Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. V. Nahodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. V. Nahodha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Feb 23, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha Alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru

  Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha Alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru  Ndugu Waandishi wa Habari, kama mnavyojua Wizara ya Mambo ya Ndani ina jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao. Katika kipindi cha Miaka 50 iliyopita, Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaimarishwa. Ili Jeshi hili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo, limeanzisha Programu ya Miaka 10 ya Maboresho. Programu hii ambayo imeanza kutekelezwa mwaka huu ina lengo la kulijengea Jeshi la Polisi weledi, mazingira bora ya kazi na kuendeleza dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi. Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake ya kudhibiti na kuzuia uhalifu kwa kufanya doria na misako ya wahalifu mara kwa mara. Vile vile Jeshi la Polisi linashirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi kupambana na ujambazi. Kutokana na hatua hizi zinachukuliwa vitendo vya ujambazi na wizi katika mabenki, maduka na majumbani umepungua sana.

  Ndugu Waandishi wa habari, Hapana shaka Jeshi la Polisi linajitahidi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa tunakabiliwa na kasoro mbili. Kwanza, upelelezi wa makosa ya jinai unachukua muda mrefu jambo linaloathiri uendeshaji wa kesi Mahakamani. Tunaimarisha mafunzo ya upelelezi ndani na nje ya nchi ili kuwapatia Askari Polisi ujuzi wa kupleleleza makosa ya jinai. Pili baadhi ya askari hawasimamii kikamilifu majukumu yao. Kwa kupitia program ya miaka 10 ya maboresho Jeshi la Polisi linawaandalia viongozi waandamizi wa Polisi mafunzo ya Menejimenti ya Rasilimali watu. Lengo la mafunzo haya ni kuwapatia viongozi waandamizi ujuzi katika kusimamia mipango ya rasilimali watu, uajiri wa askari, upangaji wa malipo na posho, kutoa motisha na zawadi pamoja na kupima utendaji kazi. Kwa mawazo yangu tunapaswa kulipa uzitomkubwa suala la upimaji wa utendaji wa askari kwa sababu kazi usiyopima haiwezi kuwa na tija. Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kuhusu kuwepo kwa upendeleo katika kupandisha vyeo. Jambo hili lisiposimamiwa vizuri linaweza kuwakatisha tamaa askari wasiopandishwa vyeo lakini wanastahili kupandishwa vyeo kutokana na utendaji mzuri wa kazi. Kwa hiyo upimaji wa utendaji kazi ni kigezo kizuri cha kumpandisha mfanyakazi cheo.Ili kuwapa ari ya kufanya kazi askari wake, Jeshi la Polisi, limefanikiwa kuwaingiza askari wote katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuwawezesha kupata huduma za uhakika za afya, na familia zao. Halikadhaika, Jeshi la Polisi linajenga ghorofa 30 kwa ajili ya familia 120 katika Kambi ya Barabara ya Kilwa. Nyumba hizi zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 16/08/2011. Vilevile Jeshi la Polisi limejenga nyumba za askari katika mikoa ya Mwanza, Mara, Iringa na Kaskazini Pemba.

  Ndugu Waandishi wa habari, Wizara yangu pia ina jukumu la kuwahifadhi na kuwahudumia wafungwa na mahabusu. Ili kuwajengea wafungwa uwezo wa kujitegemea, Jeshi la Magereza linawapatia wafungwa mafunzo ya ushoni wa nguo, utengenezaji wa sabuni, uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mkonge na utengenezaji wa chumi. Shughuli nyingine zilizoanzishwa magerezani ni utengenezaji wa samani, na kilimo.Katika jitihada za kutumia nishati mbadala, Jeshi la Magereza limeanza matumizi ya makaa ya mawe katika magereza matatu nchini, ya Ruanda, Tukuyu na Songwe mkoani Mbeya. Utumiaji wa biogas umeanza katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Gereza Kuu la Ukonga. Kuhusu kuimarisha uoto wa asili uliopo kwenye maeneo ya Magereza, miti 3,701,594 imepandwa katika eneo la ekari 6,136 katika Magereza ya Malya, Bariadi, Isupilo Msalato na Idete kwa lengo la kuhifadhi mazingira.Halikadhalika, Wizara yangu inachukua imechukua hatua za kukabiliana na tatizo la wahamiaji haramu. Idara ya Uhamiaji inafanya misako pamoja na kutoa elimu kwa raia wanaoishi katika maeneo ya mipaka ili waweze kutoa taarifa kuhusu wahamiaji haramu. Nimeiagiza Idara ya Uhamiaji ishirikiane na viongozi wa Serikali za Mitaa na Polisi Jamii ili kupata taarifa za wahamiaji haramu kwa haraka.

  Ndugu Waandishi wa habari, Pamoja na mafaniko tuliyhoyapata Wizara yangu inakabiliwa na changamoto kubwa nne ambazo ni ujambazi, ajali za barabarani, wahamiaji haramu na msongamano katika magereza. Tunatumia mikakati mbalimbali kukabiliana na ujambazi. Kwanza, Wizara inaimarisha mafunzo ya operesheni, kuimarisha ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia na kuzitumia kuwatambua wahalifu. Pili, Wizara inafanya misako na doria za mara kwa mara na kuwashirikisha wananchi kupitia mpango wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi.

  Ndugu Waandashi wa habari, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaendelea kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na wananchi wote. Tutafanya hivyo kwa sababu Wizara yangu inaamini kuwa amani ni nyenzo muhimu katika kuleta maendeleo. Bila ya amani maendeleo hayawezi kupatikana na pasipo maendeleo hakuna amani. Kwa msingi huo, Wizara itaendelea kuwahimiza wananchi washiriki katika juhudi za kuimarisha amani na usalama kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili Taifa liweze kupata maendeleo zaidi.


  Ndugu Wadau hii ni sehemu ya Hotuba ya Mhesh. Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi katika kutimiza Miaka 50 ya UHURU wa Tanganyika..


  EEE MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU..........................


  Naomba kutoa hoja:


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!!
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kila kitu kipo kisiasa zaidi, kwani kama haya yanayotolewa katika hotuba ingelikuwa ni kwa vitendo sidhani kama hali ya usalama nchini ungelikuwa tete kiasi hiki.

  Kama Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma angelifanyia kazi taarifa toka kwa wananchi kuhusu mauaji ya kutisha sidhani kama yaliyotokea jana yangelitokea.

  kama kweli ulinzi shirikishi unatekelezwa kwa vitendo sidhani kama hali ya usalama ingelikuwa tete.

  Viongozi wetu sisi wananchi si kwamba tunakosoa sana na kulalamika sana, lakini mambo yanakwenda ndivyo sivyo katikautekelezaji.

  Ni wakati wa kuamka sasa TUFANYE KWA VITENDO NA TUACHE KUTUMIA MAKARATASI NA HOTUBA. NI WAKATI WA KUINGIA UWANJANI KUTEKELEZA KWA VITENDO. ILI TUDUMISHE AMANI NA KULETA MAENDELEO TANZANIA.
  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 3. D

  DOMA JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Peleka facebook me nilijua ya waziri mbadala lema
   
 4. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mambo ya Kizenji hayo. Huyu alifaa awekwe wizara ya utamaduni na michezo angetuletea vazi zuuri la taifa.
   
 5. s

  subash Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Boooonge la hotuba nakukubali Vuai Nooza
   
Loading...