikatoa guarantee kinyume na sheria ya mikopo mwezi Aprili 2008 walitoa guarantee baada ya kuwa mkataba umeshaingiwa.

  Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge watatu waliochangia kwa maneno na wanne waliochangia kwa maandishi wakapendekeza kwamba Bunge liunde Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza mazingira kwa kuingia mkataba huo.

  Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunaendelea na michango nimepata taarifa, tulitoa taarifa kwanza Serikali haijaanza kulipa fedha zile kwenye Kampuni ya Wales Trading ya Lebanon. Lakini nimepata nyaraka ambazo zinaonyesha kwamba Serikali imeanza kulipa.

  Mpaka sasa tumeshawalipa shilingi bilioni 2.5, tumewatengenezea schedule ya malipo mpaka watakapokuwa wamekamilisha kuyalipa na ninayo hapa nitampatia Mheshimiwa Wazrri Mkuu aweze kuiona.

  Lakini linalonisikitisha ni kwamba tarehe 27 Machi, 2012 Maafisa wa Wizara ya Fedha walikutana na wawakilishi au wamiliki wa hii Kampuni Wales Trading ambayo walitukodishia ndege ambayo haikuruka na ambayo imetuingiza madeni makubwa sana na Waheshimiwa Wabunge na hasa Wabunge wa Mikoa ya Kusini naomba wanisikilize kwa makini watu hawa sasa katika nia ya kulipa deni hili wanapewa bandari ya Mtwara.

  Nina nyaraka hizi nitaziweka mezani na kuweza kumpatia Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa kutokana na mambo haya nakubaliana na mapendekezo ambayo Waheshimiwa Wabunge ambayo wameyatoa kwamba tuboreshe pendekezo namba 7.2.7 kwamba Bunge liunde Kamati Teule ili kuchunguza mazingira ya mkataba huu na mazongezonge mengine yote.

  Niwaambie tu kwamba Waziri wa Miundombinu aliishauri Wizara ya Fedha kwamba Wales wasilipwe, lakini Wizara ya Fedha imewalipa Wales hii inaonyesha mkanganyiko ambao uko Serikalini miongoni mwa Wizara. Kwa hiyo pendekezo hilo naomba lirekebishwe na litakuwa hivyo.

  Mheshimiwa Naibu Spika, la pili Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia kuhusiana na suala la special audit ya Consolidated Holdings.

  Special Audit
  ya Consolidated Holdings Corporation iko ndani ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwanza nimeshauriana na Wajumbe wenzangu wa Kamati tumekubaliana kwamba taarifa nzima ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ule ukaguzi maalum ufanyiwe kazi na Kamati na kwa ruhusa ya Wajumbe wa Kamati nimeunda timu ya Wajumbe watatu ambao watashughulikia suala hili ambaye ni Mheshimiwa Aliko Kibona, Mheshimiwa Esta Bulaya na Mheshimiwa Murtaza Mangungu na timu hii itaongozwa na Mheshimiwa Murtaza Mangungu na nitataka wamalize kazi hii ndani ya muda mfupi iwezekanavyo kwa ajili ya kuchukua hatua zinazostahili.

  Katika hili ushauri wangu ni kwamba kwa Mawaziri wote namna ya kuendesha Mashirika ya Umma naomba tufanye eyes on hands off kwa sababu ya kuweza kuepuka kuingilia Mashirika haya.

  Mheshimiwa Nundu amesema kwamba yeye ataingilia tu hata chooni sisi tutamwambia hapana, kwa sababu ya kutaka kuhakikisha kwamba Mashirika yetu yanaendeshwa kwa misingi inayotakiwa.

  Lakini lazima iwe eyes on kwa sababu pasipokuwa na eyes on madudu ya Mashirika yatakuwa makubwa sana. Kwa hiyo lazima ku-balance eyes on hands off msifanye micro managing, kwa sababu micro managing ndiyo ambayo inatuletea matatizo. Kuhusiana na Waziri wa Fedha ambaye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imemuonyesha dhahiri kwamba aliingilia na kufanya maamuzi kuhusiana na Shirika la CHC ajipime, ajione kama bado anastahili kuendelea kushikilia fedha za nchi yetu.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Bodi ya Pamba na maelezo Waziri wa Kilimo ameyazungumza na napenda nitofautiane naye Mheshimiwa Maghembe kwa sababu tarehe 17 jana nilisema tarehe 2, tarehe 17 Novemba, 2011 mmiliki mwenye Mashirika kwa niaba yetu Msajili wa Hazina aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya kuivunja Bodi ya Pamba ambayo ilikula fedha za wananchi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameshaonyesha kwamba fedha za wananchi zimeliwa.

  Waziri anasema kwamba anaomba mamlaka ya uteuzi iteue Mwenyekiti mwingine na hili ni kwa Mawaziri wote, tabia ya kumsingizia Mheshimiwa Rais katika kila jambo ambalo mnapaswa kulifanya ikome.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu Rais hayuko humu ndani ni rahisi sana kusema kwamba Rais hajafanya, Rais hajateua, suala la kuvunja Bodi ni mamlaka ya Waziri, uteuzi ni mamlaka ya Rais, Waziri anayo mamlaka ya kuweza kuvunja Bodi na kumtaarifu Mheshimiwa Rais ateue Mwenyekiti mwingine na ateue Wajumbe wengine na hatua zingine ziweze kuchukuliwa. Kwa maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Prof. Jumanne Maghembe ameyazungumza ni maelezo ambayo si sahihi.

  Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati sijayakubali na Bunge lichukulie tu kwamba yalikuwa yanapita tu kwa sababu ilikuwa ni lazima Wizara ichukue hatua, fedha za wakulima zimeliwa na tusifanye mchezo kabisa na hawa wananchi wa kawaida wa chini kabisa. Mheshimiwa Naibu Spika, suala la TBS limezungumzwa kwa kina sana. Lakini majibu hayajatosheleza.

  Hayajatosheleza kwa sababu kuna hatua ambazo ni lazima zichukuliwe. Sisi tulitoa taarifa tukampelekea Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Spika akatoa taarifa akampelekea Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa sisi hatufahamu kama Ofisi ya Waziri Mkuu haikupeleka taarifa ile kwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Maana Waziri wa Viwanda na Biashara anasema kwamba hakuwa na taarifa.

  Kwa hiyo anachokisema ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu anachokisema Ofisi ya Waziri Mkuu haikumpelekea taarifa na nyaraka zote ziko hapa kwa Spika. Kwamba baada ya taarifa yetu imekwenda na tulishauri kwenye uchunguzi Mkurugenzi Mkuu wa TBS asimamishe, apishe uchunguzi.

  Mbona ilikuwa ni rahisi sana kwa Mkurugenzi Mkuu wa CHC kusimamishwa tena bila kufuata taratibu. Lakini inakuwa ni vigumu sana kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS anayewafanya wakulima wetu watumie mbolea ambayo haina ubora, anayewalisha watoto wetu Blue band ambazo ni fake, anayeingiza matairi nchini ambayo yanasababisha ajari, inakuwa ngumu sana, lakini inakuwa rahisi kwa watu wengine.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilichokuwa nakiomba ni kwamba, maelekezo ya Mheshimiwa Spika, kwa Waziri Mkuu kuhusiana na TBS yatekelezwe na yatolewe taarifa Bungeni kwa sababu maelezo haya Mheshimiwa Spika ameshayatoa muda mrefu sana na ni zaidi ya miezi miwili sasa imepita toka Mheshimiwa Spika, ayatoe. Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho.

  Tatizo kubwa la Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutokutekelezwa ni ukosefu wa uwajibikaji; na kama nchi hii tunataka tuendelee, kama tunataka tupigane kwa dhati kabisa dhidi ya ubadhirifu, dhidi ya udokozi, dhidi ya uzembe, dhidi ya uvivu ni kuhakikisha tuna misingi sahihi ya uwajibikaji.

  Accountability
  , niliwahi kuwaambia vijana fulani kwamba kama kutakuwa kuna neno moja linalotakiwa liandikwe kwenye Katiba mpya, neno moja; ni 'accountability,' uwajibikaji na ndicho kinachokosekana.

  Taarifa hizi zinatolewa kila mwaka, nashukuru sana safari hii Wabunge mmekuwa wakali sana. Lakini bila kuhakikisha Executive inawajibika katika haya mwaka kesho tutarudia haya haya na tutakuwa wakali hivi hivi.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa taarifa kwamba; mimi na Bunge hili halina mamlaka ya Mkurugenzi wa Shirika, Katibu Mkuu wa Wizara au Mkurugenzi wa Halmashauri. Mawaziri ambao wametajwa kwa njia moja au nyingine kutokuwajibika ipasavyo na kuliingizia hasara taifa wamekuwa wagumu sana kuwajibika, wanampa kazi Rais ya kuwafukuza.

  Lakini sisi hatuwezi kuwaazimia hapa ila sisi tuna mamlaka na mtu mmoja tu humu ndani ya Bunge; na naomba mnisikilize kwa makini sana. Tuna mamlaka na mtu mmoja tu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, bila kumwajibisha Waziri Mkuu hawa Mawaziri waliotajwa hawatatoka na wasipotoka madudu haya yatarudia. Kwa hiyo Mbunge yoyote mwenye uchungu na ubadhirifu, Mbunge yoyote ambaye anakereka na watoto kwenye Jimbo lake kukaa chini, Mbunge yoyote anayekereka na madawa kuharibiwa na MSD na MSD kushindwa kupeleka madawa kwenye vijiji vyetu, nampa taarifa kwamba kuanzia kesho tunakusanya sahihi za Wabunge 70, ili siku ya Jumatatu tutoe hoja hapa Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, na kipindi hiki tunakitoa Mawaziri wote ambao wapo implicated kwenye taarifa hizi waweze kuona ama wao, au wamtoe rehani Waziri Mkuu.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wabunge wote wenye uchungu kuanzia kesho tutakuwa pale mlangoni, sahihi zinazohitajika ni 70 tu, kwa ajili ya kuleta hapa Bungeni na Wabunge wanahitajika kupitisha hilo azimio ni nusu tu ya Wabunge, 50 plus one. Tukifanya hivyo tutakuwa tumewapa heshima wananchi wetu, wataona kweli tumewatendea haki badala ya kupiga kelele bila ya kuchukua action.

  (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Wenyeviti wenzangu wote, Mheshimiwa Cheyo na Mheshimiwa Mrema nitoe hoja sasa kwamba Bunge lako lipokee taarifa za Kamati zote hizi tatu na mapendekezo yake na kuweza kuyapitisha. Naomba kutoa Hoja. (Makofi)

  Uncorrected Hansard 19th April, 2012
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona yatakuwa mambo ya Hansard haya!
  Ndo uzuri wa JF
   
 3. King2

  King2 JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pindwa Michozi inamdondoka saa hivi.
   
 4. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  taratibu barafu linayeyuka...bandu bandu humaliza gogo
   
 5. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kumfukuza kazi Waziri Mkuu siyo jawabu kwa tatizo kama hili. On the contrary,watu hao wakijiuzulu,hawatafutwi tena,wanaomdoka na hela walizoiba. Kwa sababu kujiuzulu kwao kunaonekana kwamba ni aibu tosha. Ni kama wezi wa Benki;wanaiba $6,000,000,halafu $500,000 is recovered,halafu wanapata light prison sentences,lakini most of the money is not recovered.
  Kamaunadai kuna ubadhiri katika Serikali,basi you have to take them by the horns watuhumiwa ,apprehend them.
  What I do not understand ni jinsi mwaka huu unaweza kusema 1,000,000,000sh. zimelipwa mishahara hewa. Halafu mwaka kesho,unauliza hivyo hivyo,''Kwa nini 1,000,000,000 sh. mishahara hewa imelipwa?''
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  so what is your point brother?
  Plse draw it down
   
Loading...