Hotuba ya Waziri Mkuu Bunge la 12 Mkutano wa 7 Saba, Kikao cha 55, Juni 30, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973

Serikali yapiga marufuku michango shuleni
Serikali imepiga marufu michango kiholela katika shule za umma katika ngazi ya Msingi na Sekondari baada ya kuripotiwa kuwepo kwa michango mingi licha ya sera ya elimu bila malipo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Bungeni leo Juni 30, 2022, amesema:

“Serikali kupitia waraka wa elimu namba 5 na 6 wa mwaka 2015 umetoa maelekezo bayana ya elimu bila malipo ikiwemo fedha za utawala ambazo zinatolewa na Hazina na kwenda moja kwa moja katika akaunti za shule husika Msingi na Sekondari, kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, ukarabati, uendeshaji wa ndani na utawala

“10% ya fedha hizo utumika kwa gharama za umeme, maji na ulinzi, hivyo ninaagiza TAMISEMI na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote Nchini kufuatilia matumizi ya fedha hizo na kuhakikisha hakuna michango holela inayotozwa kwa Wanafunzi.

“Pia hakikisheni maelezo ya kujiunga na shule ya umma yanahakikiwa na kupewa hidhini ya katibu tawala wa mkoa husika na maafisa elimu wa Mkoa.”

Tunashukuru kwa taarifa mkuu, lakini hatufuatilii kwa sana habari za hilo bunge la majizi ya kura. Inshort bunge halina mvuto.
 
Serikali yapiga marufuku michango shuleni
Serikali imepiga marufu michango kiholela katika shule za umma katika ngazi ya Msingi na Sekondari baada ya kuripotiwa kuwepo kwa michango mingi licha ya sera ya elimu bila malipo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Bungeni leo Juni 30, 2022, amesema:

“Serikali kupitia waraka wa elimu namba 5 na 6 wa mwaka 2015 umetoa maelekezo bayana ya elimu bila malipo ikiwemo fedha za utawala ambazo zinatolewa na Hazina na kwenda moja kwa moja katika akaunti za shule husika Msingi na Sekondari, kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, ukarabati, uendeshaji wa ndani na utawala

“10% ya fedha hizo utumika kwa gharama za umeme, maji na ulinzi, hivyo ninaagiza TAMISEMI na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote Nchini kufuatilia matumizi ya fedha hizo na kuhakikisha hakuna michango holela inayotozwa kwa Wanafunzi.

“Pia hakikisheni maelezo ya kujiunga na shule ya umma yanahakikiwa na kupewa hidhini ya katibu tawala wa mkoa husika na maafisa elimu wa Mkoa.”

View attachment 2277363
Hakuna Kiongozi muongo kama Waziri Mkuu
 
Binafsi hapa nadaiwa ada karibu elfu 27 mchango wa shule mwalimu anaehusika na michango ananidai kama vile amenikopesha pesa zake mtoto wangu anamaliza darasa la saba pale mara hii. Mi nadhan hizi kauli za waziri mkuu ni lugha za ki-bungeni tu
 
Back
Top Bottom